Mtuhumiwa wa Nyara za Serekali,Peter Laurence (mwenye kofia katikati) akiwa chini ya Ulinzi wa Maofisa wa Jeshi la Polisi chini ya ulinzi ,eneo la Kisongo Mtaa wa Mateves nje kidogo ya jiji la Arusha baada ya
kukamatwa na shehena ya nyara za serikali nyumbani kwake hapo.
Miongoni mwa Nyara za Serekali zilizokuwa
zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu kwenye nyumba ya mtuhumiwa Peter
Lawrence zikionekana kwenye maboksi tayari kwa kusafirishwa nje ya
nchi.
ngozi ya mamba ambayo ilikutwa kwenye ghala la mtuhumiwa
ikiwa ni sehemu ya nyara mbali mbali zilizokutwa kwenye ghala hilo
ikiwemo meno ya tembo,vichwa vya simba,vichwa vya nyati,ngozi ya
simba,ngozi ya tembo na nyara nyingine nyingi za wanyama mbali
mbali.
Huyu jamaa kaniuzi hadi basi yani. Natamani nimzabue vibao.
ReplyDeleteIvi kweli huyu muhusika ni mtanzania halisi? yaani wakati kuna watu wanafikiri jinsi gani ya kuikwamua hii nchi, watu hawalali kwa kufikiri yaliyo mazuri kwa watanzania na tanzania kama nchi lakini wakati huohuo kuna watu wanafikiria nafsi zao kwa kutumia rasilimali za nchi ili waweze kunufaika wao pekee tu.Ni tabia mbaya ambayo ikiachwa hivi italeta maafa kwa vizazi na vizazi, chakushangaza huyu muhusika hutomsikia akitajwa wala kumuona akioneshwa kama funzo kwa wengine na hili ndilo ambalo lenye kuwafanya wazidi kuendelea kulitafuna taifa, inauma sana kuona hali hii ikiendelea.
ReplyDeleteAcheni ujinga nyie huyu jamaa hajamuibia mtu..hawa wanyama wapo maporini hamna mtu anaewatunza isitoshe hiyo serikali haisaidii raia wake kuweza kupata ajira wafanye nini?Wakati jamaa kajiajiri anaonekana mwizi je hao mawaziri wanaochota pesa kwenye hazina za serikali na hata kuuza migodi na wanyama pori waziwazima mbona hawakamatwi na kuwekwa kwenye mablog kama huyu mjasiria mali?
ReplyDeletepori ni mali ya nani kwani ukijibu hilo ndio ntakuelewa
Deletehuyu sii jangili jamani mbona polisi ni waonevu huyu anatafuta chakula cha watoto wake na kama serekali ya Tanzania itamwita jangili wale twiga waliowauza Qatar warudishwe, alafu tutaendelea.
ReplyDeleteWewe Anoy.wa 12.35am naamini umetoroka MIREMBE! au upeo wako kishule ni mbumbumbu kabisa! Hii sio issue ya kushangilia na kusifia hata kidogo labda kwa mtu PUNGUANI kama wewe!
ReplyDeleteHuyi jamaa anatakiwa anyongwe tena hadharani kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa watu kama hawa!
Mdau wa tatu (3) Anonymous wa Tue Jan 08, 12:35:00 AM 2013
ReplyDeleteMtazamo wako ni finyu sana,
Kuna kitu kisichokuwa na mwenyewe?
Kwa taarifa yako huyo mtu Jangili ametuibia sisi wote wa Tanzania pamoja na wewe mwenyewe!
Je, ukiambiwa kuwa umeibiwa wewe mwenyewe utafurahi?
Hii ni mali na rasilimali ya nchi, inatakiwa ivunwe kwa Tija na kwa matumizi yanayoinufaisha jamii nzima ya Tanzania na si kwa mtu mmoja kuweza kupata utajiri ili aweze kulewea pombe, na kuolea wanawake wengi na kuweka vimada pembeni.
Lohhh,
ReplyDeleteBinaadamu anapotafuta fedha anakuwa jasiri namna hii?
