BAADA YA KUWA TANZANIA KWA KIPINDI CHA MIAKA 82, TOKA ENZI ZA BOAC, SHIRIKA LA NDEGE LA UINGEREZA YAANI BRITISH AIRWAYS LIMEAMUA KUITOSA RASMI TANZANIA,GLOBU YA JAMII INAWEZA KUTHIBITISHA!
HABARI ZA UHAKIKA TOKA JIKONI ZINASEMA NDEGE YA MWISHO YA BRITISH AIRWAYS KUTUA TANZANIA ITAKUWA MACHI 29, 2013 WAKATI BOEING 767 YA SHIRIKA HILO AMBAYO NI KIJEBA (ZINAZOKUJA HUKU ZINA UMRI ZAIDI YA MIAKA 20) ITATUA KWA MARA YA MWISHO.
NA KWA HUZUNI KUBWA KWA WADAU WAKE, OFISI ZA BRITISH AIRWAYS PALE SERENA INN JIJINI DAR ES SALAAM ZITAPIGWA KUFULI RASMI MACHI 31, 2013
Mkoloni hana adabu, yaani anatutosa bila noma, lakini pia ni AIBU yetu, miaka hamsini na ushee tupo zuba zuba tu, angalia wenzetu wa Ethiopia. Halafu siyo kama ngede zao zilikuwa zinasafiri tupu, la hasha, zilikuwa zina jaa kama enzi za "Chai Maharagwe". Waingereza wanausemi usemao "An opportunity is never lost, and opportunity lost is picked up and used by someone eles".
ReplyDeleteSerikali ya bongo, huu ndiyo wakati wenu kuifanya ATC iwe international, fuata nyayo za wahabeshi.
Nimejaribu ku-book flight baada ya mwezi machi 2013, na tovuti yao inasema hakuna route hiyo ya "kiwalani", na wakani-redirect kwenye route nyingine, kupitia wapi? you bet right, kwa watani wetu wa jadi, halafu KA au Precision wataku-peperusha mpaka kiwalani, na wakati wa kurudi vivyo hivyo- kiwalani- kwa watani wa jadi halafu londodo. Mie nasusia BA, hamtaniona tena, ntakuja na wahabeshi au wamanga.
ReplyDeleteHii sio Habari nzuri kwa wasafiri wa anga maana sasa price will go sky high kwasababu hakutakuwa na competition ya kutosha tuombe wengine waendelee (Swiss, KLM, Qatar, Emirates,Ethiopia, Egypt, THY) wasije wakawafuata BA.
ReplyDeleteNini kinaedelea kati ya BA na Bongo yetu mungu anajua.
Mdau
Mlomry
ATCL changamkieni njia hiyo.Turkish airline ndiyo wamewaharibia Biashara hawa watawala wetu
ReplyDeleteHii habari si nzuri hata kidogo kwa uchumi wetu. Lakini hata mmeshindwa kudodosa na kutuja what is the reason behind?
ReplyDeleteSasa Tunaposema tumepiga hatua kimaendeo maana yake nini? BP wamekimbia, British Airways shirika bora kuliko yote duniani linaondoka, baadhi ya balozi zimebadili utaratibu kupata viza mpaka uende Nairobi. Tujiangalie Vurugu zisizo na mantiki zisije kuwa ni kisababisho.
ReplyDeleteUK imekwisha sasa. Kazi zilizokuwa wabongo wakiringia sasa zinagombaniwa na watu kutoka Poland, Latvia, Estonia, Romania, Bulgaria,na wengineo. Kuna mashirika kibao ya ndege sasa duniani tena bei zao poa kuliko hao BA.
ReplyDeletewazungu wako hoi , uchumi unazidi kuporomoka, hali ni mbaya hawakuondoka kwa kupenda, UK hukosefu wa ajira ni balaaa, sasa unategemea nini. Hali kwa kweli ni mbaya sana kwa wazungu, Uingereza ni ya pili kwa kudaiwa na China baada ya Marekani, what do you expect, tatizo wazungu uchumi wao ulijengwa kinyonyaji sana sasa dunia imeamuka hawana wa kumnyonya wamebaki vibaraka wachache Africa lakini Asia, China na India hata Latin America hawana lao tena na hii ni moja ya sababu wao kuanguka msomeni Dr. Dambisa Moyo kwenye kitabu chake, The west was lost mtapata nondozzzz za kutosha, siku hizi wazungu kibao wanabeba mabox, kubeba box imekuwa kawaida kwa mzungu ndiyo maana na wengi wanawachukia WaAfrica maana ndiyo ilikuwa kazi yao.
