Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (katikati) akikagua gwaride la heshima la wahitimu wa mafunzo ya awali ya udereva wa magari kozi namba 18 na udereva wa matreka kozi namba 7 katika Chuo cha Udereva na Ufundi cha jeshi hilo (KPF) kilichopo Kingolwira nje kidogo ya Mji wa  Morogoro.  
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akimpongeza Beatrice Dugange baada ya kumpa cheti na leseni ya udereva baada ya kumaliza mafunzo ya udereva chuoni hapo. Jumla ya wanafunzi 66 walipatiwa vyeti na leseni kwa kuhitimu mafunzo hayo.  
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba yake na baadaye kufunga mafunzo hayo ya awali.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkono wa Mara iliyopo chuoni hapo wakitumbuiza katika sherehe hiyo kwa kutoa michezo mbalimbali mbele ya mgeni rasmi, Kamishna Jenerali John Minja.
Baadhi ya wahitimu wakimsikiliza kwa makini, Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja wakati akitoa hotuba yake na baadaye kuyafunga mafunzo ya udereva wa magari kozi namba 18 na udereva wa matreka kozi namba 7. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...