Waziri wa Fedha Dkt . William Mgimwa (katikati) akiwapongeza wafanyakazi wa Wizara ya Fedha walichaguliwa mwezi Mei mwaka huu kuwa wafanyakazi bora kwa mwaka 2012. Tafrija fupi ya kuwazawadia wafanyakazi bora ilifanyika leo mjini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wafanyazi mbalimbali.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma(kushoto) akipokea tuzo ya ufanyakazi bora wa kitengo kutoka kwa Waziri wa Fedha Dkt . William Mgimwa(kulia) . Tafrija fupi ilifanyika leo mjini Dar es salaam kufuatia kuchaguliwa kwake mwezi Mei mwaka huu kuwa mfanyakazi bora wa mwaka 2012.
Mkuu wa Mfuko wa Mikopo wa Hazina kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali , Wizara ya Fedha Christina Ngonyani (kushoto) akipokea tuzo ya ufanyakazi bora wa kitengo kutoka kwa Waziri wa Fedha Dkt . William Mgimwa(kulia) . Tafrija fupi ilifanyika leo mjini Dar es salaam kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa mfanyakazi bora wa mwaka 2012.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) akipokea tuzo ya ufanyakazi bora wa Wizara hiyo kutoka kwa Waziri wa Fedha Dkt . William Mgimwa(kulia) . Tafrija fupi ya kuwazawadia wafanyakazi bora ilifanyika leo mjini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wafanyazi mbalimbali.
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa , Katibu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah wakishirikiana na viongozi wa TUGHE na wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar es salaam kuimba wimbo wa mshikamano wakati wa tafrija fupi leo ya kuwapongeza wafanyakazi bora wa mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kweli aliyenacho ataendelea kupewa inamaana wafanyakazi walio chini yao wamekosekana kuwa wafanyakazi bora?wanawavunja moyo walio chini yao kwakawaida watendaji wanawajibika kuliko wakuu hapo nawaona mabosi tu wanapokea zawadi je walio chini si bora?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...