Meneja Mkuu wa Kampuni ya Zuku Tanzania,Fadhili Mwasyeba (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kuungana na Kampuni ya MaxMalipo kwenye Malipo ya huduma za kulipia huduma ya Zuku,iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo,Ahmed Lussasi akielezea kufurahishwa kwake kwa makubaliano na Zuku na kutakuwa rahisi kwa wateja wa zuku kulipa ada.

Kampuni ya Zuku Pay TV imetia saini makubaliano ya ushirikiano na Maxcom Africa Ltd ambayo itawezesha wateja wa Zuku kulipia ada zao wakitumia wakala wa MaxMalipo au mashine za kulipia za Maxcom. Uzinduzi huu ulifanyika katika mkutano na waandishi hapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Fadhili Mwasyeba Meneja Mkuu wa Wananchi Satellite Tanzania, wamiliki wa vingamuzi ya Zuku Pay TV, alisema "Wateja wetu sasa wanaweza kulipia ada za Zuku Pay TV wakitumia technoljia mpya ya MaxMalipo .


Zaidi ya hapo wanaweza kupata huduma kutoka mawakala wote wa MaxMalipo kote nchini. Lengo letu kuu ni kutumikia wateja wetu na kuboresha huduma zetu. Makubaliano yetu na MaxMalipo ni ushahidi wa dhamira yetu kuwatumikia wateja wetu.”

Ahmed Lussasi Meneja Biashara wa Maxcom Afrika Limited alisema "Tunafurahia kuingia makubaliano na kampuni ya Wananchi Sattellite, inayotoa huduma za Zuku Pay TV na kuhudumia wateja wao wote kote nchini.

Kampuni yetu inayo wakala zaidi ya 3500 nchini na huduma yetu mpya ya malipo kwa kutumia mashie maalumu za Maxmalipo inatuwezesha tuwafikie hata wateja katika pembe mbalimbali za nchi. Lengo letu kuu ni kuleta malipo ya elecktroniki karibu na Watanzania. "

Sasa kulipia huduma imerahishwa kwa wateja. Wateja wanatakiwa kuwa na Zuku Subscription ID, kuchagua kati ya huduma ya Zuku Classic, Zuku Premium, Asia Classic au Asia Premium na huduma ya Zuku inawezeshwa papo hapo.

Zaidi ya hapo, Zuku Pay TV sasa wana promosheni ya "Zuku Tunakuthamini - Pata TV Bure". Programu hii ya inayowazawadia wateja, itahitaji wateja wa Zuku kuungananisha wateja kumi (10) wapya au kuunganisha wateja watano (5) wateja wapyana unashinda televisheni ya inchi 42 na inchi 22. Programu hii hiana draw na ushindi ni wa uhakika.

Televisheni ya Zuku inatoa uchaguzi mpana wa stesheni za burudani ikiwa ni pamoja na Habari, Michezo na Sinema, majarida na muziki. Zaidi ya hapo, wanajumuisha chaneli za nje kama vile BBC, MTV Base, Sentanta Sports, MGM movies na zinginezo nyingi.

Pia Msambazaji hutoa ofa kabambe za stesheni kama vile Zuku Afrika ambayo huonesha bara la Afrika, Zuku Maishaambayo huonesha makala mbalimbali, Zuku Michezo pamoja na chaneli lukuki za sinema. Huduma hii ya Zuku hupatikana kupitia satelaiti Tanzania nzima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...