Uncle, 

 Huku kwetu Kijitonyama maeneo ya Sayansi na vitongoji vyake umeme unakatwa kama vile mtu kashika remote ya kuwasha na kuzima, yaani ni hatari hata kutumia vifaa vya umeme. Ila TANESCO wamekaa kimya hawatuelezi kitu gani kinaendelea, mtazamo wangu ni kuwa kuna mgao wa kiaina ila hawataki kutangaza. 

Cha ajabu wakianza kampeni za kukata umeme huwa wanatangaza vyombo vyote vya habari na vitisho juu, kama hilo linawezekana kwa nini ikitokea wao ndio wenye matatizo wanakaa kimya?? 

sisi wananchi tuna haki ya kujua kama ni mgao angalau tuwe na ratiba ili tujipange na vibatali na kama ni mitambo mibovu pia tujue ili tuokoe vifaa vyetu vya umeme??? wapi wahusika, maana ukipiga simu pale mikocheni wale wenzangu na mimi unaishia kuwashambulia tu hawajui hata wajibu nini? 

 Mdau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Aisee mgao upo ndugu yangu. Kama huku Kigamboni tunapigwa usiku kwa usikuunashangaa tu feni imekata joto jingi hafu unarudishiwa saa 12 asubuhi. Imbombo ngafu...Tanesco fungukeni kama upo upo tu, ila hata waipotwambia tujue mgao upo..

    ReplyDelete
  2. Ni kweli bwana,mimi mwenyewe ni mkaaji wa kijitonyama, hili tatizo la umeme limekuwa kero sana,sielewi kuna tatizo gani maanake imekuwa kama ni kitu cha kawaida kwa Tanesco kukata na kurudisha umeme ghafla kitu ambacho ni hatari kwa vifaa vyetu vya majumbani.tafadhali tunawaomba wahusika walitizame tatizo hili kwa mapana,

    ReplyDelete
  3. POLENI SANA KAMA MNADHANI KUNA SHIRIKA TANESCO ILISHAJIFIA ZAMANI YAMEBAKI MAKAPI YAKE TU MIE ZAMAAAANI NILISHANG'OA NA WAYA ZAO NATUMIA SOLAR YANGU NA GENERATOR YA KATI KWA HAHITAJI MAKUBWA MARA MOJA MOJA NINA MWAKA WA 4 SASA SIJAWAHI KULALA GIZA MIMI NA FAMILIA YANGU NA MAISHA NI BORA KULIKO KUWA NA TANESCO WEKEZENI KWENYE SOLAR NDUGU ZANGU ACHENI UMEME WA MAZOEA WA SHIRIKA LILILOJIFIA.

    TATIZO LETU WATANZANIA NI WATU WA KULALAMIKA SANA SIO WA KUTAFUTA UFUMBUZI WA MATATIZO YETU MIMI NILIKAA CHINI NKAONA NITAFUTE UFUMBUZI WA TANESCO NA MAJI PIA NIMECHIMBA KISIMA KIREFU MAJI KWANGU NI KAMA MTERA 24/7.

    SASA NINAFANYA UFUMBUZI WA MWISHO WA KUWA NA BOTI YANGU NDOGO YA KUINGILIA MJINI KUPITIA BAHARINI MPAKA PALE FERRY AU POSTA YA ZAMANI NIFANYE SHUGHULI ZANGU MJINI NIKIMALIZA NAONDOKA NA BOTI YANGU KURUDI ZANGU TEGETA NA NIMESHAANZA KUISANIFU HIYO BOTI YA UWEZO WA KUBEBA WATU MPAKA 10 TU NA 1/2 TANI YA MIZIGO INANITOSHA HII NI KUONDOKANA KABISA NA ADHA YA BARABARANI NA KUAMKA SAA 10 ZA USIKU KWENDA MJINI TU MAHALI PA DK 10 NIKITUMIA BOTI YANGU.

    ReplyDelete
  4. sio umeme tu! yaani na maji mikocheni A hatuna kabisa mwezi wa 2 sasa ukiuliza Dawasco wanasema ma Engineer wanashughulikia lkn wapi.

    Dawasco please mtusaidie tunateseka

    ReplyDelete
  5. tunapata tabu sana wakazi wa sayansi knyama imezidi kila siku wanakata

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...