Kaka issa
Heri ya Mwaka mpya 2013, Naomba kuwakilisha maoni yangu kuhusu hili la wizi wa fedha kwa kutimia mtandao
Kwa muda sasa wa wiki nzima, tumekuwa tukisoma kwenye vombo vya habari wizi wa fedha kwa mtandao au kwa kutumia kadi zinazotolewa na Bank, za ATM Card, Mastercard ama Visa. Kusema ukweli hili suala sijui kama benki za Kitanzania zinaichukua kwa umuhimu uliyonao, ni Hatari kuliko wanavyoichukulia.
Ukweli ni kwamba Benki pekee haziwezi kuhimili mapambano ya Cybercrime, kama kweli tunaelewa na kutambua kwa undani ukubwa wa hili tatizo. Mfano, katikati ya Mwaka 2012, Banki zote Marekani ziliwekwa kwenye ‘high alert’ na vyombo vya usalama kuwa kuna wahalifu wa kimtandao ambao walikuwa wakitaka kuiba fedha kwenye account za wateja wao. Kazi hiyo ilifanywa kwanza na FBI kuitercept uhalifu huo, kabla benki kuchukua hatua.
Hivi ni vita ambavyo vinapiganwa na vyombo vya usalama vya nchi. Cybercrime ni kubwa kuliko mabenki wanavyoifikiria, mwaka jana peke yake, wahalifu wa kimtandao walijaribu kuiba Paundi 2.5 Billion kutoka mabenki mbalimbali Ulaya peke yake achilia nchi zingine kama Asia na America. Ni vita ambavyo Tanzania peke yake hawawezi kuvipigania. Wakati Viongozi wetu wakifanya vikao vya kutaka kuwa kuwadhibit M23, hiyo kazi waichie drones za Obama, na waanze kupambana na Cybercrime ambayo miaka 20 ijayo itatufanya turudi kwenye ukoloni kwasababu tutakuwa tukiwategemea wazungu kutusaidia katika hivo vita.
Elimu ya usalama wa fedha za wateja unahitajika sana tena sana miongoni mwa wafanya kazi wa benki zetu. Usalama wa Banking System pia benki wanatakiwa kuangalia. Mfano, haiwezekani computer ya banki ambayo mfanyakazi wa benki hutumia kuangalia account za wateja, na akimaliza anaingi facebook kuchat. Mara nyingi mtu unaweza kuforwadiwa email ilikwisha pelekwa kwa zaidi ya watu Elfu na ukiangalia imetoka wapi usishangae ukaona john.idd@benkifulani.com.  Huwezi kuingia kwenye website yoyote kwa kutumia mtandao wa Benki. 
Kuna websites ambazo kazi zake ni kuwapatia hawa wahalifu taarifa zote za kila computer itakayoingia kwenye hiyo website. Benki zetu waache ubahiri waanze kuinvest kwenye security technology, na lazima wawe na cyberwatch team masaa 24 siku saba kwa wiki. 
Mambo mengine ni uzembe wa mawazo na kwasababu ajira ni kwa kujuana inakuwa ngumu sana kudhibiti matatizo kwenye mabenki zetu kwasababu hatujui wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye maeneo nyeti kama haya wana uaminifu kiasi gani kwa pesa za wateja wao. Na inawekana hatuna huduma ya 'security clearance' kwenye kazi yenye kuhitaji uaminifu wa kiwango hiki.
Naomba kuwakilisha kaka.
Mdau US

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mdau kutoka US, tunashukuru kwa mada yako na tahadhali yako ila siku zote mambo huwa ni nyumbani siyo ughaibuni. Wewe kama mdau tena uliye nje umeshachukua hatua gani katika kutusaidia kwenye hilo?, pia nadhani kwa kuwa uko nje huwezi kujua kinachoendelea huku nyumbani. Nadhani Tanzania tayari imeshajiweka sawa katika nyanja hiyo ya cybercrime na tunapambana vyema kabisa. Kuna Watanzania zaidi ya 100 ambao ni wajuvi wa mambo hayo ya 'uhalifu wa kimtandao" na sasa hivi just to let you know kuna kitengo maalumu "task force" inayokabiliana na mtandao huo hivyo shaka ondoa. Tanzania tuko njema na hakuna cha kutubabaisha katika kitengo hicho. Tanzania ni njema na atakaye na aje ila ajue tumejipanga na tuko sawa ukituchezea kimtandao tunakufuata hadi chumbani. JK amepanga vijana wake vizuri.
    Mdau
    Cybercrime Expert
    Tanzania

    ReplyDelete
  2. Hili ni jambo nyeti sana,

    Mzaha mzaha hutumbua usaha, tunaweza kukuta kasi ya umasikini inaongezeka badala ya kupungua kama suala hili lisipopewa kipaumbele hapa nchini.

