Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akiongoza mapokezi ya ujumbe wa Sekretarieti ya CCM,unaoelekea mkoani Kigoma mapema asubuhi hii kwa usafiri wa treni,ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana (wa pili kulia) kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM yatakayo adhimishwa mkoani humo.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza na Wanachama wa CCM mkoani Dodoma waliokuwa wamefika Stesheni ya Dodoma asubuhi hii kuwalaki Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM,Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC wameondoka jana jijini Dar kwenda Mkoani Kigoma kuadhimisha miaka 36 ya Chama hicho.Kushoto kwake ni Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na kulia kwake ni Katibu wa NEC,Itikaji na Uenezi CCM,Nape Nnauye 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiagana na baadhi ya WanaCCM wa Mkoani Dodoma waliofika kuwalaki na kuwatakia safari njema Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM,Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC wameondoka jana jijini Dar kwenda Mkoani Kigoma kuadhimisha miaka 36 ya Chama hicho.

 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiwaaga Wanachama wa CCM mkoani Dodoma waliokuwa wamefika Stesheni ya Dodoma asubuhi hii kuwalaki Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM
Katibu wa NEC,Itikaji na Uenezi CCM,Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika stesheni ya treni Mkoani Dodoma Mapema leo asubuhi.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro  akiwa ndani ya treni asubuhi hii akiwapungia mkono WanaCCM wa Mkoani Dodoma waliofika kuwalaki na kuwatakia safari njema Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. CCM-Ubunifu huu binafsi nimeufurahia.Hata hivyo,wengi mnakumbushia enzi zenu za kusafiri kwa 'WARRANTY'.

    David V

    ReplyDelete
  2. kumbe inawezekana kufika dodoma hata kwa treni..kwa nini hata wabunge wetu wanauzunguka maeneo inayopita treni hii wasiitumie ili tubane na matumizi kidogo??.

    ReplyDelete
  3. UBUNIFU GANI HAPO TENA SI USAFIRI TU WA KITANZANIA TENA NDO UNAOTUFAA WOTE. AU ULITAKAJE SASA NAONA HATA WAO YANI UTADHANI WANAKWENDA VITANI KILA SEHEMU WANATAKA KUJULIKANA WAMEPITA.NYE WAJEMANI! KHEE!

    ReplyDelete
  4. CCM Juuuuuuuuuuuu x Bilioni zote !

    Wajameni kama itatokea Wakubwa wa Chadema Wakasafiri kwa Treni mfano KATIBU MKUU na MWENYEKITI wa Chama hicho chenye fujo,

    Mimi Mdau wa CCM na YANGA damu Sele Chinga nitakunya Sokoni Kariakoo Mjini Darisalamu mchana kweupe siku hiyo!

    Nipigieni simu niwahakikishieni

    Simu yangu ni 0754-946060

    ReplyDelete
  5. Chadema mnaweza hiyo?

    Mkishika nchi (KAMA MNAVYOOTA) tutegemee mabadiliko yafuatayo badala ya kutegemea labda Vingozi wenu wa juu wanaweza kupanda Treni:

    MABADILIKO:

    1.WIZARA ZOTE NYETI KUHAMISHIWA MOSHI-KILIMANJARO

    MFANO,

    (I)WIZARA YA FEDHA
    (II) WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
    (III)WIZARA YA ELIMU NA TEKNOLOJIA
    (IV)WIZARA YA UTUMISHI WA UMMA
    (V) BENKI KUU

    Dar Es Salaam MTAACHA WIZARA KAMA ZA UTAMADUNI NA MICHEZO na MAENDELEO YA JINSIA NA WATOTO!!!

    ReplyDelete
  6. Ohooo!

    Ikitokea Chadema mkafanya kitu kama hiki cha Wakubwa wa Chama chenu kupanda Tereni, mimi naahidi ''Kujamba kwa mshindo mkubwa'' hadharani hapo hapo Kituo Kiuu cha Treni Stesheni mbele za watu!

    Iwe kuachia upepo huko ni kama dalili ya mshangao kwa tukio hilo adimu kabisa ndani ya Chadema!

    ReplyDelete
  7. CCCMMMM juuuuuu zaidi !

    Chadema mkifanya hivyo 'mimi naahidi kuumeza ulimi wangu' mpaka tumboni!

    ReplyDelete
  8. Chama chochote cha Upinzani hasa CHDM mkithubutu kufanya kama hivi walivyofanya Viongozi wa juu wa CCM, MIMI NITAMMEZA MJUSI AU NYOKA aliyekuwa hai!

