Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amefanya ziara ya uhamasishaji utunzaji wa usafi wa mazingira kwa wakazi wa kata ya Ndugumbi, jijini leo (Jan 27). Pamoja na Mambo mengine ameahidi kuwa zoezi hilo litakuwa ni endelevu ambapo kila mwisho wa wiki, wakazi wanaoishi kwenye Kata mbalimbali za Manispaa hiyo watakuwa wakitekeleza zoezi hilo. Pichani ni zoezi hilo lilivyotekelezwa leo kwa viongozi na wakazi wa Kata ya Ndugumbi.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (Suruali ya njano) akisimamia uondoaji wa taka zilizokuwa zimetelekezwa pembezoni mwa Barabara ya Mandela.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda sambamba na viongozi na wakazi wa Kata ya Ndugumbi wakisafisha na kuzibua mitaro katika Mtaa wa Ndugumbi.


Meya wa Manipaa, Yusuph Mwenda (kulia) akimkabidhi shilingi 10,000 bibi kizee ambaye ni mkazi wa mtaa huo baada ya kufurahishwa na hatua yake ya kujitolea kufanya usafi wa mazingira.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda sambamba na viongozi wa Kata ya Ndugumbi wakikatiza mitaa mbalimbali ya Kata hiyo wakiwa na mifagio na machepeo.
Mifereji ilizibuliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Meya, huyo anayezibua anahitaji Buti pia (vitendea kazini muhimu ili kufanikisha zoezi hilo kuwa endelevu)

    ReplyDelete
  2. Meya wetu wa Ilala yuko wapi? Mitaa ya Ilala Bungoni, Amana, Buguruni inanuka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...