
Walikuwa ni Diamond Musica ndio walioanza kushambulia
Jukwaa hilo la Tusker Carnival mishale ya saa mbili usilku hadi sita kasorobo
walipo wapisha Wakongwe wa Burudani na Wabishi wa mjini Twanga Pepeta ambao
walitikisa vilivyo Mji wa Moshi.
Tamasha hilo la Tusker
Carnival lilianza juma lililopita jijini Dar es Salaam na baadae kupigwa jijini
Mwanza huku Nguli wa Mziki wa dansi Koffi Antonio Olomide akiongoza
mashambulizi. Leo ni zamu ya jiji la Mbeya ambao watapata burudani kali kutoka
kwa Mapacha wa tatu na kundi la Extra Bongo chini ya Ali Choki.
Kijana wa Mjini Moshi ambaye anakula Maisha jijini Dar es Salaam akiwa na kundi la Twanga Pepeta, Mkaanga Chips, Martin 'Kibosho' Shao akiwajibika katika idara yake ndani ya Tamasha lka Tusker Carnival.
Huyu anajulikama kama Baloteli wa Bongo au Mbuyi Twitwe wa Twanga Pepeta akifanya vituko vyake katika jukwaa la Tusker Carnival mjini Moshi.
Palikuwa hapatoshi Uwanja wa Ushirika mtu nyomi zikifuatilia Burudani kutoka Tusker Carnival
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Du huyu mbuyu twite wa twanga anatumia mbavu nyingi. si mchezo nimecheka sana.ila poa sana twende kazi.
ReplyDelete