Bendi  za Musiki wa Dansi zenye miondoko ya Ndombolo ya Solo, za Twanga Pepeta na Diamond Musica usiku wa kumkia leo zilifunika na kukonga nyoyo za wapenzi wa Muziki wa Dansi mjini Moshi wakati wakali hao wawili walipotumbuiza katika Tamasha kubwa la Burudani la Tusker Carnival lililofanyika katika Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Walikuwa ni Diamond Musica ndio walioanza kushambulia Jukwaa hilo la Tusker Carnival mishale ya saa mbili usilku hadi sita kasorobo walipo wapisha Wakongwe wa Burudani na Wabishi wa mjini Twanga Pepeta ambao walitikisa vilivyo Mji wa Moshi.
 
Tamasha hilo la Tusker Carnival lilianza juma lililopita jijini Dar es Salaam na baadae kupigwa jijini Mwanza huku Nguli wa Mziki wa dansi Koffi Antonio Olomide akiongoza mashambulizi. Leo ni zamu ya jiji la Mbeya ambao watapata burudani kali kutoka kwa Mapacha wa tatu na kundi la Extra Bongo chini ya Ali Choki.
 Kijana wa Mjini Moshi ambaye anakula Maisha jijini Dar es Salaam akiwa na kundi la Twanga Pepeta, Mkaanga Chips, Martin 'Kibosho' Shao akiwajibika katika idara yake ndani ya Tamasha lka Tusker Carnival.
 Huyu anajulikama kama Baloteli wa Bongo au Mbuyi Twitwe wa Twanga Pepeta akifanya vituko vyake katika jukwaa la Tusker Carnival mjini Moshi.
Palikuwa hapatoshi Uwanja wa Ushirika mtu nyomi zikifuatilia Burudani kutoka Tusker Carnival

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Du huyu mbuyu twite wa twanga anatumia mbavu nyingi. si mchezo nimecheka sana.ila poa sana twende kazi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...