Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mawaziri, wabunge na maofisa waandamizi wa wizara na wakala wa ujenzi (TANRODS) pamoja na viongozi wa bodi ya wakandarasi akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa daraja hilo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakipozi na umoja wa wakandarasi wazalendo kutoka makampuni mbalimbali waliopewa kandarasi ya kujenga daraja hilo. PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ni makosa makubwa kwa serikali kuanza kuyapa majina ya viongozi madaraja na maeneo muhimu kabla hao viongozi hawajatoka madarakani. Kawaida majina yanatolewa baada ya mtu kuachia madaraka kwa sababu mbalimbali ikiwa na ku-avoid influence ya huyo mtu katika kujipa jina, na kutokujua kuwa huyo mtu atatoka madarakani akiwa na heshima ya aina gani? Je, kama Rais akipata kesi kubwa ya kumchafua na akakutwa ana hatia mtabadili majina ya hayo madaraja? Sina ubaya wowote na Mh. Dr. Kikwete lakini kwa mawazo yangu haya majina yanatakiwa yasubiri watu wakishang'atuka ndo uongozi wa awamu inayofuata unaamua kuwa kutokana na mchango wa kiongozi fulani barabara au jengo fulani liitwe kwa jina lake. Huo ndo ustaarabu wa dunia nzima. Mdau, CA-USA

    ReplyDelete
  2. Mdau kajipange maelezo mareefu wewe ndie unaetaka kumchafua

    ReplyDelete
  3. Basi tafuteni daraja / barabara moja liitwe Magufuli kwani anawajibika kweli kweli

    ReplyDelete
  4. Madaraja ni nyenzo muhimu sana katika tasnia ya uchukuzi wa nchi kavu nami naipongeza serikali katika uwekezaji huo.Ili kuthibitisha umuhimu wa madaraja sisi wakazi wa Kitunda,Mwanagati na Magole tunalazimika kwenda na kutoka katikati Jiji kwa kutumia barabara ya Nyerere pekee yake kutokana na ukosefu wa madaraja ambayo yangetuwezesha kupitia Mbagala au Tandika na kupunguza msongamano katika barabara ya Nyerere.

    ReplyDelete
  5. Wewe Annoy Wed Jan 09, 07:42:00 AM 2013 unadhani usipokosoa makosa utapewa cheo? Ninyi ndo mnarudisha maendeleo nyuma kwavile mnadhani kuwa mkijipendekeza mnaisaida nchi kila maoni mnayotoa ni ya kusifia...!! Kijana msemakweli, Dodoma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...