BAADHI YA WAKAZI WA IMEZU WAMESEMA AJALI HIYO IMESABABISHWA NA MWENDO KASI WA DEREVA WA BASI HILO. |
HAPA WANAUSALAMA WAKIHESABU PESA WALIZOZIKUTA KWENYE MWILI WA MAREHEMU ENOCK HUKU WANANCHI WAKISIMAMIA KWA MAKINI ZOEZI HILO LA KUHESABU HIZO PESA ZAIDI YA SHILINGI MILION 15 ALIZOKUWANAZO MAREHEMU |
PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG. |
Kwanza nitoe pole kwa watu wote wa mbeya, wanafamilia na walikuwamo ktk ajari hii.Nimefarijika kwa kusoma hizi taarifa za fedha alizokutwa nazo marehemu na usimamizi wa haki yake marehemu huyo.Hongereni sana wakazi wa eneo husika la ajari kwa kutokukubari ile sifa mbaya iliyopata kusambaa ya wakazi wa mbeya hasa wa eneo linapotokea ajari kudiriki kufanya kinyume na uungwana,Nyinyi wakazi wa eneo hili mlisimama kidete na kuweka uungwana mbele.Hongereni sana na nawaomba watanzania wote waige mfano huu wa watu wa mbeya.
ReplyDeletePoleni sana Abiria na wote mliopoteza ndugu zenu.
ReplyDeletePolisi chondechonde hizo fedha zifike kwa wahusika jamani!
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi lakini pia kifo chake ni fundisho kwa watu wote kuwa siku hizi kuna huduma nyingi sana za kuhifadhi kiasi kikubwa cha hela na pia kufanya malipo kwa watoa huduma wengine, M-pesa, Tigo pesa, Bank na kadhalika, yatupasa tuzitumie kwa usalama wa mali zetu na usalama wa watu wengine pia maana watu waweza kuishiwa imani na kuanza kupigana kwa ajili ya fedha hizo.Honereni raia wema wa eneo hilo kwa kusimamia haki.Mwenyezi Mungu awabariki sana.
ReplyDeletejamani pole sana kwa abiria wote na sana sana pole sana kwa wafiwa.
ReplyDeleteIla jamani inabidi tuangalie sana kuhusu haya magari yanayokwenda mikoani. Ukiangalia gari hili linaonekana limechoka sana tena sana.
Serikali inabidi iingilie kati ili kukagua mabasi yote yaendayo mikoani. Na vile vile madereva nao inabidi wapikwe vizuri katika kazi zao. Sielewi ajali ilitokeaje lakini mara nyingi inasababishwa na dereva au gari bovu.
ni hayo tu na asanteni
Mdau UK
Poleni sana.
ReplyDeleteEti "More Fire" kweli more fire inavyoonekana dereva alishapata moto!
ReplyDeletePoleni sana wahanga