    Mfano kwa hali halisi hapa kwetu kwa sasa hatuna Bima ya Fedha, ikitokea yakimfika mfano mtu aliyeweka Akiba yake ya mwisho ya Mafao ya Kustaafu halafu ikaibiwa.

    Je, ikizingatiwa hatuna Bima za fedha halafu mtu huyo Mstaafu akiibiwa Benki hajazama kwenye Umasikini hadi kifo?

    ReplyDelete
  3. Nipo pamoja na mdau wa US kwa mada yake nzuri. Serikali yetu inabidi ibadilike nakuweka mkazo ktk usalama wa mitandao kwani nivigumu sana raia wa kawaida kabisa kujua anaibiwa au la.
    Tuache mambo ya kuwekana kwenye kazi na tuangalie elimu na ufanisi wa mtu, hapo tutashinda kama huko ulaya na kweingineko.

    Mdau tz.

    ReplyDelete
  4. Naungana na mdau kwa kuonyesha uzalendo kwa nchi hasa katika jambo hili ambalo ni zaidi ya hatari.
    Nasikitishwa na mwenendo mzima wa ajira hapa nchini kwetu ambao umejaa upendeleo na kujuana na hatimae kuajiri watu wasio na sifa na wala maadili.
    Serikali inajaribu sana kupambana na magaidi wa kimtandao japo inashindwa kuwapa elimu wananchi juu ya kutunza kumbukumbu zao na jinsi ya kujihadhari na social networks na pia jinsi gani kuna umuhimu wa kubadili passwords mara kwa mara na mambo kama hayo.
    Nimeona ktk mabenki mengi jinsi ambavyo usalama ulivyo duni kwa kuna wakati niliwahi kuomba picha za mtu aliefanya ku withdraw ktk account yangu basi zile picha hazikuweza kuonekana sawia na wala hazikuwa na msaada.Naunga mkono hoja juu ya kuimarisha na kuboresha usalama wa mabenki,barabara,viwanja mbalimbali n.k kwani mitutu pekee haitoshi ni vyema nchi yetu na sisi sasa tuamke na kujilinda.

    ReplyDelete


  5. Mdau asante lakini that imply s abroad much compared to Tanzania
    kwanza benk za Tanzania zenyewe hazina huduma ya kuridhisha kabisaa hawatujali sana sisi diaspora wanaweka namba za simu ukipotelewa kadi upige simu lakini hizo number hazipokelewi kabisaa

    Ya kwanza ni (EXIM Bank Tanzania) nilipoteza wallet kwenye Transit lakini nikawapigia EXIM simu zoote hata zilizopo kwenye website yao hazipokelewi sasa what do u expect hapo kama namba za simu feki ndo unatarajia wataweza cyber crime??
    mara nyingne tena walikata hela kwenye account lakini hazikutoka kwenye ATM nilipo rudi tz kuwadai wakasema 2 years past hawana records kama si ujinga na wizi,,,,

    ReplyDelete
  6. Aina hii mpya ya wizi,

    Sasa ni kupandishana viwango vya visukari na mashinikizo ya damu!

    Huu wizi wetu wa kawaida unamkamata Mwizi unamfikisha Polisi zetu hizi za Posti na za Mabatini, ile unarudi nyumbani unamkuta Mwizi wako tayari zamaaani yupo Maskani kwake amesharudi na amekaa mustarehe!

    Mtu unasikia Akiba yako ya kudunduliza imekombwa, si ndio Kupooza viungo vya mwili kwenyewe tena kunakuja?

    ReplyDelete
  7. mambo hayo changamoto kwa wakubwa wafanyie kazi suala hili mapema.

    ReplyDelete
  8. Mdau wa US umeandika hoja muhimu sana,tatizo zile idara muhimu/nyeti za kuweza kupambana na wizi huu ziko BIZE na wanasiasa,inasikitisha.Na hii online fraud inaweza kuvuruga mfumo wote wa Uchumi.Nakubaliana na wewe,mabenki peke yake hayawezi kupambana na huu mtandao

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...