Wakazi wengi wa Visiwani Zanzibar wanapenda sana kutumia mikate ya Boflo kama ni chakula cha asubuhi,kutokana na kupanda bei kwa mikate hiyo hivi sasa hulundikana kwa wingi katika matenga kadhaa,pichani ni matenga ya mikate ikiwa imekaa wazi bila ya kufunika ukizingatia kipindi hiki cha upepo na mvua zinazonyesha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

 1. Kaka Michuzi nafikiri kwa hivi sasa wananchi ni waelewa na hali halisi ya upatikanaji fedha huku ni tofauti na huko Bara. Sasa itabidi watengenezaji mikate wapange bei nzuri ambayo tutaihimili tofauti na sasa

  ReplyDelete
 2. Hayo ndio mnayojuwa tuu kutuzalilisha WAZANZIBARI halafu mnakaa pembeni mnacheka yana mwisho hayo naninawakumbusha pia wahafidhina hizi pia ndio faida ya Muungano na bado zitapanda sana tuu boflo. GOD BLESS ZANZIBAR.

  ReplyDelete
 3. mbona nimenunua usiku huu kwa bei ya kawaida?imepanda lini?na kiasi gani?huko maeneo ya mjini mnapenda kuongeza bei,ukianzia kwerekwe kwenda juu bei ya kawaida tu

  ReplyDelete
 4. sinunui hata sikumoja mkate ukowaziwazi hivyo.wiki nzima unapitishwa kwenye tenga .

  ReplyDelete
 5. Jamani ndugu zangu, hivi haiwezekani kabisa mikate hii ikawekwa kwenye mifuko ya plastiki au walau ndani ya kabati lenye kioo. Nina wasiwasi na watumiaji kuugua matumbo kutokana na vumbi na nzi. Sina maana ya kudhalilisha hapa bali inawezekana magonjwa mengine tukaweza kuyaepuka.

  ReplyDelete
 6. Tutajieni hiyo bei mpya ya boflo moja hivi sasa ni shilingi ngapi,na ile bei ya awali ilikuwa shilingi ngapi,ili sisi wakandarasi wa kalamu tuanze kutembeza "nyundo zetu"!lakini,mkiacha habari hivi hivi bila takwimu,hakieleweki kitu.Huku Bara,kwamfano,Mwanza mjini,bei ya boflo moja ni kati ya shs.1,000/= hadi shs.1,400/=,inategemea umenunulia wapi,lakini,wengi bei ya shs.1.200/=watakususia mikate yako dukani!Sasa tuelezeni wenzetu huko Zanzibar,boflo moja lauzwa kwa shilingi ngapi?maana hatuwezi kukaa kimya kama wenzetu huko mnaumizwa na walanguzi!na serikali imekaa kimya kama imelewa kahawa vile!

  ReplyDelete
  Replies
  1. 2500 ndogo kubwa 500

   Delete
 7. MTU NI AFYA JAMANI!!!

  ReplyDelete
 8. wajani hivi kwa nini, sisi watu wenye asili ya bara hili hatupendi hygine,

  ReplyDelete
 9. 2500 ndogo kubwa 500

  ReplyDelete
 10. 250 ndogo 500 kubwa

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...