Treni ikiwa tayari kuondoka Stesheni ya dar kwenda Ubungo Maziwa

Hatimaye Kampuni ya Reli Tanzania -TRL umetangaza kurejesha tena huduma ya treni ya jiji ambayo iliisitisha kwa muda kutoa huduma wakati asubuhi leo Alhamis Januari 03, 2013.

Treni ya kwanza iliondoka Stesheni ya Dar es Salaam saa 10 jioni ikishuhudiwa na Katibu M kuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar Chambo akifuatana na viongozi waandamizi wa Wizara hiyo na pia wale wa TRL wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu.

Taarifa ya awali ilifafanua kuwa safari za asubuhi zilisitishwa baada ya kichwa kimojawapo kati ya viwili vinavyotoa a huduma hiyo tokea Oktoba 29 mwaka jana kuacha njia katika maeneo ya Keko jana saa 5 usiku wakati vikielekea katika Karakana ndogo ya Malindi kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi na kujazwa mafuta tayari kwa ajili ya kuanza kutoa huduma asubuhi ya leo.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa eneo palipotokea ajali lilijaa mchanga uliosababishwa na maji ya mvua iliyonyesha kuanzia jioni hadi usiku wa jana. Mara baada ya ajali hiyo Mafundi wa TRL walianza kazi ya ukarabati kwa kuondoa mchanga na pia kukirejesha kichwa cha treni katika reli zoezi lililokamilika saa 2:30 asubuhi ya leo Januari 03, 2013 na njia kufunguliwa tena kwa matumizi ya treni..

Uongozi unasikitika kwa usumbufu walioupata wateja wake hususan Wakazi wa jiji ambao wameshazoeya huduma hii kwa takriban miezi miwili sasa. Aidha TRL inatoa wito kwa Wakazi jiji wanaoishi kandokando mwa reli wajiepushe na vitendo vyovyote vitakavyoathiri miundombinu ya reli naikiwemo wizi wa kokoto katika matuta ya reli.

Uongozi unatoa rai kwa raia wema na wanaoipenda huduma za TRL kutosita mara moja kutoa taarifa dhidi ya vitendo vyovyote vinavyofanywa vya kuhujumu njia ya reli na vitendea kazi vyake.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkururgenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu.

TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Januari 03, 2013.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kila mkazi wa Dar es salaam awe Komandoo katika kuilinda miundombinu ya Reli ya Dar,ni mali yenu wananchi kwa faida yenu.Msikubali waroho wachache waihujumu reli hiyo,na kuwasababishia adha kubwa ya usafiri iliyowakabili kwa kipindi kirefu!Kila mmoja amchunge mwenzake pindi atakapo jaribu kuhujumu miundombinu ya reli!Ni uzalendo tu unaohitajika hapa.Nimpongeze kwa sana Mh.Dr.Mwakyembe kwa kuirudisha Reli tena katika heshima yake ya zamani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...