Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP),Liberatus Sabas (kulia) akiongea na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP),Camirius Wambura aliyeshika madawa ya kulevya aina ya mirungi nje ya jengo la Makao Makuu ya jeshi hilo Jijini Arusha mara baada ya kukamata shehena hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP),Liberatus Sabas (wa pili kushoto) akiongea na baadhi ya Waheshimiwa Madiwani na Waandishi wa habari nje ya jengo la makao makuu ya jeshi la Polisi Jijini Arusha.
Gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T. 284 AGL ambalo lilikuwa na shehena ya mirungi viroba vipatavyo 173 vyenye jumla ya uzito wa kilogramu 1800.(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. mbona hamkamati tumbaku? au na zile nanhiii liii....!

    ReplyDelete
  2. hahaha eti polisi wanajiona wafanyakazi bora kwa kukamata mirungi ulevi usiokuwa na maana

    kamateni bange tumbaku na nyunga na pombe za kienyeji gongo a.k.a chang'aa zimejaa mitaani au sababu na wenyewe mnapiga pia

    ReplyDelete
    Replies
    1. We koma taja zote sio bange tuachieni bange yetu itubengue tafadhali sana tunataka katiba mpya iruhusu bange

      Delete
  3. hakuna sheria inayozuia mirungi kama dawa za kulevya mnapoteza muda na nguvu hapo badala mkamate majambazi...kenya wanuza mpaka supermarket...tena waziri mkuu anahamasiha ulimaji huko Meru kwakuwa yawapatia kipato.

    ReplyDelete
  4. Mirungi ni SAWA na Bangi!

    Kwa kuwa inampatia mtu hisia za Ali Nacha na akajiona kama Bilionea fulani hivi huku kiukweli akiwa hana kitu , ama akajiona kama Jemadari akiwa hata cheo cha Mgambo wa Manispaa au Kolokoloni hana!

    HIVYO MIRUNGI NA BANGI,

    Kwa nini ZISIPIGWE MARUFUKU?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...