Nafikiri hawa Majangili ili kuwabadilishia ajira itafaa wapelekwe ktk Vikosi vya Majeshi Ulinzi na Usalama, wapewe mafunzo kwanza inaonyesha tutapata Majemedari Shupavu sana!!!
Mtu anakabiliana na mnyama mkali kama Mamba, Tembo, Simba, Nyati, Faru na Chatu hadi anamuuwa na kuchukua mali!
Hii fedha yote waliyopata Majangili imewekezwa wapi?
ReplyDeleteNadhani umefika wakati sasa wa kuhakiki Akiba za watu na vyanzo vyake ili kujua fedha za haramu walizovuna watu ktk wizi wa aina nyingi na mambo kama haya ya Ujangili!!!
Hebu angalienei kiwango cha Ujasiri!
ReplyDeleteT
Mtu anakabiliana na mnyama mkali kama Mamba, Chatu , Simba au Tembo hadi anafanikiwa kumuuwa na kung'oa meno ama ngozi!
Je, mtu huyo akiwa ktk Kikosi cha Jeshi si atakuwa Shupavu zaidi ya Chuck Norris ama Rambo?
Mfano akipelekwa Mashariki ya Kongo kwa Waasi nadhani atawakama kama kuku!
Mdau wa 3 anony wa Tue Jan 08, 12:35:00 AM 2013
ReplyDeleteMajangili wanaouwa na kuiba Rasilimali ya nchi na hao Mafisadi wote wanatakiwa kuwa jibishwa vikali!
Inatakiwa wakamatwe na wafikishwe kwenye Sheria na kuadhibiwa vilivyo!!!
Mdau wa 3 anony wa Tue Jan 08, 12:35:00 AM 2013
ReplyDeleteMajangili wanaouwa na kuiba Rasilimali ya nchi na hao Mafisadi wote wanatakiwa kuwa jibishwa vikali!
Inatakiwa wakamatwe na wafikishwe kwenye Sheria na kuadhibiwa vilivyo!!!
Hili tutusa la 12.35am litakuwa limetoroka MIREMBE.
ReplyDeletesheria ifanye kazi kwa watu wote wanao hujumu uchumi wa nchi hii wkiwemo viongozi na raia kama hawa. Mfano huyu jamaa amenitia uchungu sana naona anastahili kfungo cha miaka 20.
ReplyDeleteJakaya Kikwete unaona jinsi Hazina yako ya Rasilimali inavyo pokwa?
ReplyDeleteHawa jamaa wanastahili adhabu kali sana ikiwezekana Kifungo cha maisha kama adhabu ya kifo ni nje ya haki za Kibinaadamu, kama tulivyo shuhudia imefikia pabaya sana kiasi cha kusaidiwa Faru watatu (3) wa mbegu kutoka Uingereza mwaka jana kwa kuwa wale wetu wamekwisha woooote msituni hawapo kabisa!
waache waibe. kama twiga na faru wanatoroshwa nje ya nchi sembuse hivyo vitu vidogo? wananchi wamechoshwa. kama viongozi wanaiba ni bora na wao waibe kwani ni mali yetu sote watanzania
ReplyDeletemambo ya ngoso mwachie ngoso
ReplyDeleteKusema kweli,huyu akikamatwa peke yake ni uonezi.Inaonekana biashara hii kaifanya siku nyingi.Email zako,simu zake ziwe monitired na kugundua alikuwa akiwasiliana na akina nani hadi siku alipokamatwa na wote wafuatiliwe kila mumoja aliko na Pia watu wa uwanja wandege,maofisa wa uhamiaji,maofisa wa Polisi wote amabo namba zao zitakutwa kwake wahojiwe na kuchunguzwa ikiwa ni pamoja na kufuatilia records za transactions zote alizowahi kufanya nao na wao waeleze walikuwa wakiuzinana nini.
ReplyDeleteMIMI NINA UHAKIKA BILA WASIWASI-HUO NI MTANDANO MKUBWA SANA-WA KUANZIA POLISI,MAOFISA WA UHAMIAJI,TRA,WAFANYAKAZI WA UWANJA WA NDEGE,MAOFISA WA WIZARA,TANAPA,NA BAADHI YA MAOFISA WA UBALOZI WA NCHI ANAZO UZIA MZIGO HUO.Haiwezekanai ukasafirisha vitu hivyo bila document fake na bila kuhusisha watu zaidi ya kumi.
