Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa hotuba ya ufunguzi wa jengo
la ghorofa kwa ajili ya makazi ya Askari Magereza mjini Iringa. Ufunguzi huo
uliambatana na sherehe kubwa ambayo iliudhuriwa na viongozi mbalimbali wa
serikali pamoja na maofisa wa Jeshi la Magereza. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini CGP John Minja
Bila kujali mvua
kubwa inayonyesha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak
Abdulwakil akiukata utepe akiashiria ufunguzi wa jengo la ghorofa kwa ajili ya
makazi ya Askari Magereza mjini Iringa.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (aliye vaa kiraia kushoto)
akifunua kitambaa kuashiria ufunguzi wa jengo la ghorofa kwa ajili ya makazi ya
Askari Magereza mjini Iringa. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini CGP John Minja.
Baadhi
ya sehemu ya nje na ndani ya jengo hilo pamoja na maafisa mbalimbali wa jeshi
hilo wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo hilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akipata maelezo wakati alipotembelea vyumba vya jengo hilo
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini CGP John Minja katika picha ya pamoja na maafisa waandamizi wa jeshi hilo baada ya ufunguzi wa jengo. PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA
SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Haya magorofa yatakua machafuuu, meusiii, fii kokodo kama yale ya mwenge pale dar es salaam kwa jinsi niwajuavyo askari wetu.
ReplyDeleteMtu anashindwa kupiga rangi hata balcon ambayo anaishi yeye mwenyewe kwa kusubiri jeshi au serikali ije ipige rangi.
Taabu kwelikweli.
Asante kwa kuwakumbuka askari hawa ambao nyumba zao nyingi ni mbaya kuliko gerezani. Zoezi hili liendelee mikoa yote. Bravo!!
ReplyDeleteUongozi wa Magereza hauna gender balance? I trust Bw Minja kwa uelewa wake baada ya UN ataliona hili na kulirekebisha.
ReplyDelete