Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi akiwaangalia watoto waliolazwa katika wodi ya watu wa ajali kwenye hospitali ya Mnazi Mmoja,Zanzibar kabla ya kukabidhi msaada kwa ajili ya wodi hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi akizungumza wakati akimkabidhi Muuguzi Mkunga wa Wodi ya Watoto waliopata ajali Bibi Leluu Omar Said msaada wa vitanda 14, magodoro na mashuka yake kwa ajili ya wodi hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif akifuatana na Waziri wa Afya wa Zanzibar,Mh. Juma Duni Haji, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dr. Saleh Mohd Jidawi na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi na Ushirika,Mh. Haroun Ali Suleiman wakiangalia msaada wa vitanda, magodoro na mashuka yaliyotolewa na msamaria mwema katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na mmoja wa wagonjwa wa wodi ya Mifupa aliyelazwa kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vilivyotolewa na wasamaria wema,Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi Muuguzi dhama wa wodi ya Mifupa Bibi Afsa Abdulla msaada wa vitanda 24, magodoro na mashuka yake kwa ajili ya wodi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ni vizuri lakini hayo magodoro kwa hospital sio mazuri yalitakiwa yawe na plastics protection ili kuepusha maambkizo hospital. na mgonjwa akiondoka t kwenye kitanda inakuwa ni easy kuwaip na madawa yanayotakiwa, kwa vile ni yavitamba juu sirahisi kusafishika na ni easy kuleta maambukizi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...