Ankal, Wawekee wadau waweze kuiona meli hii ambayo ni Mojawapo ya meli kongwe hapa nchini,Hii ni Meli ya MV. Victoria inayosafiri kati ya jiji la Mwanza na mji wa Bukoba, MV. Victoria ambayo ilianzarasmi kufanya kazi mwaka 1962 na bado inadunda mpaka leo pamoja na changamoto nyingi, tuangalie video ya hali halisi ya uendeshaji wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. jamani na hii pia mna taka itokee kama mv bukoba haistahili hata kwenda popote ni risk mna hatarisha maisha ya watu.itoeni au mnunue mpya hela zina kwenda wapi nunueni hata kama ya azam.meli yote ni giza kama upo shimoni.mpaka naogopa.hivi nyinyi macaptain roho zenu hamzitaki.naandika kwa uchungu.zito kabwe achana na mambo ya gesi fwatilia hili.watu wakizama elfu 2000 ndio utaanza kuongea anza sasa na hili.

    ReplyDelete
  2. KWA NINI!????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. KWA NINI???!!!!!!!!!!!!!!! KWA NINI???????!!!!!!!!!!!!!!. HII MELI INAJAA KILA SIKU OVER CAPACITY. VIPI WAMESHINDWA KUBORESHA MAZINGIRA?????? PESA IMEJILIPA ZAIDI YA MARA 50 VIPI UNAWEZA KUTOKWA NA AIBU UKAONYESHA UCHAFU KAMA HUU KWA DUNIA??? AIBU AIBU AIBU. WIZI WIZI WIZI. HUWEZI KUNIAMBIA SABABU YOYOTE KWANINI BAKHRESA ANAONGEZA MELI KILA MWAKA AKIWA NA 70% CAPACITY WAKATI MELI HII WITH 110% CAPACITY HAIJABORESHA HUDUMA ZAKE TOKEA 1962. AIBU AIBU AIBU!!

    ReplyDelete
  3. I would advice them to get a new ship man. This ship is too old, and we shouldn't wait until it goes down with our innocent citizens. Then, we will be the first ones to comment here. Come on! "prevention is better than cure"

    ReplyDelete
  4. wewe anonymus wa jan 22 at 12:22:00
    Umesema una washauri wapate a new shipman maana hii ship imezeeka.Ha ha`ha what do you mean?nini kimezeeka the ship man or the ship it self?

    ReplyDelete
  5. Mwakyembe umeona?? Tanzania sio Dar peke yake nenda huko kaokoe roho za watanzania wasio na hatia wanasafiri kwenye Floating Coffin hilo.

    ReplyDelete
  6. Yaani mikungu ya matoke imefurika namna hiyo hataka kama watasema uzito haujazidi lakini upakiaji wa mizigo dizaini hiyo inaweza ku-destabilize' meli haswa kama kuna mawimbi makubwa kupita kiasi au upepo mkali.

    Hapo mikungu ya ndizi na viroba ilipowekwa palitakiwa pawe wazi ili kama kuna kuchafuka kwa ziwa Victoria mawimbi makubwa yanakatiza au kuangukia sehemu hiyo ya kurejea ziwani bila kuitikisa meli kwa mawimbi.
    Mdau
    Baharia Mwandamizi wa Bahari Kuu

    ReplyDelete
  7. ndo upuuzi wako weye huyo kasisitiza jambo kwa kusema get a new ship man! ni serikali man.acha kuangalia mambo madogo unatutoa kwenye mada kabambe kingereza chako cha upande mmoja cha kukariri chana nacho aibu yako.la msingi ni kwamba serikali lioneni hilo walau mzungumze kuandaa bajeti yake inatoa mtazamo hata kwa waendeshaji kujua kwamba hiyo siyo meli wapunguze tamaa za kubeba mizigo mizito zaidi,Haya jameni.

    ReplyDelete
  8. DR MWAKEMBE TAFADHALI LIPE KIPAU MBELE USAFIRI WA ZIWA VICTORIA. MELI MJA, IMECHAKAA, INAJAZA SANA,INASAFIRI MRA3 TOKA BKZ NA MARA 3 TOKA MWZ. HALI YA HATARI INAKUJA,JUKUMU LA SERIKALI. DAR MWAKEMBW TATUA

    ReplyDelete
  9. Hallo wadau...
    Jambo meli hii ni nzee kupita kiasi lakini bado inabaki meli salama zaidi ziwa victoria. Kama ni kutoa hii meli basi shirika la meli alitakuwa na meli ya kubaki, wana meli kwa jina mv clerias hii ndo balaa mwenye akili ata kupanda uwezi jaribu hiyo nyingine kwa jina la mv serengeti nayo balaa.
    Sasa hiyo mv serengeti imekuwa meli ya mzigo.
    JK kumbuka ahadi yako kwa wana bk. Ben Mkapa alitoa ahadi haikutimia mpaka kamaliza awamu yake... wadau mimi napita tu.

    ReplyDelete
  10. natoa pendekezo,meli hiyo ya Mv Victoria sasa igeuzwe kuwa Hoteli ya Kitalii,hapa hapa jijini Mwanza ikiwezekana au popote pale,iwe Bukoba au Kemondo,kulingana na soko la wateja!Na ikiwezekana,itangazwe kwenye open tender ili wenye uwezo na nia ya kufanya biashara hiyo wajitokeze kuinunua!Hata kama ni foreign investors!Pesa zitakazo patikana,ziwe down payment ya Mkopo wa Benki,ukipewa financial boost na ruzuku ya serikali kuu,ili,Meli nyingine Mbili za Kisasa ziweze kununuliwa.Meli moja itakuwa na Abiria,na ya pili,ya Mizigo!Lakini,wakati huohuo,wawekezaji Binafsi wahamasishwe kuwekeza katika Usafiri wa Meli katika Ziwa Victoria,LAKINI PIA,katika ziwa Tanganyika,ambako nako ni Aibu tupu,na katika ziwa Nyasa,ambako ni balaaa!Utashangaa,na uendelee kushangaaaa,ukiambiwa kwamba,hata katika ukanda wa bahari ya Hindi,Tanzania haina Meli za kisasa na za kuaminika kwa ajili ya abiria na mizigo,kati ya bandari zetu za Tanga,Pangani,Wete,Chakechake,Mkoani,Bagamoyo,Mafia,Rufiji,Kilwa,Lindi na Mtwara;mbali na Lamu,Mombasa,hadi Maputo na Afrika ya Kusini!Hivi nchi hii tuna Viongozi kweli?sick and tired!

    ReplyDelete
  11. tanzania! africa! gotta get used to this. Otherwise

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...