Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa akikata utepe wa uzinduzi wa maabara ya kisasa iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 49 ikiwa ni sehemu ya mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola wilayani Uyui wakati Waziri huyo alipotembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyotekeleza mradi huo. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uyui,Said Shaban Ntahondi na kushoto ni Mbunge wa Jimbo Tabora Kaskazini,Mh. Mamlo Shafin Sumar na wapili kutoka kushoto ni Kiongozi wa Mradi wa Vijiji vya Milenia wa Mbola,Dkt Gerson Nyadzi.
Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa (kushoto) akiongea na viongozi wa vijiji 16 vinavyotekeleza mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola jana wilayani Uyui juu ya kuufanya mradi huo kuwa darasa endelevu kwa ajili ya vijiji vingine nchini kwenda kujifunza juu ya utekeleza wa malengo 8 ya Milenia . Waziri huyo alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Katikati ni Mwnyekiti wa Halmashauri ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uyui mkoani Tabora Said Shaban Ntahondi(kulia) akimwelezea jana wilayani Uyui mkoani Tabora Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa (katikati) jinsi mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola ulivyosaidia kuboresha maisha ya wakazi wa eneo la mradi na hivyo kupunguza umaskini. Kushoto ni Mbunge wa Tabora Kaskazini Mamla Shafin Suma.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha(kulia) akitoa maelezo mafupi jana wilayani Uyui mkoani Tabora kwa Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa(kushoto) juu ya mafanikio waliokwishapata katika utekelezaji malengo ya Milenia chini ya mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola. Waziri huyo alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uyui Said Shaban Ntahondi.
Mbunge wa Tabora Kaskazini Mamlo Shafin Sumar (katikati) akimshukuru Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kulia) jana wilayani Uyui kwa niaba ya wapiga kura wake kwa juhudi za serikali za kuidhinisha shilingi milioni 900 kwa ajili ya usambazaji wa umeme katika vijiji mbalimbali katika jimbo hilo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt Servacius Likwelile.
Viongozi na wananchi walioko katika mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola wakimsikiliza jana wilayani Uyui juu Waziri wa fedha Dkt William Mgimwa(hayupo pichani) wakati akiwahimiza juu ya kuufanya mradi huo kuwa darasa endelevu kwa ajili ya vijiji vingine nchini kwenda kujifunza juu ya utekeleza wa malengo 8 ya Milenia . Waziri huyo alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo.PICHA na GCU - HAZINA
Tuelezeni,Miradi hiyo ni ipi?Na iko mingapi?Je,kabla ya mradi hali iliuwaje hapo katika vijiji hivyo 16 vya mradi?Na sasa,baada ya mradi huo wa Milinea,hali ya vijiji ikoje,imebadilika kwa vigezi vipi?Maelezo kwa kifupi sana,ilil kusudi,hata wale walioko katika mikoa mingine,wapate picha na ufahamu utakao washawishi wafunge safari toka huko waliko hadi Uyui ili kujifunza!i think that would be fair to the target group!
ReplyDelete