Nchi hii inadhulumiwa sababu ya uozo wa jeshi la Polisi na pia TRA.
...kama mdau aliposema hapo juu, huyo jamaa sioni kama amefanya jambo baya zaidi kuzidi hao wanaoiba mamilioni na mabilioni ya walipa kodi, maliasili nyingine za taifa kama vile migodi, wanyama tena walio hai! Bora hata huyu alijiusisha na kutafuta hiyo riziki kwa kuchapa kazi ya kuwatafuta hao wanyama kwanza, kuwakausha na hakumnyang'anya mtu yeyote tonge mdomoni. Pengine labda kakosea kidogo kwa kutokuwa na kibali cha kufanya hivyo! Na kibali hicho hatakipataje wakati yeye siyo Waziri serikalini au mla rushwa? Pengine ukute kachongewa na hao ambao walikuwa wanamtumikisha kufanya hiyo kazi ya magendo.
ReplyDeletehivi sio nchi hii siku za nyuma zilikamatwa nyara nje zikarudishwa hata hatuna habari.. ?? situliambiwa haitatokea tena?? huyo kaka alimruka mtu katika mgao wakamchongea... otherwise huo ni mtandao uliokaa kisawa sawa... hao polisi wanatu piga changa la mawe??? bado nauliza ..je ni hii hii nchi mali kama hizi zilikamatwa nje hat hatuna habari??? hivi ile kitu kinaitwa usalama wa taifa au mashushushu wako wapi???
ReplyDeleteKIUKWELI HUYU JAMAA INABIDI AKAMATWE ILA BAADAE AACHIWE HUU NIUONEVU KABISA ANAJITAFUTIA KIPATO KWANI YEYE ALICHO KIFANYA KINA TOFAUTI GANI NA WAKIFANYACHO VIONGOZI KARIBIA WOTE WA SERIKALI AU KWAVILE YEYE HAYUPO MIONGONI MWAO,,,SHERIA IWABANE WATE WATAKAO IKYUKA KWA SABABU WOTE NI WATANZANIA ,,ISIBANE WACHACHE KWASABABU HAWAPO SERIKALINI NOOOOO! HUU NI UONEVU
ReplyDeleteUhalifu ni uhalifu Fisadi ni mhalifu na Jangili ni mhalifu wote wanatakiwa kuwekwa chini ya Sheria na kuadhibiwa!
ReplyDeleteMdau wa 21 anony wa Wed Jan 09, 10:48:00 AM 2013
ReplyDeleteNinyi ndio baadae mnalalamikia Serikali
-Mnataka Huduma za Kiserikali,
-Mnataka Matibabu,
-Mnataka Vitambulihso vya Kupigia Kura,
-Mnataka Vitambulisho vya Uraia vyote mnataka bure,
-Je, una uhakika mapato atakayovuna huyo Jangili kwa mauzo ya Mali hizo za wizi za Umma atatumia kwa manufaa ya Wananchi?
-Wewe na wenzako mnafikiri Serikali itapata wapi pesa zote hizo kama sio kwa kutumia kwa Tija Rasilimali zake kama hizi ?maliasili, kwa kuzilinda na kuwavutia Watalii kutuletea DOLA $$$ hapa Tanzania ili Mamlaka iweze kuwa na fedha za kuendesha nchi?
Wewe unafikiri huyo Jangili atalipa Kodi kwa uvunaji huo wa maliasili?,,, unafikiri Serikali yako inayokupatia wewe huduma za Kiraia itapata kitu kutoka kwa huyo Jangili?
Acheni ujinga wenu kabisa hawa watu wanatakiwa waadhibiwe vikali kabisa!
Mimi nahisi kuna mtu ambaye amemchongea. Haiwezekani nyara hizo zote zisiwe na vibali.
ReplyDeleteHuu ni uonevu na ukweli lazima utapatikana.
Inapashwa upelelezi ufanywe,kwasababu nyara zina tags kutoka game department,hacheni kuropoka oviyo
ReplyDelete