MAREHEMU MZEE ESMAIL MANAMBI CHOKA
( SEPTEMBA 06, 1947 - JANUARI 23, 2011)

Hatimaye siku , miezi imepita hadi hii leo ambapo imetimia miaka miwili (2) tangu ulipofariki bila ya sisi kutarajia Alfajiri ile ya siku ya Jumapili, Januari 23 , 2011.

Kwetu sisi kifo chako kimetuachia butwaa na hali ya kutoamini kilichotokea na majonzi endelevu kwa kipindi chote cha hiki cha miaka miwili.

Hakika tumezikosa bashasha zako , busara na hekima zako na kwa hivyo basi unakumbukwa sana na Mama yako Mzazi ( Bi Hafsa Issa Kihenya), Wadogo zako ( Issa, Midladjy na Mwajelah) Watoto wako wapenzi Manambi, Masayanyika, Usamah, Natasha, Bahati,Salhina, Himidi, Jamilu, Hawa na Buhari pamoja na Ndugu, Jamaa na Marafiki lukuki.

Ingawa kimwili hauko nasi , lakini sisi tunaamini kuwa kiroho uko nasi kutokana na misingi bora ya kimaisha uliyotuachia tuizingatie na kuifuata.

Tutaendelea kukukumbuka daima siku zote za uhai wetu, wakati huo huo tunakuombea Mwenyezi Mungu aendelee kuiweka roho yako mahali pema peponi.- Amina!

INNALILLAH WAINA ILLAHIY RAJOOUN!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...