Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakusudia kuwatumia wataalamu wa Kitanzania walioko ndani ya nchi na wale walioko ughaibuni (Diaspora) katika kutekeleza mipango yake kadhaa yenye umuhimu kwa Taifa.

Hapo awali, Serikali iliwatumia zaidi wataalamu kutoka nchi nyingine, ambapo kwa sasa lengo ni kuona kwamba wataalamu wa nchi nyingine wanatumika pale tu ambapo wataalamu wa Kitanzania walio ndani na nje ya nchi hawajapatikana kufanya kazi husika.

Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali itapenda kupata wataalamu wa Kitanzania kwenye maeneo yafuatayo:-

(i)                             Mfumo mzima wa utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na usambazaji wa gesi asilia  na mafuta.
(ii)                          Kuimarisha matumizi salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuboresha utendaji wa Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi.
(iii)                        Kuboresha utekelezaji wa malengo ya Serikali na kupima matokeo kupitia mfumo unaokusudiwa kuhakikisha tunapata matokeo  makubwa na ya haraka katika maeneo ya kipaumbele na kimkakati katika maendeleo ya Taifa.

Wataalamu watakaojitokeza na kukubaliwa kufanya kazi Serikalini katika maeneo haya, watafanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi, lakini inayoweza kuongezwa iwapo utendaji utaridhisha.

Mwito unatolewa kwa Wataalamu wa Kitanzania popote walipo, ughaibuni au ndani ya nchi, kujitokeza na kuleta wasifu wao (CV’s) pamoja na maelezo ya kwa nini wanafikiri wao ni aina ya watu tunaowatafuta.  Tumia anuani ifuatayo:-


Katibu Mkuu Kiongozi                                                                        
Ofisi ya Rais, Ikulu
S.L.P. 9120
DAR ES SALAAM.
E.mail:chief@ikulu.go.tz


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

 1. Naomba mtafsiri huu waraka kwa kiingereza maana siku hizi kuna maneno mengi mapya ya kiswahili. thank you

  ReplyDelete
 2. nafikiri njia nzuri ya kuwarudisha wataalamu ni kuweka uraia wa nchi mbili kama vile zilivyofanya baadhi ya nchi duniani

  ReplyDelete
 3. Naipongeza Serikali yetu kwa hili, Katibu Mkuu hongera kwa kazi yako tunaifahamu huna budi kupongezwa na iwe hivyo naamini kuna wataalamu wengi sana Ughaibuni. Ninaomba wataalamu pia wajitokeze kwa wingi kuisaidia nchi yetu. Heko serikali ya Kikwete, patriotism ni suala la msingi katika kuleta maendeleo ya nchi yetu

  ReplyDelete
 4. This is so good...good job Katibu Mkuu. Wayahudi walishaanza hivi vitu miaka mingi na vimewasaidia sana. Watu walioko nje ambao ni watanzania wataliletea taifa faida kadhaa ikiwa pamoja na kubakiza pesa nyumbani. I'm working on my CV right now...!!
  Mdau-USA

  ReplyDelete
 5. Tafadhari ainisha maneno hayo mapya katika walaka huo tukusaidie tafsiri ndugu yetu

  ReplyDelete
 6. HII ni hatua kubwa na inastahili pongezi za dhati, Kwa kweli haya ni mapinduzi!

  ReplyDelete
 7. Naomba ufafanuzi kwenye kifungu namba tatu. Asante sana.

  ReplyDelete
 8. Ningefurahi sana endapo huu utaratibu usingekua na hata chembe ya siasa ndani yake. Maneno kama mchakato,mpango endelevu,mifumo mama na mengineo ya longolongo yasiwepo tunapoulizia hili suala limefikia wapi

  ReplyDelete
 9. hamuwezi, hawa hawatoi 10% ambazo mmezoea kwa wazungu.

  ReplyDelete
 10. Huu ni mwanzo mzuri wa mabadiliko katika utendaji Serikalini. Pongezi nyingi KMK na Heri ya mwaka mpya.

  ReplyDelete
 11. nimefurahishwa sana na tangazo hili. mhesh.Sefue nadhani sasa tunaanza kuona faida ya kuwa na katibu kiongozi kutoka kwenye diaspora!!tunachoomba kingine ni usawa wa ushiriki(Level playing field) kwenye sekta zote.ili hata wana-diaspora waweze kushiriki vizuri kwenye private sector yetu kwani kwa sasa bado makampuni kutoka kwenye diaspora hayana uhusiano mzuri na sector zetu huko nyumbani kwani kwa kuyapa usawa yatasaidia kuongeza uwazi kwenye taasisi zetu huko nyumbani.Diaspora ikichambuliwa vizuri inaweza kuongeza thamani ya raslimali zetu na hata kusaidia kukuza utalii kwa haraka.

  ReplyDelete
 12. Hii ni zuga. Katibu Mkuu Kiongozi anaweza kuwa na lengo zuri ila atakwamishwa na watendaji walio chini yake.

