Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe (kulia) akionge na Mbunge wa Korogwe Mjini Yusuph Abdallah Nassir katika viwanja vya Bunge leo Dodoma.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa (kushoto), Mbunge wa Viti Maalumu Margaret Sitta(wa pili kushoto) akifuatiwa na Waziri wa fedha William Mgimwa(mwenye miwani)pamoja na Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia(kulia) wakibadilisha mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo , baada ya Mbunge James Mbatia kuwaslisha hoja yake binafsi kuhusu Udhaifu ulioko katika sekta ya Elimu nchini.
Mwanasheria Mkuu Mkuu wa Serikali Mh. Jaji Frederick Werema (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Wazir wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa akionyesha baadhi ya vitabu vinavyotumika mashuleni alipokuwa akijibu hoja mbalimbali zinazohusu elimu baada ya Mbunge wa kuteuliwa wa NCCR- Mageuzi James Mbatia kuwakilisha hoja yake binafsi ya Udhaifu ulioko katika sekta ya elimu nchini
Mbunge wa Iramba Magharibi Mwingulu Nchemba (kulia) akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari leo Dodoma katika viwanja vya Bunge.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Angellah Kairuki(katikati) pamoja na Mbunge wa Viti maalumu Ester Bulaya(kushoto)katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mbatia vipi siku hizi?

    ReplyDelete
  2. Mkataba hauwezi kuwa siri kwa Umma!! Ni kipi kinachofanywa kuwa siri kama ukweli katika mkataba husika ni dhahiri kwamba ni kwa ajili ya manufaa ya Umma wenyewe!! Ni nani hasa anayefichwa kuhusu hicho kinachotajwa kuwa ni siri kubwa?! Je ni huyo huyo mtanzania aliyeridhia mwenyewe kuwaweka madarakani?! Au ni majirani zetu, kwa maana ya nchi zinazotuzunguka pamoja na zile za mbali?! Kama ni mimi mwananchi ndiye ninyimwaye fursa ya kufahanmu kuhusu makubaliano katika mikataba, je mnafanya hivyo kwa manufaa ya kundi gani lenye dhamana ya kufahamu yaliyo sirini?! Kwa kiasi kikubwa dunia sasa imebadilika sana, mkubali msikubali, watu sasa wana ufahamu wa hali ya juu sana kuhusu haki na maslahi yao mengine ya msingi, mwenye elimu kubwa ya darasani na ile ya kawaida ya msingi na sekondari, wote hao sasa nim waelewa na wamekuwa ni kitu kimoja. Ifahamike kuwa fikra nyingi zinazofikiriwa na watawala wetu wa zama hizi zimepitwa na wakati na zinafananishwa na zile za enzi za watemi na watawala wengine wa jadi/mkoloni. Mfano mdogo ni kwamba, historia inaeleza kuwa mtawala mmoja wa jadi huko Kilwa kisiwani aliingia mkataba na mkoloni kuiuza Kilwa kisiwani kwa makubaliano kwamba mtemi/matawala huyo wa jadi apatiwe shuka yenye ukubwa sawa na kisiwa hicho. Kwahiyo ni lazima mwananchi wa sasa apewe fursa ya kujidhirisha kama je mikataba hii ya sasa haifanani na ile ya kijinga iliyofanywa na watemi wetu pamoja na mabwana wa kikoloni!! Siku zipo, nazo haziko mbali zinakuja ambapo nyie watawala mtaisababishia nchi hii matatizo makubwa ya ukosefu wa amani na utulivu, kwa kawaida fikra na mawazo havigandi isipokuwa hubadilika kutoka kizazi hadi kizazi, vivyo hivyo kwa ujasiri, utayari na hata uamuzi, wito wangu ni kwa wote waliopewa dhamana kutawala nchi hii kubadilika kifikra. WEKENI MIKATABA YOTE MEZANI AU KWENYE MAKTABA MAALUM, MAHALI SALAMA AMBAKO MWANACHI YEYOTE ATAKAYETHIBITIKA KUWA NI RAIA MTANZANIA ATAKUWA NA UWEZO WA KUISOMA KWA KUZINGATIA TARATIBU ZITAKAZOWEKWA. KUMBUKENI KUWA NYIE VIONGOZI HII NCHI SIYO YENU, MLICHOPEWA NI DHAMANA TU YA KUTAWALA, UMMA UNA UAMUZI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...