MAREHEMU MZEE ROBERT LUCAS JAKA
Hatimaye siku , miezi imepita hadi hii leo ambapo imetimia mwaka mmoja (1) tangu ulipofariki mchana ule wa siku ya Jumapili, Januari 22 , 2012.
Japokuwa haupo nasi hapa duniani lakini tupo nawe Kiroho kwa kuendeleza mema yote uliyotufundisha na kutuasa.Tunakukumbuka kwa Upendo, Busara, na Ukarimu uliokuwa nao kwa familia na marafiki.
Daima unakumbukwa sana na watoto wako wapendwa,wapendwa wajukuu zako, ndugu zako, wanajumuiya, majirani, jamaa na Marafiki zako wote.
Tutaendelea kukukumbuka daima siku zote za uhai wetu, wakati huo huo tunakuombea Mwenyezi Mungu aendelee kuiweka roho yako mahali pema peponi.
-RAHA YA MILELE UMPE EH BWANA NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE ROHO ZA MAREHEMU MZEE ROBERT JAKA IPUMZIKE KWA AMANI
Rest In Peace ,Mzee Jaka!Ewe Muumba wa Vyote,uwape Nguvu ya kustahimili vishindo vya Upweke familia ya Mzee Jaka,wapate nguvu mpya ya kusonga mbele,na kuyakubali yaliyopita kwamba ni sahemu ya maisha,kwani,kila kilichozaliwa na mwanamke kwa uwezo wake Mungu,lazima kitarudi mavumbini!Siku za mwanadamu hapa duniani zimehesabiwa!Sisi tulimpenda sana ,lakini Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi,Uamuzi wake hauna makosa!Mzee Jaka atakumbukwa daima kwa wema wake na unyenyekevu wake!Tuzidi kuomba,apate uzima wa milele,amina!
ReplyDeleteMungu amlaze Baba Mzee Jaka Mahali pema na apumzike kwa amani.
ReplyDelete