Ikiwa ni siku chache zimepita tangu mtandao wa kijamii na kiuchumi nchini (socio-economic Network) Mambopoint kuwekwa hewani , maelf ya watumiaji wanaoendelea kujiunga ili kuona kazi zinazotangazwa, kubadilishana habari kwa njia ya picha, maandiko pamoja na kupiga soga (chating) wanaweza kuwaalika rafiki zao waliopo katika mitandao mingine kama facebook.

Raymond Mtani ni meneja mahusiano wa kampuni ya Maarifa Informatics LTD wabunifu na wasimamizi wa mtandao huo alisema mambopoint.com Inatoa huduma hiyo ili kuwarahisishia watumiaji wa mambopoint kupata marafiki wengi ambao watashiriki kupiga soga katika mtandao huo.

Aliongeza kuwa ili mtumiaji wa mambopoint amwalike rafiki kutoka facebook, anapaswa kujisajili katika anuani ya www.mambopoint.com, kama amejisajili aingie katika ukurasa wake wa (home page) hapo ataangalia alama na maandishi ya upande wa kushoto ambako atakuta kitufe cha (find friends) akibofya hapo atakutana na orodha ya marafiki walio mambopoint tayari lakini pia ataona linki ya kualika rafiki kutoka faceboook.

“ kwanza tunawashukuru wanamtandao kwa kuchagua mambopoint, ni katika kuzingatia hilo tumeamua kuwarahisishia watumiaji wa mtandao wetu namna ya kutafuta marafiki ili waweze kuhabarishana, kuburudishana kwa picha utani na kadhalika, na njia rahis ya kufanikisha hilo ni kuwapa uwezo wa kualika marafiki kutoka mitandao mingie ya kijamii. Kwa sasa tumeanzan na facebook baadae tutaenda twitter, google + BBM na mingine mingi.” Alisema.

Aidha, watumiaji wa mtandao wa mambopoint wanaombwa kutoa maoni yao kupitia linki ya “please write to us” ili mambopoint indelee kuboresha huduma zake, wakati huo huo chat line inaendelea kufanya kazi kama kawaida mtumiaji aangalie kulia katiaka home page yake ataona kitufe cheusi chenye neno (Friend) akibofya ataona marafiki walioko hewani.

Wakati dunia ikikimbia kwa kasi katika technolojia ya mawasiliano na science kwa ujumla mambopoint.com yaweza kuwa ni miongoni mwa harakati za watanzania kukimbizana na kufuata kasi hiyo na kuiweka nchi yetu katika ramani tofauti duniani ya kitechnolojia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...