Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

 1. Naunga mkono hoja ya mdau maana mafanikio yaliyotokana na uchimbaji wa dhahabu, almasi, rubi na madini mengineyo kwa mikoa na wilaya husika yako wazi kabisa.

  Hivyo sidhani kama ni sahihi kuvipa sifa vyama vya upinzani, kama baadhi ya watu wanavyodai, kwa kupambana na haya yanayotokea Mtwara.

  CCM Hoyeeeee!

  ReplyDelete
 2. Wewe kweli ni Dr? na ni Dr nini? vingineyo kabla ya kuandika fanya research ya kutosha, unasema mtwara na lindi hawana umeme wa uhakika wakati wao ndio mikoa ya kwanza kuwa umeme wa gesi kutoka Artumas na uwezo wa mtambo ni kubwa kuliko matumizi ya mikoa yote 2, jambo kama hulijui fanya research kabla ya kuja kwenye mtandao, tena mwaka huu wao walipewa fursa ya kupunguziwa gharama za kuvuta umeme kwenye nyumba kutoka laki 3 mpaka elfu 90, watu kama nyinyi ndio mnafanya issue ya mtwara iwe kubwa bila sababu

  ReplyDelete
 3. Mambo yasiyokubalika katika Mradi wa Bomba la Gesi Mtwara-Dar Es Salaam:

  1.Maendeleo ya upendeleo wa eneo moja pekee (Dar Es Salaam) pekee tumechoshwa nayo, tumechoka kusikia kila kitu ni Dar Es Salaam, Makao Makuu ya Serikali yapo Dodoma lakini Wizara zote zipo Dar Es Salaam, huku wengi wakikataa ama kusua sua kuhamia Dodoma.
  (TUNATAKA MAENDELEO YA KILA SEHEMU KATIKA TANZANIA YETU)

  2.Umbali huko wa kutoka Mtwara hadi Dar ni KM 586 ambapo inahitajika ujazo wa gesi katika bomba kwa umbali huo ili gesi ifike Dar Es Salaam, hivyo licha yakuwa pana makadirio ya kiwango cha 100TCF (100 Trilion Cubic Feet) ni kuwa gesi nyingi itapotea.

  3.Usalama wa Bomba la Mradi kwa kuvuja Gesi utakuwa ni mdogo kwa kuwa ni ghali kuweka ALD (Automated Leakage Detective Device Systems kwa umbali huo KM 586 na sijui kama imewekwa ktk Plan ya Mradi.

  4.Inaonyesha Mpango ni kuiuza Gesi ikiwa ghafi bila kuwa na Mipango endelevu ya kuifua Gesi ili kuiongeza Thamani na kuzalisha ajira, kwa kuwa Masoko ya Dunia na Kimataifa hununua Rasilimali zilizo ghafi kwa bei ya chini sana.(Inaonyesha moja kwa moja gesi hata kama itafika Dar ikazalishwa umeme, ile itakayouzwa itauzwa kwa bei ya kutupwa ikiwa (ghafi)un-processed.

  5.Waliobuni Mradi na Mpango huu(Bomba la Gesi Mtwara-Dar) inaonekana kabisa hawakuzingatia 'Economies of scale' (yaani Uchumi wa Kujikimu) kwa kuwa hawakuzingatia kanuni za Kiuchumi kwenye Master Plan hii.

  ReplyDelete
 4. Udaktari wa mwingine...Mmmh... Yaani unandika paragraph yenye mistari 7 bila kituo ama koma. Hata mtoto wa shule ya msingi asingeandika hivyo.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...