Mkuu wa Jimbo Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Anta Muro akizungumza katika hafla ya kuangalia jengo jipya la Kitega Uchumi cha Kanisa la KKKT Usharika wa Msasani.
 Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiteta jambo Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malalusa.wakati wa  ziara ya kukagua jengo la kitega uchumi  la Usaharika wa Msasani, lililogharimu sh. bilioni 9.909 ambazo sehemu ya fedha hizo ni mkopo  kutoka CRDB. Benki hiyo pia ni sehemu ya wapangaji katika jengo hilo lenye ghorofa saba. 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malalusa.akizungumza wakati wa  ziara ya kukagua jengo la kitega uchumi  la Usaharika wa Msasani, lililogharimu sh. bilioni 9.909 ambazo sehemu ya fedha hizo ni mkopo  kutoka CRDB. Benki hiyo pia ni sehemu ya wapangaji katika jengo hilo lenye ghorofa saba. 
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki wakati wa  ziara ya kukagua jengo la kitega uchumi la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usaharika wa Msasani, lililogharimu sh. bilioni 9.909 ambazo sehemu ya fedha hizo ni mkopo  kutoka benki hiyo. Kushoto ni Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Dk Alex Malalusa na Naibu Katibu Mkuu Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Chadiel Sendoro. CRDB pia ni sehemu ya wapangaji katika jengo hilo lenye ghorofa saba. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akipokea ufunguo kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malalusa (wa pili kushoto) wakati wa ziara ya  kukagua jengo la kitega uchumi la kanisa hilo Usaharika wa Msasani, lililogharimu sh. bilioni 9.909 ambazo sehemu ya fedha hizo ni mkopo  kutoka benki hiyo. CRDB pia ni sehemu ya wapangaji katika jengo hilo lenye ghorofa saba.
 Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyo akipeana mkono na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malalusa.wakati wa  ziara ya kukagua jengo la kitega uchumi  la Usaharika wa Msasani, lililogharimu sh. bilioni 9.909 ambazo sehemu ya fedha hizo ni mkopo  kutoka CRDB. Benki hiyo pia ni sehemu ya wapangaji katika jengo hilo lenye ghorofa saba. 
 Mkuu wa Jimbo Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Anta Muro akiomba baraka. kwa ajili ya jengo jipya la Kitega Uchumi cha Kanisa la KKKT Usharika wa Msasani.
 Askofu Malasusa akitoa baraka.
 Mandhari ya Ukumbi wa mikutano katika jengo la kitega uchumi la Msasani Multpurpose Development Centre (MMDC)
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malalusa akikagua jengo la kitega uchumi la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usaharika wa Msasani, lililogharimu sh. bilioni 9.909 ambazo sehemu ya fedha hizo ni mkopo  kutoka benki ya CRDB. CRDB pia ni sehemu ya wapangaji katika jengo hilo lenye ghorofa saba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. jamani kwa nini hamuweki uwazi kwenye hilo jengo? hata kama crdb wametoa mkopo kiukweli na washarika tulijitoa sana hapo kwenye ujenzi kila jumapili kuna bahasha ya sadaka ya jengo kwa muda wa miaka saba, usharika una watu zaidi ya watu elfu tatu. tunapofanya kitu kizuri mjaribu kushirikisha na washarika na si kuwatenga jambo linapokamilika kama hivi. siyo crdb pekee wamehusika na washarika wote wa msasani wamehusika kwenye ujenzi wa jengo la kitega uchumi.

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana KKKT pamoja na CRDB lakini angalieni sana yasije yakawa kama yale ya KKKT Arusha!

    ReplyDelete
  3. Inabidi liwekewe bima ya maana hili jengo la (KKKT)

    ReplyDelete
  4. Hizi Bank na Hii Mikopo ni Ruksa kwa wote! Ukilaza damu, ujilaumu mwenyewe na siyo kushikia bango walio jitosa na kufunga mikanda kulipa madeni

    ReplyDelete
  5. Haya sasa hii ni changamoto chanya kwa wale wenzetu wenye Imani fulani,jifunzeni kutoka kwa hawa ndugu mnao waita WAGALATIA.
    Msiishie kwenye maandamano yasiyo na tija na kuchomea wenzenu MAKANISA yao!wakati umefika sasa nanyi mfunguke macho!..... message sent and delivered!!!! lol

    ReplyDelete
  6. SAFI SANA! CHEZEA JESUS WEWE?

    ReplyDelete
  7. Hili ni jambo la kheri na la kupongezwa sana!Pongezi sana Kwa Dr.Kimei kwa ubunifu mkubwa alioufanya,na bila shaka "kwa mkono wa Mungu" hilo limewezekana!Pongezi za dhati kwa Dr.Malasusa pia kwa kunyesha njia na uthubutu kwa rehema zake mwenyezi Mungu,hilo limefanyika!Ofcourse kwa wana Usharika wao,kwa kujitoa na uvumilivu mkubwa!Huu uwe mfano kwa Taasisi nyingine za Fedha na za Kijamii!Lengo la muda mrefu ni kuyafanya haya ma taasisi ya kiroho yafike mahali yaweze kujitegemea,hususan katika nyanja za kutoa elimu kwa wote,vyuo vya ufundi,na huduma za afya kwa gharama nafuu na huduma nyingine zote za kijamii!God Bless All!

    ReplyDelete
  8. hongera KKKT

    ReplyDelete
  9. Hongereni washarika wote wa Msasani na ahsanteni sana CRDB. Jamani washarika tumejinyima sana u need to recognize us, tunatoa michango kila jumapili, tulikusanya harambee ya charity walk wakati tunaanza mradi, nasikituka hamjatu-recognise...I hope muandishi amepitiwa, lakini nikiambiwa management ya kanisa ndo ilipitiwa kututaja nitasikitika sana

    ReplyDelete
  10. Anony wa 5, ki ukweli maneno yako uliyotumia ndio hasa yanakuwaga chanzo cha vurugu..nasikitika michuzi hajakupiga ban kwani wewe huna hata ndugu mmoja wa hiyo dini fulani unayoisema? Si vyema kuwaonyesha watu upumbavu wako kwani huko ni kujidhalilisha tu.Na pia ufahamu kuwa hakuna vurugu isiyo na sababu watu kama nyie hampaswi hata kuwepo duniani kwani mmejaa uchonganishi usio na maana.Ni bora upuuzi wako ukamuonyeshe mkeo na wanao nyumbani kwako na sio humu....mambo mengine hayaitaji shule na utambue kuwa kuichukia dini nyingine ni kupoteza muda wako..crap

    ReplyDelete
  11. ANON WA 5,

    KWENYE HILI BADO UKO NA MAWAZO YA MTOTO WA UMRI WA MWAKA MMOJA, UKO NA SAFARI NDEFU SANA KWENYE UFAHAMU WA MAMBO.

    ReplyDelete
  12. Hongereni sana SUMAJKT kwa kujenga jengo zuri na lenye mvuto.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...