Wakati Mahabusu wakikosa haki ya kupelekwa mahakamani wilayani Ruangwa kwa kukosekana Mafuta ya gari la kuwachukua Magereza Nachingwea,Cha ajabu ni kwamba Mafuta ya kwenda umbali kama huo wa Nachingwea yapo kwa kwenda Kuvizia magari na pikipiki ili kujipatia ulaji yapo au mafuta yanapatikana hapo walipotega? Inatokea wakati mwingine Mfungwa akahukumiwa Ruangwa akakaa mahabusu ya Polisi Ruangwa kwa takriban siku tatu kabla ya kupelekwa Magereza.Wizara na Jeshi la Polisi Makao Makuu Tupieni macho Polisi Ruangwa na suala la Mafuta wakati mwingine ushindwa kuwahi tukio kwa sababu ya eti Magari yao hayana Mafuta.Ruangwa ina matukio mengi ya kujichukulia sheria Mikonini ikiwamo mauaji na ujambazi.Picha na Mdau Abdulaziz,Lindi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. hapa nampongeza sana Camera Man kweli amewanasa wenyewe wakiwa pumbazoni kwa mshiko!matukio kama hayo yapo sehemu nyingi sana hapa nchini!Dawa yake nini hasa,kutafutana?Au kila mmoja kuwajibika kikamilifu sehemu yake ya kazi?Hivi kweli,hapa duniani "kuna mshahara utakaotosha mahitaji ya mtu?".Ukweli ni kwamba,"hakuna!".Lakini,lazima pawepo na "Bottom Line","Kiwango au Kima cha chini cha mshahara wenye thamani ya Utu ndani yake",mshahara utakaotosheleza mahitaji ya msingi kabisa katika familia,japo kwa wiki tatu mfululizo katika mwezi wenye wiki nne!Unatakiwa utoshe mahitaji ya mwezi mzima.Lakini,kwasababu tunajua hilo halitawezekana,basi tuanzie na mahesabu ya wiki tatu katika mwezi.Na wafanyakazi waanze kulipwa Katikati ya mwezi(nusu mshahara),na mwisho wa mwezi(nusu ya pili ya mshahara), hiyo kidogo itapunguza Ukata kwa wafanyakazi,japo pesa haito tosha.Pili,somo la maadili kazini lifanyike kila siku asubuhi mahala pa kazi,kuwakumbusha wafanyakazi wajibu wao kwa umma,madhara ya kupokea rushwa na adhabu zake mtu akikamatwa anapokea au kudai rushwa,na kuipenda kazi yako inayo kuwezesha kukupatia kipato ukawa mtu miongoni mwa watu!binadamu wana vichwa vigumu sana,hilo tukumbuke!tusikate tamaa katika kupambana na mdudu Rushwa na Ufisadi!Raia mnaposhuhudia vitendo kama hivyo vikifanyika,chukua namba ya gari,andika eneo la tukio,chukua idadi ya askari waliopo katika eneo la tukio,na ukibahatika kunasa namba ya askari chukua;kisha taarifa hiyo itume kwa sms kwa Kamanda wa Polisi Mkoa au Wilaya,haraka iwezekanavyo!

    ReplyDelete
  2. Hapo wameambiwa kila wiki wapeleke mgao kwa RTO na RPC,ndio mwendo mdundo kwa nchi zinazoendeshwa ki rushwa rushwa,uozo wa rushwa huanzia juu.

    ReplyDelete
  3. Wangekuwa wapo hapo kwa nia njema ya usalama wa wananchi, ingependeza na kupongezwa.

    ReplyDelete
  4. Utasikia Bosi wao Makao Makuu Darislama atawatetea !

    Ngoja uone taarifa na picha hizi zikizagaa.

    ReplyDelete
  5. Daaa !

    Sio bure hapa 'Mamba' ametega atakaye yakanyaga amemezwa mzima mzima!

    ReplyDelete
  6. watanzania sijui ni lini tutaelimika jamani, sasa sijui mnataka wafanye kazi zao vipi.wakikaa ofisini wasiende huko kuangalia usalama mtasema hawana kazi wanakaa ofisini tu, wakienda huko kuangalia usalama wenu oooh wanatega. sijui wafanyeje jamani. wanaofanya kazi zao vizuri siku zote ndio huwa wanaonekana hawafanyi. MIMI SIKUBALIANI NA HOJA YAKO HII ULIYOIPOST HAPA BWANA MICHUZI.ANGALIA HABARI ZA KUTUWEKEA SIO ZA KUKATISHA WACHAPA KAZI TAMAA...watu hawaachi kusema hata ufanyeje

    ReplyDelete
  7. Hivi inaposemwa mshahara mdogo hautoshi ni kwa hawa jamaaa tu? mbona na akina siye tunabanwa hivyohivyo Je nasiye tutege vipi!?
    Hapo ndipo unaskia bandari wamelamba mamilioni.... Na huko na huko mwendo ni huohuo.... Ila Jamaa hawa wamezidi na siku hizi ni mchana kweupeeee!

    ReplyDelete
  8. Hamuishi kusema ovyo, nani ana ushahidi wa rushwa hapo? Mie naona watu tu wapo kazini. Usalama barabarani pia ni muhimu. Acheni utamaduni wa kulalama ovyo, peleka ushahidi wenye mashiko polisi au mahakamani.

