TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII TOKA MKOANI SHINYANGA HIVI SASA,INAELEZA KUWA MOTO UMETOKEA KATIKA HOSPITALI KUU YA MKOA WA SHINYANGA BAADA YA KUTOKEA HITILAFU YA UMEME KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI NDANI YA HOSPITALI HIYO NA KUPELEKEA KUTOKEA KWA MADHARA NDANI YA CHUMBA HICHO.
JUHUDI ZA HARAKA ZILIWEZA CHUKULIWA NA KUWASILIANA NA WATU WA FAYA NA BAADA YA MUDA MFUPI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUUZIMA MOTO HUO.
HAKUNA MTU YEYOTE ALIEDHULIKA NA MOTO HUO NA INASEMEKANA NDANI YA CHUMBA HICHO KULIKUWA NA MAITI MOJA TU YA MTOTO MDOGO AMBAYO ILIOKOLEWA PIA.
INAELEZWA KUWA TUKIO LA NAMNA HIYO SIO LA KWANZA KUTOKEA KATIKA CHUMBA HICHO CHA KUHIFADHIA MAITI NDANI YA HOSPITALI HIYO,HIVYO JUHUDI ZA HARAKA ZINAFANYWA KUWASILIANA NA TANESCO ILI KUWEZA KUTATUA KABISA TATIZO HILO.
TUTAENDELEA KUJULISHANA KADRI TAARIFA ITAKAVYOKUWA IKITUFIKIA.
Ahhh, hii sio bure pana kitu hapa!
ReplyDeleteInawezekan wamechoma ili kupindisha ushahidi wa maovu!
Shinyanga inavuma sana kwa kuendekeza Imani za jadi, inawezekana wamechoma wakisaka Maiti za Vikongwe waliowauwa wao wenyewe kwa tuhuma za Uchawi ama ma ALBINO !!!