Na. Lemmy Hipolite-Mo Blog.
Kofia ngumu za kusaidia kuokoa kichwa dhidi ya majanga mbalimbali iwe ni katika maeneo ya ujenzi au katika vyombo vya usafiri ni muhimu sana kwetu tunapokuwa katika mazingira hayo.
Tunaishukuru serikali kwa kutumia idara zake husika kuhimiza matumizi ya kofia hizi hasa kwa madereva wa usafiri wa pikipiki maarufu kama Bodaboda.
Kama inavyojulikana mtu ni afya na pia tunafahamu kuna baadhi ya magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya kugusana, kutumia kitu kimoja watu wawili au zaidi na mengine kwa njia ya maji, hewa, mbu, kujamiiana na kadhalika.
Hapa kwenye hili la kofia ngumu bado hainiingii akilini vizuri jinsi gani twaweza kukwepa magonjwa ya ngozi na mba japo sio lazima tuyapate wala hatuyaombei ila tunaangalia uhalisia wa matumizi ya kofia hizi.
Ndugu zangu wataalamu wa magonjwa ya ngozi na tiba hili likoje katika uhalisia wake? Sichokonoi ila naomba kufahamu tu kwamba tuwe tunazifua? Au hakuna neno? Mzingatie pia je zitakauka?.
Wadau sijasema msivae helmet la hasha nimeulizia tu ili woote tupate fahamu.
Karibu uchangie maoni yako kwa kubofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Kabla hujaoa,au hujaolewa wakati bado ukicheza "nje cup" ulikuwa unavaa "soksi" kabala ya mechi, au ulikuwa una"take chance" na kusononeka kesho yake? je ulipima ukimwi kabla ya ndoa? (kama ni mwana-ndoa).Maisha ni ku- take risks, mtu unaangalia kama kitu kina "tija" au "hakilipi", kama "hakina nyimbo" basi unaachana nacho. Sasa wewe chagua kati ya GONJWA LA NGOZI,KIFO,KULEMAA MIGUU/MIGUU NA MIKONO-PARAPLEGIA/TETRAPLEGIA NK.

    Au ndo nyie mnaoenda "Commando" wakati wa joto kali kwa kuogopa "Tine Cruris" aka "jock itch",
    ENOUGH SAID!

    ReplyDelete
  2. Helmet ni kitu personal yaani kitu cha binafsi sio cha kuchangia.
    Ukinunua pikipiki unapewa helmet ya bure ama unanunua.
    Kwa matumizi ya nyumbani yaani sio ya biashara utakuta mara nyingi mtu anakuwa na ya ziada kwa ajili ya ama mke au vinginevyo.

    Pikipiki sina hakika kama imepasishwa kubeba abiria aliyelipa ama kwa maneno mengine kufanyia biashara ya kupakia abiria.

    KWA KUWA NDIO TUMEKUBALI KWENDA KIENYEJIENYEJI KI STONE AGE STONE AGE, INABIDI KUKOMAA HIVYOHIVYO MAANA SIONI MHUSIKA KUFUA HIYO HELMET MAANA NI KWELI ZINA HARUFU MBAYA SANA. AU KUZI 'DRY CLEAN'.

    KUHUSU PUBLIC TRANSPORT BADO TUKO MBALI.

    ReplyDelete
  3. USIBOFYE "HAPO" KUNA JINI!

    ReplyDelete
  4. Inawezekana. Ukienda Kigali kila dereva wa bodaboda ana plastic bag maalum anakupa unavaa ndipo unavaa helmet. Ukishuka unatafuta pipa la taka unaitupa. Hili halina visingizio. Ni,muhimu.

    ReplyDelete
  5. helmet ni ya mtu mmoja sasa hapo mnapoanza kuchngia ndio kimeo.

    ReplyDelete
  6. kuna head gear flani km kwenye fomula one wanavaa kabla ya helmet ni ya kitambaa inavutika inafunika kichwa chote kasoro macho na mdomo ziko za bei rahisi pia acheni kukuza mambo!

    ReplyDelete
  7. Ni ukweli usiopingikana juu ya uwezekano wa kusambaza aina fulani ya magonjwa kwa kushirikiana kuvaa kofia iwe ya iana yoyoyte au hata hiyo ya helmet,Taulo,shuka au hata nguo tu za kawaida,kugusana iwe kwa aina yoyote ile.Haya yote yanawezekana iwapo mgonjwa ameacha vimelea vya ugonjwa na mwengine akavichukua kwa njia ya kugusa sehemu husika. Kwa kulitambua hilo baadhi ya wadau wa afya huwa wanatushauri kutokuchangia vitu kama taulo,mashuka na hata nguo.Vilevile huwa wanatushauri kunawa mikono au kuoga kwa sabuni mara kwa mara ili kuepuka uwezekano wa kupata maradhi yanayosambaa kwa njia ya mgusano.Kuhusiana na kofia za helmet na hasa zinazotumiwa na hao watoa huduma ya usafiri wa pikipiki kwa wateja wao ni changamoto kubwa hasa kwakua pikipiki si chombo halisi kukitumia kama chombo cha kutoa huduma ya usafiri wa umma kama ambavyo inafanyika nyumbani ukweli ni kwamba ni chombo kinachoweza tumika binafsi. Kuna tofauti kubwa kukitumia chombo hiki binafsi ukilinganisha na utumiaji wake kwa umma.Wakati mwengine matatizo yakikuzidi waweza ruhusu kitu baadae ukajutia na hata kujishangaa ni vp uliruhusu.Hili la kuchangia helmet na athari zake si geni kwa wadau wa afya labda nadhani ugumu wa usafiri umetufumba macho na mdomo.

    ReplyDelete
  8. Mdau kama unajua ni mtumiaji wa kofia ngumu aidha kwenye maeneo ya ujenzi au vyombo vya usafiri ni bora kujali pia afya yako. Nunua mfuko wa plastik maarufu kama marlboro vaa kichwani fuatia na kofia ngumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...