ReplyDeletewashafilisikaa hawawezi kukeep up na competition.
ReplyDeleteDuh, this is bad! So they are joining SAS, Lufthansa, Sabena, AirFrance etc katika kufunga virago!!
ReplyDeleteGoodbye BA....infact we dont need you anymore. There are better airlines now.
ReplyDeleteKifo cha nyani miti kuteleza!
ReplyDeleteSasa wajameni Shirika limekuwepo nchini kwa miaka 82 umri wa Babu Mzaa mama au baba na leo linafunga virago?
Au ndio Bongo imekuwa pagumu Kimauzo na Faida?
Wacha wanende zao baada ya Karne ya mavuno ya faida!
ReplyDeleteHaya Mashirika yanaimarika sehemu za Dunia zenye ukosefu wa Nishati kama Gas and Oil kwa kisingizio cha kuwa NAULI ZAO ZIWE JUU KWA AJILI YA GHARAMA ZA MAFUTA NA KODI.
Jamaa wamesoma alama za nyakati wakaona Gas yetu ni asilia saba ba ni rahisi kuibadili kuwa 'HELIUM' yaani mafuta ya ndege, HIVYO LICHA YA KUHUDUMIA KWA KARIBU KARNE NZIMA WAMEONA PIA USHINDANI UTAKUWA MKUBWA KUTOKA KWENYE MAKAMPUNI YA DUNIA HASA YA MAREKANI NA KANADA AMBAYO YANA MKAKATI WA NAULI ZA CHINI SANA.
HIVYO TUSISHANGAE KUSIKIA BAADA YA MIEZI SITA KUONDOKA WAO WANAKUJA MASHIRIKA KIBAO YA MAREKANI NA KANADA!!!
waaache wasije sisi tutapanda Egypt air way inatosha na zingine,,kwani faida si ilikuwa wanapata ,wanaleta siasa wasibembelezwe hao tena ,wanataka kubembelezwa kama watoto wadogo hao watu wazima waacheni ,,uone kama hawatokuja kuja wenyewe kuomba
ReplyDeleteOhooo!
ReplyDeleteWakongwe British Airways wanaondoka?, SASA TUJIANDAE KUSAFIRISHWA NA WAGANGA WA KIENYEJI KWA UNGO!!!
Wacha waende zao!
ReplyDeleteHakuna sababu ya kuwa na huzuni wala nini, yatakuja mashirika yenye kuheshimu wasafiri angalia sisi wanatubeba kwenye madege ya zamani miaka 20 umri nyuma!
Ahhh wapi!
ReplyDeleteWameona ATCL imeingia Mkataba na Oman wamejua Ushindani utakuwa mkubwa hivyi wameona wafunge virago!
Hamjui hawa na mashirika mengine fulani (kwenye mabano) ndio walikuwa wanga wakubwa wa maendeleo ya ATCL?
na waende.
ReplyDeletemdau
ujiji kigoma.
Bora waondoke ba Nauli zao za juu kwa kuwa hawa ndio watafanya ATCL iruke sasa baada ya kuidumaza kwa miaka na miaka!
ReplyDeleteIlikuwa kama vile BA ndio Shirika letu la Taifa la ndege!
Nauli zao ziko juu sana toka LHR-DAR. KLM wamewafunika sana kwenye soko la tanzania, walifanya makosa makubwa kujitoa kwenye ile route ya LHR-JRO-DAR.
ReplyDeleteWAMESHANYONYA NA SASA WANAONA UTAMU HAKUNA TENA SO WANAJIKATA UTAMU UKITOKEA TENA WATAKUJA TU, THEY DONT HAVE PERMANENT FRIENDSHIP THEY HAVE PERMANENT INTEREST MKAE MKILIJUA HILI WABONGO WENZANGU.
