Habari iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa kundi kubwa la wananchi waliojawa na ghazabu Wilayani Rufiji leo wamevamia kituo cha Polisi Kibiti Wilayani humo na kuanzisha vurugu kubwa kufuatia raia mmoja mkazi wa kijiji hicho kudaiwa kufa kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na kipigo cha Polisi.

Chanzo chetu cha Habari kutoka Kibiti kinatupasha kuwa,kijana huyo aliyefariki kutokana na kipigo hicho afahamikae kwa jina la Hamis Mpondi ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,jijini Dar es Salaam na taarifa hiyo ilipowafikia wananchi hao ndipo wakachukua uamuzi wa kwenda kituoni hapo na kuanzisha vurugu hizo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa,hivi sasa wananchi hao wanateketeza nyumba za Askari Polisi hao zilizopo jirani kabisa na kituo hicho, licha ya juhudi za Polisi kuwatawanya kwa mabomu kuendelea kufanyika.

Aidha wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe, magogo na kuchoma matairi ikiwa ni umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti.

Inaelezwa kuwa hali imezidi kuwa tete katika eneo hilo huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu ya machozi hewani kujaribu kutawanya umati huo wa watu.

tutaendelea kupeana taarifa zaidi kadri zitakavyokuwa zikitufikia. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Polisi wetu hawajui wajibu wao.

    Imefika wakati warudishwe shule ili angalao waelimike.

    Yaani hawajui wanadfanya nini.a

    ReplyDelete
  2. Jamani askari chonde chonde musionee raia sasa watu wamejawa na hasira na matokeo yake itakuwa ni hasara.

    Jeshi la polisi tunawaomba mufikirie hao munaowaajiri siyo wakipewa silaha ndiyo waone wanaweza kuzifyatua tu au kupiga watu mpaka kufa.

    Wananchi wamechoka na uonevu wa askari sasa.

    ReplyDelete
  3. haiingii akilini mtuhumiwa anapelekwa polisi akiwa mzima halafu mauti inamkuta akiwa kituoni kwa ku[igwa na maafande, huku wananchi tunaambiwa tusichukue sheria mkononi kuuwa vibaka huko polisi nako wanachukua sheria mkononi na kuuwa, nini maana ya mahakama? ikiwa jeshi la polisi linaua mtuhumiwa naona hakuna haja ya mahakama. ninawaunga mkono, miguu na kichwa wananchi walioteketeza nyumba zenu, yani nyinyi polisi wa bongo inabidi wote muende israel mkajifunze upolisi. zaidi mnachojua ni rushwa na mabavu, kuua raia kwa makusudi, ubabe mwingiiii kichwani 0, mkishavaa hayo magwanda yenu mnajiona miungu watu. na sio rufiji tuu hii tabia ya kuua raia vituoni ipo tanzania nzima, hii kitu lazima iingizwe kwenye katiba mpya, kuwa polisi akiuwa raia kwa kipigo adhabu yake ni KUNYONGWA!!!

    ReplyDelete
  4. Hii nimeipenda saaana na ndio inavyotakiwa hasa ili jeshi na polisi wa tanzania wapate funzo sio kuonea watu kila siku kwa kutumia nguo zao

    ati askari ila kama tukiendelea kupeana kipigo na tukakirudisha kwao kisawa sawa hasa basi lazima heshima itakuwepo na hapa kimaoni yangu haina haja ya kuharibu jengo wameuwa mtu mmoja na sisi tuuwe askari mmoja tu

    sio zaidi ili tuwe sambamba nao tusiwadhulumu wala wasitudhulumu HAKI SAWA KWANANI .....SOTE

    ReplyDelete
  5. hii ni hali mbaya sana, imani ya wananchi kwa polisi imekwisha kwa kuwa matendo ya polisi kupiga na kuua raia yanaongezeka bila kuchukuliwa hatua kali kwa hiyo wameamua kuchukua hatua wenyewe!!!Nchi ikifikia hapo ni balaa tupu hasa kwa kuwa polisi wengi wanaishi uraiani.

    ReplyDelete
  6. Maumivu ya kichwa huanza polepole.......

    ReplyDelete
  7. Sasa kama ingekuwa gesi ipo Kigoma au Petrol iko Ruvuma nyinyi watu wa Mtwara na Lindi msingetaka kodi iwanufaishi Watanzania wote? Raia wa TZ anahaki ya kuishi popote. Kama anaona sehemu fulani ya TZ angehamia ili aishi vizuri basi afanye hivyo. Viwanda vitajengwa pale ambapo kutalate faida zaidi kwa kuangalia ammbo mengi.

    ReplyDelete
  8. Bado yatatokea mengi! Watu wana hasira siku hizi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...