Mwakilishi wa Mratibu wa Lishe katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sarah
Mshiu (kulia) akikabidhi unga wa lishe na maziwa kwa mkazi wa Lindi,
Zainabu Ali na mtoto wake Bright Abdallah, ambaye aliweza kueleza
vizuri masuala ya lishe, katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha
umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama
wajawazito na watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save the
Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika
Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. Katikati ni
Mkurugenzi wa Save the Childern Tanzania, Rachel Pounds.
Mwakilishi wa Mratibu wa Lishe katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sarah
Mshiu (kulia) akikabidhi zawadi ya simu ya mkononi kwa mkazi wa Lindi,
Asha Mkingamila, ambaye aliweza kueleza vizuri kuliko wengine nini
maana ya lishe bora , katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha
umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama
wajawazito na watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save the
Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika
Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni
Mkurugenzi wa Save the Childern Tanzania, Rachel Pounds.
Baadhi ya watoto wa Lindi wakitembea kwa maandamano katika
uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo
la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na
Shirika la Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la
Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni
mwa wiki.
Mkurugenzi wa Shirika la Watoto la Save the Children Tanzania,
Rachel Pounds, akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha
umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama
wajawazito na watoto ulioandaliwa na shirika hilo kwa kushirikiana na
Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi
mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mratibu wa Lishe
katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sarah Mshiu, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa
wa Lindi, Hamidi Nassoro, Mbunge wa Viti Maalumu, Lediana Mafuru
Mng’ong’o na Mbunge wa Serengeti, Dk Kwebe Stephen Kwebe.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Lediana Mafuru Mng’ong’o,
akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu
wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na
watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save the Children kwa
kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa
Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki.
Mwanamuziki mkongwe nchini, Kassim Mapili, akifanya vitu vyake
pamoja na wasanii wa Mjomba Band, katika hafla ya katikasherehe za
uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo
la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na
Shirika la Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la
Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni
mwa wiki.
Msanii wa Mashairi, Mrosho Mpoto, akikonga nyoyo za wakazi wa
Lindi waliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa kampeni ya
kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya
mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save
the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA)
katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki.
Hongera Save the Children pamoja na wananchi wa Mkoa wa Lindi.
ReplyDelete