ReplyDeleteWACHENI WATURUKI WARUSHE NDEGE ZAO BEI TENA BEI POA SI MNACHOKIPENDA
wamekosa biashara. Vitu vya ni ghali sana!
ReplyDelete
ReplyDeletewabongo hawana hela ya kupanda BA acha wabaki qatar, emirates nad ethiopia air lines
kijema KLM bado atabaki tuu akifunga na yeye basi ujue kuna jambo
safi sana.bado emirates,qatar,turkish nk
ReplyDeleteWaondoke tu waache maringo yao hawa...!!
ReplyDeleteInasikitisha hasa kwa sisi tuliopo nje ya inchi kwani inapunguza upinzani wa kibiashara na hivyo ticket zinaweza kuwa bei juu. Je, Mr. Michuzi unaweza kututafutia sababu za maamuzi ya BA kusitisha huduma hapo? Itabidi sasa kutua kwa watani wetu wa jadi pale Nairoo!!
ReplyDeleteDaaa nakumbuka ndio ndege yangu ya kwanza kutoa gundu na kwa safari yangu ya kwanza kutoka TZ kwenda ushokani.Baada ya hapo aaahhh mbona mambo ya kawaida sana tu.
ReplyDeleteEthiopian Airline (ET) has agreed to provide full support to Tanzania Tourist Board (TTB) in terms of organising international tourism trips and road show in the Pacific’s, Europe, Asia and America to promote the country as a tourist destination in the world.
ReplyDeleteGeofrey Tengeneza, TTB's Senior Public Information Officer told The Guardian that this was revealed that TTB ET recently signed a two-year pact under which the latter would promote Tanzania abroad for the two’s mutual benefits.
David V
Tumieni thy turkey airline hao wakoloni bei yao iko juu, wamechemsha kwa mturuki, wazalendo tunataka unafuu sio jina, tumieni wahabeshi pia au egypt air wako cheap pia, kwa ujumla hatu regrate kwa ba kusitisha safari kwani hazijahathiri lolote, wamejistukia
ReplyDeleteNimesikitika kuisoma habari hii.. :(
ReplyDeleteLabda sababu ni hii:
Flight ya BA kutoka Lusaka ilibidi ishushwe mjini Entebbe sababu ya engine kuzimika. Route ya Bongo pia inatumia aircraft aina ile (767).
http://avherald.com/h?article=45c24847&opt=0
Ningependekeza hata waje siku 1 tu kila wiki..
Ali..
UK.
mimi naona profit ndio tatizo na british airways awawezi kupunguza bei zao hata kidogo kwanza kama wewe masikini kama mimi bora upande egypty au oman na kasheshe yake mnaijua kwa hivyo wameona bora wakate safari za tz maana kunafaida gani yakwenda na ndege tz wakati wakifanya safari mbili tu za hapo kenya zinatosha ndege inatumia mafuta sio gas, na sasa hivi ngege kibao zinakuja bongo nani hatapanda BA.faida haipatikani, airport yenyewe tu mbovu,tax kubwa,mlete ndege zenu kufanya nini?
ReplyDeletenastikitika baadh ya maoni et BA ndio ndege bora dunian kasema na nan top five Ba haimo cha ni role ni ngumu na bei zao ziko juu ukilinganisha na ndege nyingine chepest class usd 1200.00 wakati wenzake wako usd 850.00 cha pili huduma zao na mwisho ni transist visa kwa wabongo kwenda ulaya nchi yeyote ile hii ndilo tatizo kubwa watu kutoipenda BA, ASANTE
ReplyDeleteMmh,wanaondoka kwa kuwa wanaona bongo biashara haina maslahi uchumi upo chini Mungu inusuru Tz
ReplyDeleteNitawamiss sana BA jamani nimeitumia nikienda likizo huko kwao.
ReplyDeletePia raha yake ni bei ya extra luggage hakuna ndege nyingine kubwa duniani iliyo cheap kama wao.
ndugu yangu juzi amesafiri kuja amebeba mizigo mingi, watoto na car seat zao ailikuja bure + push chair bure mtoto yoyote under 11 years I think.