    ReplyDelete
  9. wewe mdau wa Fri Jan 18, 07:45:00 pm 2013, nadhani hauwajui, au hayajakukuta, yatakapokukuta utakuja hapa kutuambia, kama wewe ni muungwana. Labda tuseme si wote wanaofanya hivyo, ila asilimia kubwa ndio lengo lao. Na hili linajulikana na halina ubishi. Watanzania uzalendo umekwisha imebaki kila mtu kujitafutia kwa nafasi yake kwa namna yoyote. Inasikitisha sana!

    ReplyDelete
  10. Anon jan 18 08;32;00pm
    Nahisi wewe ni polisi la unashirikiana nao katika uhalifu,au ndugu yako atakua ni polisi mkubwa hivyo unanufaika na hayo mazingira somehw.
    Tanzania hii ya leo,who are you to fool people eti polisi wako hapo kufanya kazi yao yaani nina hasira na wewe japo sikujui.
    UNAWAJUA POLISI WA TZ WEWE KWELI?Watu wanaokukamata na kosa jingine wakuombe rushwa ukatae wakubambikie kesi! WHAT R U TRYING TO TELL? WANAMLINDA NANI HAPO NA WANALINDA NINI ILHALI BASI LITAPITA LIMEJAA KUPITA KIASI NA HALINA BREKI SAWASAWA NA WAKIPEWA PESA WATALIACHA LIENDE.HEBU TUJARIBU KUWA WAKWELI POLISI WETU WAMEKOSA UTU NA DAMU NA VILIO VYA WATU WANAOWADHULUMU AIDHA KWA KUTOWAJIBIKA KWAO AU KWA KUWAONEA HAVITAENDA BURE NA VITAWAFWATENI MPAKA VIZAZI VYENU VYA NNE.ENDELEENI KUTETEA UPUUZI WENU,NANI ASIYEWAJUA NYINYI!

    ReplyDelete
  11. NDUGU ZETU TUACHE JAZBA KUNA USHAHIDI GANI KUWA POLISI HAO WAKO HAPO KUTEGEA RUSHWA NA SIO KUFANYA KAZI? PIA INABIDI MFAHAMU KUWA POLISI WETU WANAFANYA KAZI KTK MAZINGIRA MAGUMU NA UHABA WA VITENDEA KAZI, UTAKUTA MAHITAJI HALISI YA MAGARI KWA WILAYA NZIMA NI MAGARI KUMI LAKINI MNAPATIWA MAWILI KATIKA MAZINGIRA KAMA HAYA NI LAZIMA KUNA PRORITY, HIVI KWELI KUMUWAHISHA MFUNGWA KWENDA KUANZA KUTUMIKIA KIFUNGO NI DHARURA? PIA TUKUMBUKE SUALA LA KUHUDUMIA MAHABUSI SI LA POLISI NI LA IDARA YA MAGEREZA.

    ReplyDelete
  12. Mdau wa Sita anony wa Fri Jan 18, 08:32:00 pm 2013
    ===================================
    watanzania sijui ni lini tutaelimika jamani, sasa sijui mnataka wafanye kazi zao vipi.wakikaa ofisini wasiende huko kuangalia usalama mtasema hawana kazi wanakaa ofisini tu, wakienda huko kuangalia usalama wenu oooh wanatega. sijui wafanyeje jamani. wanaofanya kazi zao vizuri siku zote ndio huwa wanaonekana hawafanyi. MIMI SIKUBALIANI NA HOJA YAKO HII ULIYOIPOST HAPA BWANA MICHUZI.ANGALIA HABARI ZA KUTUWEKEA SIO ZA KUKATISHA WACHAPA KAZI TAMAA...watu hawaachi kusema hata ufanyeje

    ===================================
    MKAO WA ULAJI RUSHWA NA UCHAPAJI KAZI HAVIFANANI!!!
    ===================================

    Hiyo gari ni PATROL na siyo gari ya kutegea sehemu moja tu!

    Inatakiwa iwe inatembea sehemu tofauti ili kufanya kazi!

    Jamaa wamepewa mafuta wafanye kazi kwa ku patrol kwa kuwa majukumu yapo sehemu tofauti KWA MAANA UHALIFU HAUFANYIKI HAPO NJIA PANDA PEKE YAKE , jukumu ni kuzunguka na sio kutega sehemu moja!

    HUO SIO UCHAPAJI KAZI BALI NI UTEGAJI, KWA MAANA NI KUWA HAPO WALIPOSIMAMISHA GARI NDIO PENYE MFEREJI WA MAPATO!

    ReplyDelete
  13. Mdau wa Sita hapo juu:
    ...................................

    ...MIMI SIKUBALIANI NA HOJA YAKO HII ULIYOIPOST HAPA BWANA MICHUZI.ANGALIA HABARI ZA KUTUWEKEA SIO ZA KUKATISHA WACHAPA KAZI TAMAA...watu hawaachi kusema hata ufanyeje
    ...................................

    Hao Maafande wamekaa mkao wa kula kabisa na hapo wapo kwenye mkao wa Ki-Saccos !

    Kwa nini kama huamini usiendeshe gari wewe au Pikipiki upite hapo kama hawajakurarua?

    ReplyDelete
  14. Nyie wapuuzi mnaotetea hawa jamaa kuwa wapo hapo kikazi ni watanzania kweli au? na kama ni watanzania mtakuwa hamuishi nchini ndio mana mwabwabwaja tu upuuzi hapa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...