Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Benin, Mheshimiwa Dkt. Boni Yayi amewasili nchini usiku wa jana, Jumanne, Januari 15, 2013, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, Rais Boni Yayi amepokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mara ndege yake ilipotua kiasi cha saa tano unusu usiku.

Kesho asubuhi, viongozi hao wawili watafanya mazungumzo rasmi kabla ya Rais Boni Yayi kuondoka nchini kuendelea na ziara yake Barani Afrika.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akimkaribisha mgeni wake Mheshimiwa Dkt.Boni Yayi wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu julius Nyerere usiku wa jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Dkt.Boni Yayi wakifurahia jambo katika hoteli ya Kilimanjaro.(picha na Freddy Maro).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ankalumekuwa na kawaida ya kubana comments zangu ninapoongelea serikali.Ila sitaacha kutoa comments.Huyu mgeni wetu ametutembelea kama Rais wa Benin au Mwenyekiti wa AU.Maana nadra sana kuwaona marais wa nchi za kifaransa(Francophone) wakitembelea wenzao wa nchi za kiingereza(Anglophone)-Wazungu watawala wetu walitulisha sumu mbaya sana.Hawa wenzetu wa Francophone ambao wengi wako Afrika ya Magharibi ni kama wamejitenga,wana sarafu yao(CFA/XOF Francs) ambayo mfaransa anaitawala kwa remote,ninavyoandika hivi dola 1=CFA Francs 497-500.Kwenye karatasi(on paper),pesa yao inaonekana ina nguvu kuliko Shilingi ya Tanzania,kwenye domestic purchasing power(ununuzi wa la ndani),pesa yetu ya kibongo ina nguvu sana.(Hilo niwaachie wachumi).Sisi Tanzania ni Maskini Jeuri,kimaendeleo tumeziacha mbali sana hizi nchi nyingi za kifaransa(kwa kuangalia!).Tukijipanga,tuna uwezo mkubwa wa kupeleka na kuuza bidhaa zetu wenyewe kwenye vinchi hivi kama tunavyofanya vizuri kwenye soko la Congo DR.Ziara ya huyu bwana mkubwa ni muhimu sana ifungue Fursa kwa Watanzania kuwekeza/kufanya biashara Benin.

    David V

    ReplyDelete
  2. Namwona Bw. Ali Mwadini, big up sanaaaa

    ReplyDelete
  3. Karibu Rais wa Benin na Mwenyekiti wa AU.Tanzania! David V. tatizo la uchumi na umaskini kina changamoto kila nchi kwenye bara la Afrika siyo Tanzania pekea yake.WaTanzania siyo wajeuri,wanafahamu haki zao.Wana fahamu maendeleo ya utapele hata kama kuna changamoto kwenye serikali siyo maendeleo ya ukweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...