
Head of Primary Medical Centre Bwa. Siwawi Konteh (wa pili kulia) ambaye pia ni mratibu wa mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja ili kuokoa Afya ya Mama na Mtoto akizungumzia Malengo Makuu ya mradi huo kuwa ni kuongeza kiwango na matumizi ya Huduma ya Afya ya Mama Mjamzito na Watoto na kushirikiana na kujifunza kuhusu Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto. Kutoka kushoto ni Acting Medical Director wa Aga Khan Hospital Dr. Ambrose Chanji, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib, Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Dr. Sebastian Ndege na Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu cha Hospitali hiyo Bw. Anis Nazrani.
Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi magari ya kubeba wagonjwa kwa hospitali ya Aga Khan ambapo amesema vifo kadhaa vinavyotokea katika hospitali nyingi kwa sasa vinawahusisha akinamama na watoto wasio na hatia ambao hukosa huduma za awali za haraka zikiwemo usafiri na hivyo katika kujali hilo wametoa magari hayo.
Aidha amesema Ndege Medics inashukuru kuwa sehemu ya mradi endelevu wa kujaribu kuokoa maisha ya akina mama na watoto ambao lengo lake ni kuchangia katika kuboresha afya ya uzazi wa mama na watoto wachanga katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Mwanza, Mbeya na Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari ya kubeba wagonjwa kwa Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni katika mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania
Wakipongezana baada ya makabidhiano hayo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Ndege Medics akionyesha baadhi ya vifaa vilivyomo ndani ya magari hayo ya kisasa.
Pichani Juu na Chini ni muonekano wa magari hayo ya kubebea wagonjwa kwa ndani yaliyotelwa kwa hospitali ya Aga Khan na NDEGE Medics kwa ajili ya mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania.
Pichani Juu na chini ni baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege Medics, Hospitali ya Aga Khan na waandishi wa habari walioshuhudia tukio la makabidhiano hayo.


Baadhi ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyokabidhiwa rasmi leo kwa Hospitali ya Aga Khan jijini Dar ikiwa ni sehemu ya mradi Endelevu utakaohusisha Mikoa ya Mwanza, Dodoma, Iringa, Mbeya na Morogoro kwa ajili ya kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto.
Ni msaada mzuri huu lakini tatizo litakuwa kupata spare za hayo magari. Itakuwa ni usumbufu kupata spare za Renault. Walikuwa walete magari ya Toyota ambayo kila sehemu spare zimejaa Tanzania.
ReplyDeleteMichuzi mi napongeza kwa huo msaada lkn pia nasikitika kukwambia hiyo hospya Aghakan ingejaribu pia kufikiria kuhusu kupunguza gharama za matibabu kwa watanzania walio wengi ambao ni walala hoi maana gharama zao ni kama hosp ya aghahakan kama ni kwaa ajili ya watu wenye uwezo tu, wakati huduma ya afya ni ya msingi kwa kila raia bila ya kupata ukiritimba wa gharama na mengineyo, naomba pia usiibanie hii na wadau wenginepia wachangie
ReplyDeleteWell done dr sebastian ndege.......kawa wanavyosema TWAWEZA...change ni sisi......kuna vitu vingine sisi watanzania tunaweza kufanya wenyewe....sio kulia lia tu kila siku....serikali...serikali.....
ReplyDeleteBure Aghali, na waingereza walisema "there nothing like a free lunch", kama msaada si angewapa Hospitali za serikali especially za wilaya, kwani Agakhan si Hospitali ya walala hoi, wanasaidiana wenyewe kwa wenyewe, anyway mtu akitoa msaada ni juu yake aupeleke wapi. Nilikuwa nafikiria kwa SAUTI.
ReplyDelete
ReplyDeleteHuyo anesema kwamba wapunguze garama namuonea huruma sana hajui anacho kisema yaani kama unataka cheap nenda muhimbili ndugu yangu,,,,,there is no chepa medical service in this world its only availabla in Tanzania na ndo maana kila siku tuanlia afya mbaya
tena naona siku hizi hii hospital ishakua ya wengi sana ukienda foleni kubwa na woote wanataka express service ni wakati wa kupandisha bei zaid sasaa ili paendelee kua pa wachache na waweke good doctors sio muhimbili graduates ambao hata mama akipata miscarriage they dont care
ReplyDeleteMSAADA HUU WANGEPEWA HOSPITALI ZA MASIKINI VIJIJINI INGELETA HAMASA ZAIDI..
Jamaani unatakakusema leo nikipiga agakhan napata huduma ya usafiri bure kwenda hapa agakhan? Naomba ufafanuzi
ReplyDeleteVery good gesture and hongera sana Dr. Ndege ila itasaidia misaada kama hii ikipelekwa hospital za serikali kuwasaidia walala hoi. God bless you.
ReplyDelete