
Mtandao wa FULLSHANGWEBLOG umerejea hewani usiku wa kuamkia leo mara baada ya timu ya wataalam wetu kukamilisha kazi ya marekebisho na tayari tulishaanza kumuvuzisha matukio usiku huohuo.
Tunasema
asante kwa uvumilivu wenu na kutuelewa kila mlipotupigia simu kuulizia
hali ikoje,tunawashukuru pia kwa simu zenu kwani tumejiona ni wenye
bahati na kumbe mchango wetu mnautambua vizuri asanteni sana wadau.
Tunatoa
shukurani kwa wadau wetu wawezeshaji Benki ya NBC, Benki ya NMB,NHIF,
TTB, SERENGETI BREWERIERS , WILNA INTERNATIONAL ,BAYPORTna R&R kwa
uvumulivu wenu tunasema asanteni sana na Mablogger wote ambao
walitusemea wakati tulipokuwa na tatizo hili.
Shukurani
za Pekee zimwendee Mustafa Selemani mtaalam wetu na timu yake kwa
kuhakikisha wanarekebisha tatizo hilo mpaka tunarejea tena hewani usiku
wa kuamkia leo tunakushukuru Mustafa na timu yako ya G5CLICK.
Mwisho
tunasema kazi inaendelea mbele na wadau wote mnakaribishwa kututumia
habari na matukio mbalimbali kupitia Email ya johnbukuku@gmail.com na
info@fullshangweblog.com nasi tutazimuvuzisha mtandaoni kama kawaida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...