  Kuna kitengo cha Diaspora pale wizara ya mambo ya nje. Mkurugenzi wake ana nyodo utadhani serikali ni mali yake. Hata ukienda na tatizo dogo linalohitaji utatuzi wa haraka, utaambiwa usje kesho ama keshokutwa. Sina uhakika kama suala hili litafanikiwa. Yangu macho!!!

  ReplyDelete
 13. HAYA MLIOKO UGHAIBUNI MLETE cv ZENU: TUNAJUA WENGI WENU HUKO HAMNA CV ZA AINA HII KWANI KAZI NYINGI WANAZOPEWA WAAFRIKA WALIOKO UGHAIBUNI NI ZA KUBEBA BOX TU. LABDA KIDOOOOGO KWENYE IT NDO KUNA WAAFRIKA. HUKO KWNINGINE NI ZIRO. NGOJA TUSUBIRI CV ZENU. SIWAKATISHI TAMAA LAKINI.

  ReplyDelete
 14. SASA BALOZI UNAELEWA FIKA TULIOKO HUKU WENGIN TUNAKUWA NA VYETI BUT WORK EXPERIENCE YA MAANA HATUNA HATA KIDOGO, SASA SIJUI UNATUFIKIRIAJE KWA HILO, MANA ISIJE KUWA UNATAKA WATU WENYE 10YRS EXPERIENCE YA KAZI, BASI BORA TUENDELEE KUBEBA BOKSI TU.ILA KAMA MTAFAFANUA WAZI KUWA WORK EXPERIENCE SIO ISSUE KIVILEE, BASI MTATUPATA WENGI SANA TUNATAKA KURUDI HOME,DEGREE 1 TUNAYO, WENGINE WANAZO 2, ILA UMRI UMEENDA NA HATUJAFANYA DECENT JOBS HUKU HATA SIKU 1.

  ReplyDelete
 15. cv yangu inakuja mbiombio nije kutumikia taifa langu.....hongera Mh. Kikwete..hapo umepiga watu kitchen sink maana haijawahi kutarajiwa hii habari...

  ReplyDelete
 16. Tatizo la Diaspora bwana ni Vyeti na CV zao zimeoza. Bora Sefue umewaonea huruma. Usisahau hawa ndio wanaturingia wakija home na vidola na vipound vya box..waje tubanane

  ReplyDelete
 17. Mwaka jana tu mtaalamu mmoja wa mitambo ya kifua umeme na mifumo yake alipeleka pendekezo serikalini. Yeye yuko ughaibuni miaka mingi ktk taasisi maarufu. tena kaandika textbooks za mambo hayo. kweli si mbeba mabox. jitihada zake za kusaidia harakati za ufuaji umeme bongo hazikufika popote kwa sababu viongozi ktk ngazi zote walimpuuza. ninafahamu fika kwamba waheshimiwa wakuu serikalini wanamfahamu sana bingwa huyo.kasoro tu si mwenzao ktk 10% nadhani. secondly nadhani kama alivyosema muhongo watu wanacreate uhaba na matatizo ya umeme makusudi. kutatua tatizo hilo kutamaanisha kuziba mwanya wenye faida kubwa.
  ninachotaka kusema ni kwamba watu wengi ktk diaspora ambao ni wataalam hawapewi ushirikiano kwa sababu hawako ktk mifumo ya kibadhirifu ya wakubwa. na wanapokaribisha cv hivi wengi hawaoni uhakika wa nia ya serikali. miaka yote serikali inahimiza wataalamu wetu warudi, na wasaidie nchi yetu. lkn wanapokuja na kukutana na mambo haya wanajiona kwamba hatuwakaribishi kwa hakika bali tunawahadaa na kuwadhihaki.
  je kuna ushahidi gani mambo yamebadilika, mheshimiwa katibu mkuu kiongozi?,

  ReplyDelete
 18. Wewe anonymous wa Fri Jan 04, 11;43;00 AM 2013 unahitaki tukutoe nje uje uoshe macho huku majuu. Kila mtu anaanza kwenye box then ukipata ukazi na vibali vya kazi watu wanapandisha shule au kama ulisoma Africa unatengeneza CV unatafuata kazi. Kama hapa STATES mmulize balozi Sefue anatufahamu Watanzania tupo kwenye kila fani, lecturers, doctors, nurses, CPA accountants, teachers, scientists, IT specialists na orodha inaendeleakatika maofisi ya level zote from private to government. FUNGUA UBONGO WAKO KILA NCHI INA WATU WA LEVEL ZOTE HATA BONGO KUNA WABEBA MKOKOTOTENI MAHOUSE GIRLS DIRECTORS MINISTERS THE SAME APPLIES IN FOREIGN COUNTRIES. SIKU HIZI TUKIWA NA PARTY HATUNA HAJA YA KUHIRE MGENI DJ MMBONGO, MPAMBAJI MMBONGO, CATERER MMBONGO ANAKUPIKIA CHAKULA CHA KINYUMBANI VITUMBUA CHAPATI SIO MPAKA USUBIRI KURUDI BONGO NDIYO UKALE KISAMVU, WARECORD VIDEO NA PICHA NDIYO MAANA SIKU HIZ PARTY ZETU MNAZIONA LIVE SABABU WATU WAMEJIAJIRI. SO U NEED TO GET EXPOSED AND SEE HOW WE LIVE AND STRUGGLE TO MAKE A LIVING NOT BY CARRYING BOX