    ReplyDelete
  9. Wapinzani mnaona hiyo?

    Hasa hasa kile chama chenye fujo Wakubwa wake wakifanya kitu kama hiki, mimi nitatembea kwa mikono miguu ikiwa juu kutoka Dar Es Salaam hadi Morogoro!!!

    ReplyDelete
  10. Hawa ndio aina ya Viongozi tunaowataka katika Tanzania yetu!

    Tunataka viongozi tunaoweza kuchanganyika nao kwenye maisha yetu ya kawaida kama kwenye mikusanyiko mfano Waheshimiwa walipokuwa wanaagwa Dar na wakati wanasalimiana na Wananchi walipofika Dodoma.

    Tunataka Viongozi kama hawa wanaosafiri kwa usafiri wa kawaida tunaotumia sisi ili waone viwango vya usafiri na hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ipo vipi.

    NI UTENDAJI MZURI KAMA KIONGOZI UTAANDAA AINA YA USAFIRI HALAFU WEWE MWENYEWE UKAUTUMIA USAFIRI HUO KWA MAJARIBIO, MFANO MHE. DR.HARRISON MWAKYEMBE ALIPOWEKA SAWA USAFIRI WA TRENI AKAPANDA KWA SAFARI YA MAJARIBIO.

    SIO KIONGOZI ANAANDAA USAIFIR WA TRENI HALAFU YEYE ANAONA KINYAA HATA ILE KUUJARIBU KWA KUPANDA SAFARI FUPI TU!

    Mhe.Abdulrahman Kinana ni mtu Mkubwa sana hapa nchini, angekuwa mtu wa kujikweza asingekubali kupanda Treni !

    Mhe.Dr. Asha-Rose Migiro ndio karibuni ametokea UMOJA WA MATAIFA, huko Marekani akiwa na Madara makubwa kabisa Duniani kama nagekuwa wa kujikweza kwa daraja alilofikia asingekubali kupanda Treni!

    Mhe.Nape Nnauye ni mtu Mkubwa katika Chama asingekubali pia kujishusha kupanda Treni!

    Lakini kwa kuwa wote hawa ni Viongozi wa kweli hawakuona ajabu kutumia usafiri huo kuwafikia wananchi!

    Sio wale Mabwenyenye wanaosafiri kwa VX-V8 na Ndege tena Daraja la kwanza!

    Sio wale wanaosomesha watoto wao St.Marys na Majuu wakati hapa hapa wanapo ongoza zipo Shule!

    ReplyDelete
  11. Mpishi mzuri ni yule aonjae mapishi!

    Viongozi kutumia Usafiri huu wa Treni ni dalili nzuri ya kuwa viwango vitaimarika zaidi kwa kuwa Wakubwa wameona kwa vitendo!

    ReplyDelete
  12. Lindi na Mtwara watakwenda lini?

    ReplyDelete
  13. jamani usalama kwanza acheni kutoa vichwa nje mnaweza kukatwa...ni hatari!

    ReplyDelete
  14. Rose Mingiro is the next President of Tanzania.

    ReplyDelete

  15. hahaha jamani hyo train ina nikumbusha safari ya kutoka singapura kwenda bangokok thailand kuna tmu aliniambia tume panda train ya wafu lakini hyo nayo iona hapo ni zaidi ya train ya wafu hahahahha nitaipanda siku moja

    ReplyDelete
  16. Kwani cha ajabu hapo ni nini? Hawa si binadamu ti wa kawaida? Mbona ulaya wakati mwingine hata Rais ama waziri mkuu anatumia usafiri wa umma?

    Hawa wanaigiza 'show case'. Wanatafuta kura na zaidi wanawachelewesha abiria safari, wao wameshiba ndio maana hawana hata haraka ya safari wakatu=i kuna abiria wafanya biashara na watoto wa shule na wengine ni wagonjwa wanataka kuwahi, sasa wanacheleweshwa na wasanii wa kisiasa.

    Kwani CHADEMA ama CUF ina uhusiano gani na kupanda treni? Usafiri kila mtu anapanda kulingana na kipato chake, 'it is a private matter' Kama CHADEMA wana pesa ya kupanda ndege wapande, hii siyo ishu. Cha muhimu ni sera za chama zenye kuleta maisha bora.

    Acheni ushamba wa kushabikia watu waliotufanya kuwa masikini wa mwisho duniani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...