BA wamejiunga na ndege ingine kubwa huko Europe ila lazima ni tatizo kubwa kwetu yaani hata minister wa mambo haya aongei kusikitishwa na habari hii.
ukijaribu ku bok ticket mwisho ni tarehe 29/3/2013 hakuna fligths za kuondoka Dar baada ya tarehe hiyo sku ya Ijumaa. I guess kutakuwa na sherehe hapo Airport siku hiyo asubuhi na wafanyakazi wao watarudi nayo kama passengers as watakuwa wamechoka. au watabukiwa flight ya kampuni ingine.
Bye bye BA nitakumiss airmiles zangu nitatumia parteners wenu au nyie kwa route za huko huko muendako.
SHAME ON TANZANIA KULIPISHA VOLUNTEERS LOTS OF MONEY.
HAMJUI KUWA WAO WANAPOTUMIA PESA KWENYE NCHI NDANI NDIO PESA ZINAINGIA? MNATUMIA PESA KUTANGAZA UTALII WAKATI NI HAKUNA KITU.
Ukifuatilia sababu mnaweza kuwagomea au? mnataka kuandamana huko mnakobebea maboksi? Njooni nyumbani Ooo tikiti zitapanda. kuna mapipa kibao hapa! BA sio wenyewe tu! Yaani bila wao hatutafika au? Waache waende washashiba! Si kazi yetu waTZ kuwalisha mapebari! tena hata hamjitambui!
ReplyDeleteDah! niliizoea sana hii ndege sana tu! roho imeniuma sio siri! tunategemea Delta na wengine watatinga hivi karibuni, ndege za wamanga kama Qatar siipedi hata kuiskia wanachana mabag ya watu na ushindwe kutumia tena ! afadhali Emirates sijui wengine ... Ila Kaka michuzi these are not breaking news, to me they are HEART BREAKING NEWS ...
ReplyDeleteHakuna Lolooote!
ReplyDeleteWengi wanaolalamika humu ni WASAFIRI WA MASANGA ,mliogopa kusikia ATCL inasaini ushirikiano na Oman Air majua kwa sasa MTAKUTA THEMOSI ZA CHAI NA MAANDAZI ndani ya ndege badala ya VIBUYU VYA POMBE KALI ndani ya ndege!
Mseme tu ya kuwa British Ariways walikuwa wanahudumua sana ndani ya ndege zao POMBE KWA WASAFIRI !!!
Manao ogopa kuondoka kwa British Airways ni POMBE tu za ndani ya ndege mtazikosa!
ReplyDeleteWengi mmeona ule Mkataba wa ATCL na Oman Air mkajua sasa NDANI YA NDEGE ZA KUSAFIRI KIMATAIFA KWA TANZANIA MTAKUTA CHUPA ZA KAHAWA CHUNGU ISIYO NA SUKARI NA CHUPA ZA CHAI NA MAKAPU YA MAANDAZI !!!
Kiboko ya Waingereza kwa Usafiri wa Kiwango cha juu na gharma za chini ni Mashirika ya Marekani na Kanada ndio yatamiminika nchini muda sio mrefu.
ReplyDeleteKwanza BA wamesoma nyakati wamekuata watakabiliana na wapinzani ambao wengi wao ndio Mashirika ya US and Canada ndio yamewekeza sana na yanazidi kuja katika MIPANGO YA GESI MAFUTA NA MADINI !
sababu zao ni za kiusalama zaidi, tanzania ni nchi moja inayoelekea kwenye hatari, majasusi yao wameshaona kuna janga linakuja
ReplyDelete"gonjwa la kukurupuka kutoa kasoro",bado tatizo kubwa sana hapa bongo!British Airways has been here for the last 82 years,since the days of darkness airline technology,few countries could operate by then!Huu ulikuwa,kwanza,wakati wa kutoa shukrani zetu kwa huduma zao kwa kipindi chote hicho!No doubt,kupitia kwao,walichangia sana katika maendeleo ya nchi yetu.Pili,wabongo mnatakiwa kutafiti kwanza na kutafakari sababu zilizo sababisha wajitoe katika hii route yetu,je,wapo katika zoezi la kupunguza gharama za uendeshaji wa Kampuni yao kwa kuanzia na zile Route ambazo hazina wateja wa kutosha?au katika zile Route ambazo gharama zao pamoja na kodi za viwanjani ni kubwa mno?Au katika zile Route ambazo hawapati "vivutio vyovyote maalum (special attractive packages)kuifanya shughuli yao iwe na faida?",au ni sababu zipi hasa? Katika biashara,kanuni ya kwanza kabisa,ni "kupata faida".Huduma baadaye.Hakuna Kampuni yoyote duniani ambayo itakubali kurusha ndege zake kuja Bongo,iwapo,haipati biashara ya kutosha kurejesha gharama za uendeshaji!Cha muhimu hapa,kwa "Wagumu Wetu",waanze kujipapasa, "Mchumba"amewakimbia,kuna matatizo gani ndani ya nyumba,ambayo majirani si rahisi kuyajua?Kisha wajirekebishe na kusawazisha mambo!British Airways itarudi tena!Lakini,kama inaweza kuishia Nairobi kwa faida,na wanaounganisha safari kuja Dar hawatapata shida ya kuunganisha safari,basi mjue tumeumia!Tusikimbilie Lawama,Kwanza Tuchichunguze,nani kajipaka "Kinyesi!"
