BASI LA KAMPUNI YA NGANGA LILILOKUWA LINATOKEA MBEYA KWENDA DAR ES SALAAM LIMEPINDUKA LEO KATIKA ENEO LA IMEZU NJE KIDOGO YA MJI WA MBEYA. AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA MBILI ASUBUHI NA ABIRIA MMOJA  ALIFARIKI PAPO HAPO NA WENGINE ZAIDI YA 40 WAMEJERUHIWA VIBAYA NA KUPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MJINI MBEYA. ABIRIA ALIYEFARIKI AMETAMBUWA KWA JINA LA ENOCK LWILA MKAZI WA ENEO LA MAMA JOHN MJINI MBEYA NA NIMFANYABIASHARA KWENYE SOKO LA MWANJELWA
BAADHI YA WAKAZI WA IMEZU WAMESEMA AJALI HIYO IMESABABISHWA NA MWENDO KASI WA DEREVA WA BASI HILO.

MWILI WA MAREHEMU ENOCK LWILA  UKIWA UMELAZWA CHINI KUSUBIRI WANA USALAMA KUJA KUUCHUKUA.MAREHEMU ENOCK LWILA AMEKUTWA NA ZAIDI YA SHILINGI MILION 15 KATIKA SOKSI NA KWENYE MIFUKO YAKE YA SURUALI INASEMEKEANA ALIKUWA ANAENDA DAR ES SALAAM KUNUNUA BIDHAA MBALIMBALI ZA DUKANI KWAKE.

HAPA WANAUSALAMA WAKIHESABU PESA WALIZOZIKUTA KWENYE MWILI WA MAREHEMU ENOCK HUKU WANANCHI WAKISIMAMIA KWA MAKINI ZOEZI HILO LA KUHESABU HIZO PESA ZAIDI YA SHILINGI MILION 15  ALIZOKUWANAZO MAREHEMU 

PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kwanza nitoe pole kwa watu wote wa mbeya, wanafamilia na walikuwamo ktk ajari hii.Nimefarijika kwa kusoma hizi taarifa za fedha alizokutwa nazo marehemu na usimamizi wa haki yake marehemu huyo.Hongereni sana wakazi wa eneo husika la ajari kwa kutokukubari ile sifa mbaya iliyopata kusambaa ya wakazi wa mbeya hasa wa eneo linapotokea ajari kudiriki kufanya kinyume na uungwana,Nyinyi wakazi wa eneo hili mlisimama kidete na kuweka uungwana mbele.Hongereni sana na nawaomba watanzania wote waige mfano huu wa watu wa mbeya.

    ReplyDelete
  2. Poleni sana Abiria na wote mliopoteza ndugu zenu.
    Polisi chondechonde hizo fedha zifike kwa wahusika jamani!

    ReplyDelete
  3. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi lakini pia kifo chake ni fundisho kwa watu wote kuwa siku hizi kuna huduma nyingi sana za kuhifadhi kiasi kikubwa cha hela na pia kufanya malipo kwa watoa huduma wengine, M-pesa, Tigo pesa, Bank na kadhalika, yatupasa tuzitumie kwa usalama wa mali zetu na usalama wa watu wengine pia maana watu waweza kuishiwa imani na kuanza kupigana kwa ajili ya fedha hizo.Honereni raia wema wa eneo hilo kwa kusimamia haki.Mwenyezi Mungu awabariki sana.

    ReplyDelete
  4. jamani pole sana kwa abiria wote na sana sana pole sana kwa wafiwa.

    Ila jamani inabidi tuangalie sana kuhusu haya magari yanayokwenda mikoani. Ukiangalia gari hili linaonekana limechoka sana tena sana.

    Serikali inabidi iingilie kati ili kukagua mabasi yote yaendayo mikoani. Na vile vile madereva nao inabidi wapikwe vizuri katika kazi zao. Sielewi ajali ilitokeaje lakini mara nyingi inasababishwa na dereva au gari bovu.

    ni hayo tu na asanteni

    Mdau UK

    ReplyDelete
  5. Poleni sana.

    ReplyDelete
  6. Eti "More Fire" kweli more fire inavyoonekana dereva alishapata moto!
    Poleni sana wahanga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...