Kwa Niaba ya Familia ya Bi Arafa (Pichani) Napenda kutoa shukrani za
Dhati kwa wale wote ambao waliguswa na hali ya Mgonjwa huyu na
kuridhia kumchangia ili kumtoa wilayani Ruangwa na kuwezesha kumfikisha katika Hospital ya Muhimbili Mwezi Nov 2012 na juzi
kufanyiwa Upasuaji.
Hali ya Mgonjwa huyu inaendelea vema katika hospital ya Muhimbili
akisubiria kutoa Nyuzi
Mungu aliwawezesha na kumsaidia mpaka hali ilivyofikia sasa na Kubwa
Nawaomba Muendelee kumuombea Dua ili aweze kupona na kuendelea
kujitafutia riziki ya kila siku
Ahsanteni sana.
Ni Mimi Abdulaziz Ahmeid Video
Mungu akuponye kabisa urudi kulijenga taifa letu.
ReplyDeleteTunaomba basi ndugu yetu uliyefanikisha kupatiwa msaada kwa binti huyu utupatie picha yake baada ya kufanyiwa upasuaji
ReplyDeleteMola ni mwingi wa rehema,tunamwombea bi Alafa apate kupona haraka ili aweze kuendelea na shughuli zake kama kawaida.Amin.
ReplyDelete