ReplyDeleteHakuna uwanja wenye sifa jamani wazungu wanachoka hamna hata kiyoyozi majirani zetu waliochelewa kupata uhuru wametuacha!Bongo inanuka rushwa!!
ReplyDeleteIla jamani anagalieni watakuwa hawachangii tena BAJETI yetu jamani kwani naye ndio mdau mkubwa wa bajeti!! msiongee mkamaliza jamani nyieasipochangia bajeti sasa inamana migomo ya wafanya kazi itazidi sasa balaaa.
ReplyDeleteWabongo kwa kashfa hatujambo,BA hata mtukane ilikua inasaidia sana,hao wengine angalieni bei zao na mda wa kufika dar,Airport mnayoita International hali yake ni tete,viyoyozi hakuna,mvua ikinyesha mwaweka ndoo,mabakuli kukinga maji,kwa nini msilaumu uongozi wa nchi,kazi wizi tu.BA watawatupa kenya kwa bei ile ile na mtapanda tu.kama mnaweza kamateni mitumbwi.na ndege zao hazitasimama.
ReplyDeleteSasa Tunaposema tumepiga hatua kimaendeo maana yake nini? BP wamekimbia, British Airways shirika bora kuliko yote duniani linaondoka, baadhi ya balozi zimebadili utaratibu kupata viza mpaka uende Nairobi. Tujiangalie Vurugu zisizo na mantiki zisije kuwa ni kisababisho.
ReplyDeleteThu Jan 17, 06:05:00 pm 2013
..................................
WEWE ULIYESNDKIKA HAPA UNATAKA useme kwamba Tz kuna vurugu kushinda Kenya? Acha zako hebu tafakari usituchefue!
Jonathan Maarufu anony wa Fri Jan 18, 06:46:00 am 2013
ReplyDelete...Mmh,wanaondoka kwa kuwa wanaona bongo biashara haina maslahi uchumi upo chini Mungu inusuru Tz...
-----------------------------------
Inawezekana una mitazamo yako ya Kisiasa!
Ebo ati nini?
Uchumi wa Bongo upo chini?
Bwana Mkubwa hivi huwa unapitia taarifa mbali mbali za Mashirika kama WORLD BANK na IMF?
Kwa taarifa yako Uchumi wa Tz unakuwa kwa kasi ya ajabu Duniani!
Wastani wa Dunia ni 5% lakini sisis tupo juu ya wastani kwa kuwa na kiwango cha 7.1% !!!
Jonathan Maarufu,
ReplyDelete=-===
Mmh,wanaondoka kwa kuwa wanaona bongo biashara haina maslahi uchumi upo chini Mungu inusuru Tz
=====
Waingereza walitudhika kwa udhaifu wetu kwa makarne yote hayo, na sasa ushindani umewakamata na kwao Uchumi umeyumba ndio maana wanaondoka!
Kwa nini Makampuni yao mengi ya Utafiti na Uchimbaji mafuta na gesi BG (British Gas), na BP (British Petroleum) yanamiminika kuja huku kama TZ haina Uchumi?
