Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipunga mkono kuaga baada ya kupanda treni stesheni ya Dar es alaam tayari kuelekea  Kigoma ambako sherehe za miaka 36 ya chama hicho tawala zitafanyika kitaifa mwaka huu
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipanda treni kuongoza msafara wa Sektretarieti  kwenda Kigoma kutoka Dar es salaam jioni hii
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dkt Asha-Rose Migiro akipunga mkono baada ya kupanda treni kutoka Dar kwenda Kigoma leo
Ndugu Kinana, Dkt Migiro na Ndugu Nape Nnauye  wakiwaaga wana-CCM na wananchi akwa jumla katika stesheni ya Dar es salaam kabla ya kupanda treni mjini Dar es salaam kwenda Kigoma leo
WanaCCM wakimuaga Ndugu Kinana na msafara wake kutoka stesheni ya reli Dar es salaam kwenda Kigoma. Picha zote na Bashir Nkoromo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Vema nao watajionea adha za reli ya kati.

    ReplyDelete
  2. Hawataiona adha. Mana wamepanda baada ya kazi ya Mwakyembe ya ukarabati kuanza na hiyo ni kampeni wanaifanya eti. Sijui kwa nini hawakupanda wakati Chenge ni waziri wa wizara hiyohiyo na akatuletea matapeli wa kihindi?

    ReplyDelete
  3. Je Watarudi kwa Treni???

    ReplyDelete
  4. Che GUevaraJanuary 26, 2013

    CCM mnashindwa nini kuwapiga chini mafisadi ambao ndio wanawapa jeuri CHADEMA kutusema? Au kila kiongozi ni MCHAFU hivyo wa kumsema mwenzie hayupo?

    ReplyDelete
  5. Mhe.Nape Nnyauye,
    Mhe.Abdulrahman Kinana,
    Mhe.Dr.Asha-Rose Migiro,

    CCM NYUNDO YA CHUMA!

    CCM piga nyundo CHADEMA kwa pigo moja kubwa lenye mshindo na nguvu imeguke vipande vipande!

    ReplyDelete
  6. walilipa nauli lkn?

    ReplyDelete
  7. HAPANA SIO ADHA WAMEKWISHA FANYA UTAFITI WAMEONA IKO SAFI HIYO SI KAZI YA JEMBE MWAKYEMBE WAJANJA HAO NDO WANATAKA KUGEUZA NI KAZI YA CCM HIYO NA SIO JEMBE NGUVU ZAKE JEURI HAO UTAWAWEZA LAKINI HATA MKIENDA KWA BASIKELI 2015 HAMNA CHENU WAJANJA NYIE CCM.

    ReplyDelete
  8. Viongozi wasafi wachache walishamwagwa chini,we angalia viongozi waliokuwepo kabla ya huu mtandao wa mafisadi kuchukua nchi. Unaona kashfa( epa,uswissi etc.) zimeanzia awamu ya tatu na nne. Huoni Mzee Mwinyi wala baba wa taifa wana akaunti uswissi wala tuhuma hizo.

    ReplyDelete
  9. Huu ndio uongozi tunao utaka wa kuweza kutufikia wananchi wa kawaida katika usafiri wa Treni!

    ReplyDelete
  10. Hakuna kitu,mshindwa kudhibiti mafisadi.hamuwasikilizi wananchi mnafanya mambo kwa mabavu mpaka mnasababisha vurugu.mnalindana sana katika madaraka yenu.tunaona watu wachache wakichapa kazi wakati wengine wanafanyakazi kwa itikadi ya chama ili waonekane.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...