Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Mkoani Mtwara, Askofu, Chilumba akiomba  kabla ya kuanza kwa kikao kati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na viongozi wa madhehebu ya dini  ya Kikristo mkoani Mtwara kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukmbi wa VETA mjini Mtwara Januari 18, 2013. Jana Mheshimiwa Pinda alikutana na Viongozi wa dini ya Kiislam mkoani humo.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wafanyabiashara wa Mtwara kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara, Januari 28, 2013. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  viongozi wa madhehebu  ya Kikristo kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA  mjini Mtwara, Januari 28, 2012.Jana Mheshimiwa Pinda  alikutana viongozi wa dini ya Kiislam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Mfanyabiashara wa Mtwara, Fatuma Embe akichangia katika mkutano kati ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na wafanyabiashara wa Mtwara kuhusu gesi kwenye ukubi wa VETA mjini Mtwara.
 Baadhi ya Wafanyabiashara wa Mtwara wakinyosha mikono kuomba nafasi ya kuchangia katika mazungumzo kati yao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara.
Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya  dini ya Kikristo Mkoani Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza nao kuhusu mgogoro gesi kwenye ukumbi wa VETA Mjini Mtwara, Januari  28, 2013. Jana Mheshimiwa Pinda alikutana na Viongozi wa dini ya Kiislam.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Wadau wa  PRIDE FM, Andrew Mturi na Sospeter Magumba wamezungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria kikao cha jana baina ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na viongozi wa kijamii wa Wananchi.

1·         Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini ndugu Wilman Kapenjama Ndile alitamka kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwatumia ujumbe Mawaziri wapatao 6 kuwaita ili kuungana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Emanuel Nchimbi hapo saa 3 asubuhi, ili kufanya kikao cha majumuisho ya “Yatokanayo” na mikutano ya wadau mbalimbali.

Mawaziri hao ni pamoja na Waziri wa Ujenzi (Dkt. John P. Magufuli), Waziri wa Uchukuzi (Dkt. Harrison Mwakyembe), Waziri wa Viwanda na Biashara (Abdallah Kigoda), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji, - (Dkt. Mary Nagu) na Waziri wa Elimu (Dkt. Shukuru Kawambwa).

2·         Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini ndugu Wilman Kapenjama Ndile alitamka kuwa Waandishi wa habari wamealikwa kwa ajili ya kikao cha muhstasari (briefing) wa “Yatokanayo”.

3·         Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu kwa Mkoa wa Mtwara, Sheikh Idrissa Lingondo amesema kilichosabababisha vurugu na yote ya uharibifu yaliyotokea katika kipindi hiki, ni kauli mbovu za kuudhi na kuvunja moyo kama vile kukataa kupokea maandamano ya watu na kuwaita wahaini na/au wapuuzi. Majibu kama hayo ndiyo yaliyoamsha hasira.

Akashauri kuwa watu wote (viongozi kwa wananchi) watumie diplomasia. Akatoa wito kwa Wananchi kuwa wasikivu na watulivu katika kipindi hiki ambacho mazungumzo na Viongozi wa juu wa Serikali yanaendelea.

4·         Askofu George Mussa wa Kanisa la TAG (Tanzania Assemblies of God), alisema ukimya wa viongozi na kutokukubali kuzungumz ana wananchi na kuwajibu maswali yao, ndiyo uliochochea wananchi kushikwa na hasira iliyosababisha hasara. Akahoji ni kwa nini viongozi wanakuwa kimya kusubiri mpaka maafa yanapotokea ndipo wanajongea kuzungumz  na Wananchi?

Akasisitiza kuwa siyo kwa Mtwara tu, bali nchi nzima, kwamba wananchi wamekuwa wanapuuzwa na hawasikilizwi hoja zao hasa pale wanapotaka kuwasilisha masuala yanayowazunguka. Akaonya kuwa maandiko ya Biblia yanasema Waisraeli waliopoacha kusikiliza kilio cha watu wao, Mungu aliruhusu uasi utendeke, ndipo Watawala walipoamka na kuwasikiliza.

Askofu Mussa akasema kuwa mtu yeyote ana haki, hata kama hajaenda shule, kwani hilo halimaanishi kuwa hajui kuhusu yanayomzunguka. Akasema iachwe dharau ya kudhani kuwa Watu wa Kusini hawajasoma au/wala kuelimika. 

Amehoji, ikiwa ahadi walizopewa wananchi –kujenga mitambo ya miradi, kutoa ajira n.k.– haijawekwa wazi, Je, Wananchi wataijuaje? Ni wazi kuwa watahoji.

Alipotakiwa kutoa maoni yake kwa ujumla, alionya dhidi ya matumizi ya nguvu kwa kusema kuwa mara nyingi nguvu za Watawala huzaa uasi wa Wananchi ili kukabiliana na nguvu hizo, akasema ndiyo mifano iliyotokea kwenye nchi ambazo zimejitahidi kutumia mabavu kuongoza wananchi.

Kuhusu nafasi yao kama viongozi kushirikishwa katika masuala ya kijamii, ameuliza, viongozi wanasubiri mpaka machafuko yatokee ndipo maombe viongozi wa dini wawatulize wananchi?

Mwishowe akaomba na kuwasisitiza Wananchi wawe watulivu, wasikivu, Waitii mamlaka –kama agizo la Mungu katika Biblia linavyosema– na kutokuasi kwani ni laana kwa Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Katika habari hizi, hata mheshimiwa Waziri Nkuu hawajalaani wala kutamka chochote kuhusu mali za serikali na watu ambazo ziliharibiwa. Inasikitisha sana! Hakuna mtu ambae yupo juu ya sheria, hawa watu lazima waadhibiwe. Ingekua wao wangekubali?

    ReplyDelete
  2. "waliopoacha kusikiliza kilio cha watu wao, Mungu aliruhusu uasi utendeke, ndipo Watawala walipoamka na kuwasikiliza"

    Mungu haruhusu uasi, ni mapungufu ya binadamu. ALIJUA binadamu ataasi, hukuruhusu.

    ReplyDelete
  3. Is it true that,Mtwara was about to be denied of its natural gas? How is possible, I can't imagine, water can get out of a well without spilling around the well rim.

    ReplyDelete
  4. Kwanini yote hayo hayakufanyika mapema kabla ya vurugu kutokea? Dharau.........,na dharau inazaa Kiburi........,Kiburi kitazaa Ubabe......., na Ubabe utazaa Mapambano! na ndicho kilichotokea!Bubu akizidiwa,naye pia huzungumza!Tujifunze kutokana na makosa ya nyuma!

    ReplyDelete
  5. 'Bubu hutaka kusema mambo yanapo mzidia'

    ReplyDelete
  6. Wakulaaniwa hapa ni wabunge ambao waliunga mkono hoja bungeni na wakapewa semina bungeni lakini elimu hiyo waliyopewa bungeni hawakuirejesha kwa wapiga kura wao. Wabunge wa mikoa hiyo walipelekwa mpaka nchi za nje kujionea manufaa ya gesi kwa jamii na ilikuwa wao waelimishe wapiga kura wao. Wala hawapingi gesi kuja Dar, tatizo ni tofauti kubwa ya kipato baina ya aliyenacho na asiyenacho.Vugu vugu la uasi limepamba moto hasa kufanya nchi isitawalike kwa kueneza uchochezi.Falsafa ya " Nalitote tugawane mbao"! !

    ReplyDelete
  7. ...

    Gesi ni Nishati, vipi waziri wa Nishati hakuwepo?

    Mungu Ibariki Afrika!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...