Mdau wa friday 18 10:39..... yani wewe unaonekana unachangia mada lakini huja wahi kupanda pipa kabisa... nani alikuambia oman air su emarat su qater airways hawa serv pombe kwenye ndege...unadhani ni BA tu ndio wanapombe.. kwa taarifa yako hizo ndege za kiarabu zina gawa pombe za kila aina ndani ya ndege hata mwezi wa ramadhani.... unaonekana huna mazoea ya kupanda pipa na kama ulipanda labda ulipanda hizo local internal flight.....usiseme usilolijua ni aibu..
ReplyDeleteMdau wa 47 hapo juu anony Fri Jan 18, 08:05:00 pm 2013
ReplyDeleteMakampuni ya Uingereza ya kutafiti na kuchimba Gas na Oil ni mengi ya yanazidi kumiminika, huku yakitolewa kamasi vibaya sana kwa Uhsindani wa Mitaji na kugombea Tenda na ya Canada, Marekani, Norway na Australia!
Ya kwao ni
1.Tullow Oil PLC.
2.British Gas (BG)
3.British Petroleum (BP)
4.Pan continental Energy PLC.
5.Ophir Energy PLC.
Sasa wakisema na kudai Bongo hakuna uchumi kama Mdau mwenzetu humu Jonathan Maarufu ukweli uko wapi ikiwa Makapuni ya uwekezaji ya Nishati ya Uingereza yanahaha kupigania biashara na nafasi INA MAANA BA WAMESHINDWA USHINDANI UNAOTARAJIWA KUJA KATIKA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA NCHINI TANZANIA, KWA MTAJI HUU TUTEGEMEE MASHIRIKA MENGINE KUTOKA AUSTRALIA, MAKEKANI NA CANADA !!!
Wamefilisika Tanzania inagombewa kama mpira wa kona kutokana na mimali iliyogundulika!
ReplyDeleteHivyo nchi zinazokuja na mashirika ya uwekezaji ktk Gas, Oil na Minerals zitaalika pia makampuni yao ya usafiri wa anga, tena madege ya maana sio ndege vijeba za miaka 20 nyuma.
Tutanda sasa ndege matoleo mapya kamajumbo jets 2012 and so on!
Muingereza kwa dharau?
ReplyDeleteHana mpinzani, nakumbuka Baba wa Taifa liakutana na Malkia akiwa amevaa Glovu mkononi akanyoosha mkono kushikana na Julius, ili kuonyesha kuwa ana akili nzuri Julius akanyoosha Kifimbo chake!
Ndio Malkia akapata akili akachomoa Glovu na ndio JK akashikana naye kusalimiana.
Sasa hawa watu wanataka tuwe na msimamo kama alivyowafanyia Julius kwa Malkia wao!
Waende zao BA kwanza wametudharau kwa kutubeba kwenye ndege za zamani!
Tunataka Mashirika yanayotumia ndege mpya kwanza wameshindwa hata na Precision Air yetu Tanzania inatubeba kwa ndege mpya.
Tanzania imepanda hadhi Kiuchumi, na sio kuwa uchumi umeshuka kama baadhi ya watu wasio Wachumi na wafuatiliaji wa mambo wanvyodai humu.
ReplyDeleteSasa ina maana kupanda hadhi Kiuchumi na pia Ushindani unakuwa ni mgumu, Waingereza BA wameliona hilo na ndio maana wameogopa aibu wananyanyua jamvi lao na mapema wasije adhirika.
Kama sababu za kuondka Tanzania hakuna biashara na uchumu umeshuka katika Sekta ya Biashara ya Usafiri wa anga JIULIZENI mbona Makampuni ya uwekezaji wa Sekta ya Nishati na Madini ya hiyo hiyo Uingereza yenye BA yanagombania uwekezaji hapa TANZANIA?
Na hii bongo imezidi sasa na hawa wanasiasa uchwala. wasio kuwa na mwelekeo bali, wameona njia rahisi ya kujipatia kipato ni siasa, na wale wenzangu na mimi, wasienda shule wakizungumziwa kingereza kidogo, na kumwagiwa tupesa kidogo, ohhh basi alakahalaka wanamchagua, michosho sana hii, kwani inachangia, kupolomoka kwa uchumi, watu waende shule, ndio na wawe wanasiasa, ndio watajua kuingoza nchi, na kakabiliana na wakati
ReplyDelete