Mkuu
wa kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi
Marison Mwakyoma akiongea na madereva wa Boda Boda kwenye mkutano
uliofanyika katika uwanja wa wazi uliopo kata ya kimandolu jijini
Arusha.(Picha na Mahmoud Ahmad - Arusha)
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Mkuu
huyo wa Usalama barabarani amesema ameanzisha kampeni hiyo ili kila
mmoja apate mafunzo yake kupitia chuo hali ambayo itasaidia kupunguza
ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa.
Mkutano
huo uliohudhuriwa na Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi
Gilles Muroto, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi toka Dawati la Jinsia na
Watoto, Maria Maswa, Polisi tarafa, viongozi wa tarafa ya Suye, kata,
mitaa na madereva wapatao 100 ulitawaliwa na makofi ya pongezi pamoja na
vifijo kutoka kwa madeva hao baada ya Mkuu huyo wa Usalama Barabarani
kuwaahidi kuwa kama wangekuwa tayari hata siku ya pili yake (jana)
wangeweza kuanza darasa.
Alimalizia
kwa kuwaasa madereva hao kutojichukulia sheria mkononi pindi mwenzao
anapogongwa na gari kwani vitendo hivyo vinaweza kuwagharimu badala yake
aliwataka wafanye mambo manne muhimu; kwanza kuandika namba ya gari
iliyosababisha ajali, kuielewa mahali ajali ilipotokea, kutoa taarifa
polisi na mwisho kumwahisha mwenzao hospitali.
Programu
ya mafunzo kwa waendesha pikipiki mkoani hapa ilianza rasmi mwezi
Agosti mwaka huu baada ya kufunguliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas kutokana na kuwepo
kwa ongezeko kubwa la ajali.
Hadi
sasa waendesha boda boda wapatao 900 kutoka wilaya za Arusha mjini,
Arumeru na Monduli wamekwisha pata mafunzo ya udereva toka vyuo
mbalimbali vilivyopo mkoani hapa.
MAFUNZO YA UDEREVA BODA BODA!
ReplyDeleteInachekesha lakini ni mpango mzuri sana kufuatia wimbi la ajali za aina hii ya usafiri.
Pamoja na kufundishwa taratibu za uendeshaji wa bodaboda,waendeshaji hawazingatii kabisa mafundisho,hizo pikipiki zenyewe zintobolewa exhaust na zinapiga kelele sana zinasumbua jamii,lakini polisi mnaangalia tu,naomba polisis yenyewe iende kenya waone jinsi gani wavunjaji sheria wanavyothibitiwa,mjini hakuna pikipiki kabisa,sababu ni hivi mjini kuna usafiri wa kutosha wa daladala na taxi,pikipiki ni za kupita njia nyembamba sio kusongamana na magari.Nendeni nchi za nnje mkajifunze kwanza namna sheria inafanya kazi,kwani hao jamaa ni wavunja sheria, sio kwamba wao ni watoa huduma.
ReplyDeleteVigezo vya Madereva wa Bodaboda,
ReplyDeleteNi muhimu vipimo vya afya ya akili vikazingatiwa!
Maana hawa waendesha Bodaboda wamekuwa kama akili zao sio nzuri kabisa.
Siku moja tulishuhudia tukiwa ndani ya gari palikuwa na foleni, palikuwa na gari moja lenye matairi makubwa sana kiasi kwamba uvunguzi mwake panapitika!,,,tulishuhudia Dereva wa Bodaboda akichungulia chini akiangalia uwezekano wa kupitisha pikipiki uvunguni mwa lile Lori!.
Abiria nyuma ya kiti cha pikipiki alipoona Dereva wake yuko vile alipiga kelele na ndio jamaa Bodaboda alipositisha jaribio lake la kupita uvunguni mwa Lori!!!