Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi Marison Mwakyoma akiongea na madereva wa Boda Boda kwenye mkutano uliofanyika katika uwanja wa wazi uliopo kata ya kimandolu jijini Arusha.(Picha na Mahmoud Ahmad - Arusha)

Na Mahmoud Ahmad,Arusha

Mkuu huyo wa Usalama barabarani amesema ameanzisha kampeni hiyo ili kila mmoja apate mafunzo yake kupitia chuo hali ambayo itasaidia kupunguza ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa.

Mkutano huo uliohudhuriwa na Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi Gilles Muroto, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi toka Dawati la Jinsia na Watoto, Maria Maswa, Polisi tarafa, viongozi wa tarafa ya Suye, kata, mitaa na madereva wapatao 100 ulitawaliwa na makofi ya pongezi pamoja na vifijo kutoka kwa madeva hao baada ya Mkuu huyo wa Usalama Barabarani kuwaahidi kuwa kama wangekuwa tayari hata siku ya pili yake (jana) wangeweza kuanza darasa.

Alimalizia kwa kuwaasa madereva hao kutojichukulia sheria mkononi pindi mwenzao anapogongwa na gari kwani vitendo hivyo vinaweza kuwagharimu badala yake aliwataka wafanye mambo manne muhimu; kwanza kuandika namba ya gari iliyosababisha ajali, kuielewa mahali ajali ilipotokea, kutoa taarifa polisi na mwisho kumwahisha mwenzao hospitali.

Programu ya mafunzo kwa waendesha pikipiki mkoani hapa ilianza rasmi mwezi Agosti mwaka huu baada ya kufunguliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas kutokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la ajali.

Hadi sasa waendesha boda boda wapatao 900 kutoka wilaya za Arusha mjini, Arumeru na Monduli wamekwisha pata mafunzo ya udereva toka vyuo mbalimbali vilivyopo mkoani hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. MAFUNZO YA UDEREVA BODA BODA!

    Inachekesha lakini ni mpango mzuri sana kufuatia wimbi la ajali za aina hii ya usafiri.

    ReplyDelete
  2. Pamoja na kufundishwa taratibu za uendeshaji wa bodaboda,waendeshaji hawazingatii kabisa mafundisho,hizo pikipiki zenyewe zintobolewa exhaust na zinapiga kelele sana zinasumbua jamii,lakini polisi mnaangalia tu,naomba polisis yenyewe iende kenya waone jinsi gani wavunjaji sheria wanavyothibitiwa,mjini hakuna pikipiki kabisa,sababu ni hivi mjini kuna usafiri wa kutosha wa daladala na taxi,pikipiki ni za kupita njia nyembamba sio kusongamana na magari.Nendeni nchi za nnje mkajifunze kwanza namna sheria inafanya kazi,kwani hao jamaa ni wavunja sheria, sio kwamba wao ni watoa huduma.

    ReplyDelete
  3. Vigezo vya Madereva wa Bodaboda,

    Ni muhimu vipimo vya afya ya akili vikazingatiwa!

    Maana hawa waendesha Bodaboda wamekuwa kama akili zao sio nzuri kabisa.

    Siku moja tulishuhudia tukiwa ndani ya gari palikuwa na foleni, palikuwa na gari moja lenye matairi makubwa sana kiasi kwamba uvunguzi mwake panapitika!,,,tulishuhudia Dereva wa Bodaboda akichungulia chini akiangalia uwezekano wa kupitisha pikipiki uvunguni mwa lile Lori!.

    Abiria nyuma ya kiti cha pikipiki alipoona Dereva wake yuko vile alipiga kelele na ndio jamaa Bodaboda alipositisha jaribio lake la kupita uvunguni mwa Lori!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...