Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kusini Magharibi, Dominican Mkama (wa pili kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa chakula, vinywaji na mavazi kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Bi. Wamoja Ayubu, kwa ajili ya Kituo cha Kulele Watoto Yatima cha Daily Bread Life Tanzania, kilichopo Mkimbizi, katika Manispaa ya Iringa. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Iringa, Bi. Theresia Mahongo.
Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kusini Magharibi, Dominican Mkama, akijibu maswali kutoka kwa waandishi waliohudhuria tukio hilo.
Watoto wa kituo cha Daily Bread Life Tanzania kilichopo Mkimbizi katika Manispaa ya Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Vodacom na Serikali ya Mkoa.
Baadhi ya watoto wa kituo cha Daily Bread Life.
Sehemu ya zawadi hizo.

Ni msaada kwa ajili ya kampeni yake ya 'Pamoja Daima na Vodacom msimu huu wa sikukuu Iringa , Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imeendelea kuwarudishia wananchi kile walichovuna baada ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Watoto Yatima cha Daily Bread Life Tanzania Children's Home kilichopo Mkimbizi katika Manispaa ya Iringa.

Msaada huo wenye thamani ya takriban Shs 3 milioni unahusisha vyakula na vinywaji mbalimbali pamoja na mbuzi ikiwa ni mchango wake kwa yatima hao katika maandalizi ya msimu huu wa sikukuu, ikiwa ni utekelezaji wa kampeni yake ya 'Pamoja na Vodacom'. Ambapo kwa mwezi huu Kampeni hiyo imetenga zaidi ya shilingi milioni 50 kwa lengo la kuwafikia watoto yatima nchi nzima.

Kampeni hiyo ya Pamoja na Vodacom inayoendeshwa na Mfuko wa kusaidia jamii"Vodacom Foundation," ambayo awali ilijulikana kama Care and Share.

Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kusini Magharibi, Dominician Mkama, akikabidhi zawadi hizo kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Bi. Wamoja Ayubu, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, alisema wanaona fahari kubwa kurejesha kwa wananchi sehemu ya kile ambacho walichangia, lakini kwa kuwakumbuka na kuwajali zaidi watoto yatima ambao wanahitaji faraja na upendo.

"Kila mwaka wakati kama huu wa sikukuu, Vodacom imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa jamii, wakiwemo watoto yatima, na tunafurahi kuona kwamba nao wanajisikia faraja pindi wanapoonyeshwa upendo," alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...