  ReplyDelete
 19. Anony wa Fri Jan 04, 06:15:00 PM 2013, kama ulinielewa vizuri nilisema wengi wenu hamjaajiriwa kwenye kazi za maana kiasi cha kuitwa msaidie nchi. Wachache wenu wanaweza. Bongo sawa kuna wabeba mikokoteni lakini hawajaambiwa wapeleke CV kwa katibu mkuu. Hata ninyi wabeba box tunawaheshimu kwani mnatoa mchango mkubwa through remitances lakini si utaalamu uliotukuka. Wazungu wameshikilia kila kitu wenyewe. Kama mna macv mazuri mbona hamji kufungua viwanda mbalimbali nchi ikaondokana na tatizo la ajira na pia tukauza bidhaa zenu nje ya nchi? Ughaibuni nilishafika lakini nilichokiona ni wabongo kuongea lugha za majigambo, kutambishiana magari na kudharauliana.

  ReplyDelete
 20. Jamaa wanaozungumzia sijui "wabeba maboksi" Anony. wa Fri Jan 04, 11:43:00 AM 2013 Au Anony. wa Fri Jan 04, 04:16:00 PM 2013 Eti hawa "jamaa wanakulingia wakija na tudola twao". Yaani inaonyesha jinsi mlivyo na mawazo mgando na ya kitoto. Rudia kauli zenu na jisikilize kwanza. Elewa maendeleo ya Taifa ni makubwa kuliko wivu wenu wa kitoto. Kila mtu anakuja na CV yake na uwezo wa elimu yake kufanya kazi basi. Mnapiga kelele kwa ndugu zenu wakati wazungu wakija mnawauzia nchi nzima, lakini kwa vile ndugu zenu ni weusi basi mnaona wana nyodo? Mungu atusaidie kwa ili.

  ReplyDelete
 21. Ni kweli wabongo ustaarabu hatuna. Hata mlioenda ughaibuni bado mna mawazo yaleyale ya kijingajinga yasiyokuwa ya kimaendeleo. Leteni CV acheni longolongo. Kama mnakerwa na longolongo za viongozi wa tz mbona hamtaki kuja na mkakati wa kupambana na longolongo hizo?

  ReplyDelete
 22. Wabongo wenzangu majibishano ya kejeri kati yetu tulioko ughaibuni na wale walioko nyumbani hayatusaidii. Wote sisi ni Watanzania na tunasitahili kuheshimiana bila kujali nani yuko wapi, anafanya kazi gani au anacheti kipi. Wito umetolewa na viongozi wetu kwenda kuchangia katika harakati za maendeleo ya nchi yetu. Wito huu ni mzuri na wenye maana kubwa sana kwani maendeleo ya nchi yeyote ile huletwa na wananchi wenyewe. Wakati umefika wa kuondokana na tabia ya kutegemea wataalamu kutoka nje. Wataalamu wengine tumepokea ambao kwa kweli hawakustahili hata kuletwa nchini kwani utaalamu wao siyo wa kuridhisha na hivyo wamekuwa wanaishi nchini kama watalii tu. Nchi yetu, ndani na nje ya mipaka yetu, ina wasomi na wataalamu wengi tu na waliobobea katika nyanja za kila aina. Kwa pamoja sisi sote ni vito vya taifa na tukishirikiana tunaweza tukaleta changa moto kubwa sana kataika maendeleo ya taifa letu. Kama wahenga walivyosema “umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu”. Kwa maoni yangu tuuchukue wito huu kwa moyo mkunjufu na tushirikiane na serikali katika kufanikisha azma yake ya kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata nafasi ya kuchangia katika gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Tanzania itajengeka tu vile tunavyoitaka kama kila mmoja wetu atashiriki katika harakati hii. Kunamo miaka ya nyuma marehemu Baba wa Taifa alisema, na nakuu, “It Can Be Done, Play Your Part”. Mimi pamoja na umri wangu kusogea mbele napeleka CV yangu nyumbani.

  ReplyDelete
 23. Namshukuru Mungu kwa hili wazo. Mimi niko Ughaibuni na ninapata kazi za kutoa ushauri wa kitaalam kwenye mashirika mbalimbali, SIDA, UNHABITAT, UNESCO, Etc.. Kama nyumbani watanipa kazi hizo.. itakuwa asante Mungu maana nilianza kuamini kuwa ile Methali ya "Mcheza kwao hutunzwa imefutika".

  Natuma CV kama ilivyoelekezwa. Mijadala ya kipuuzi kukatishana tamaa na kudharauliana sipendelei. Ila napenda kusema tu, hata wenye kutunza wazee nk majumbani Ulaya wana Utaalam kwa hiyo usidharau mtu na "box" lake.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...