Mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa jengo la Uhuru Heights,Balozi wa Pakistan nchini Tanzania,Tajammul Altaf akizungumza katika uzinduzi huo ambapo amasema amefurahishwa na jitihada zilizofanywa na mfanyabiashara kutoka nchini kwake na jinsi Tanzania ilivyoweza kumpa ushirikiano na hatimaye sasa matunda yameonekana kwa kuzaliwa jengo la Uhuru Heights lenye hadi ya Kimataifa.Aidha amesema huo ni mwanzo tu na kuwataka wafanyabiashara zaidi kutoka Pakistan kuja kuwekeza Tanzania kwa sababu mahali ambapo ukiwekeza matunda yanaonekana kutokana na amani na utulivu uliopo na ushirikiano wa serikali.
Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights, Muhammad Owasi Pardesi akizungumza na wageni wakati wa uzinduzi wa jengo hilo na kutoa shukrani zake akisema sasa wakazi wa Dar es Salaam wataweza kununua nyumba kwa njia ya mkopo kutoka Benki ya International Commercial (ICB) na kulipa kwa muda wa miaka 10 na kuishi katika miongoni mwa majengo marefu ya makazi yaliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam lililojengwa kwa gharama ya Dola za Kimarekani Bilioni 40.
Amesema Malengo ya kampuni ya Cosmos Group ni kuboresha miundo mbinu na maisha ya watu na hayo yamezingatiwa kwa kujenga jengo la Uhuru Heights.
Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser Mohamed (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya EXIM Anthony Grant (kushoto) ikiwa ni ishara ya kuingia mkataba wa kufanya biashara pamoja baina ya Cosmos, IBC Benki na Exim.
MC katika uzinduzi wa Jengo la Uhuru Hegihts Taji Liundi.
Muonekano wa Jengo la Uhuru Heights lililopo barabara ya Bibi Titi Mohammed liking'arisha jiji la Dar nyakati za usiku.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Si amini kwamba jengo imegharama US$ 40 BILLION! (mara 4 ya bajeti yetu!!) nadhani walimaanisha TZS 40 billioni..
    Ali..
    UK.

    ReplyDelete
  2. Dolla million 40 au Billion 40. Hawezi kuwa dolla billion 40 hata kwa dawa ni nyingi hizo.

    ReplyDelete
  3. US $40bn mchezo??? Labda kama liko huko Manhattan lkn sio bongo

    ReplyDelete
  4. Hilo jengo ni kiboko $ zito hizo, limejengwa kwa dhahabu tupe?


    ReplyDelete
  5. Hujui watanzania ni mabingwa wa kuongeza sifuri? mradi unakuzwa mara aidha kumi, mia au elfu kwa hiyo usishangae. Kama umeshafanya kazi serikalini huo ndio mchezo wao kuongeza ongeza hiyo misifuri yao, kila kitu ni ku-inflate. Sijui kwanini michuzi hakuliona hilo? au na yeye yumo huko serikalini?

    ReplyDelete
  6. naungana na mchangia maoni wa kwanza, jengo hilo haiwezekani kugharimu US$ 40 BILLION. kwani jengo refu duniani ni BURJ KHALIFA LA UAE na limegharimu US$ 1.5 BILLION, itakuwa mwandishi kateleza.
    FMB
    UK.

    ReplyDelete
  7. Yeah anko kateleza, naona uchovu wa safari matokeo yake kaandika kifaransa . bilioni arobaini sio mchezo ankali

    ReplyDelete
  8. Hata jengo la Pentagon haligharimu $40 bilion.Rekebisha number.

    ReplyDelete
  9. Rekebisheni hiyo figure...labda ziwe ni dollar za zimbabwe! ZIM DOLLAR!!!!!!

    ReplyDelete
  10. ngoja tuangalie financial statements za ICB kama wanaweza kutoa loan ya US$ 40bn.

    Watz fursa hizi tuzione tusisubiri watu watoke abroad kuja kuinvest kwa kutumia fedha za mabenki yetu wenyewe tu.

    ReplyDelete
  11. Dola bilioni 40??? yaani unamaanisha sh trillion 64 (64,000,000,000,000)bajeti ya miaka minne ya Tanzania, Haiwezekani.
    Ankal naona unataka kusabakisha kuchafua hali ya hewa na kujeruhi hisia za watu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...