Siku kadhaa zilizopita timejionea wenyewe tena kwa macho yetu Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania (TCRA) ikiamua kuingia rasmi katika Mfumo wa kurusha Mawasiliano ya Televisheni na Redio katika mfumo wa kisasa wa Dijitali kutoka ule mfumo wa zamani wa Analojia, kwa upande mwingine leo Shirika la Usambazaji Umeme TANESCO nao wameamua kuingia katika Mfumo huo wa Dijitali kwa staili yao ya kipekee kwa kupandanisha nguzo ya Umeme katika mti halisi ambao bado unamea kama jinsi taswira hizi zinavyoonesha. Taswira hii imepatikana Huko Mkoani Ruvuma, na TANESCO mkoani humo wameamua kutumia njia hii kurahisisha usambazaji umeme.
  Jionee jinsi Tanesco walivyo na teknolojia ya kisasa katika kipindi hiki cha Mwaka 2013.
 Jiulize kwa hali kama hii Tanesco wako juu kwa mfumo huu au wanajaribu nao mfumo wao mpya?.Picha na Demashonews Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

 1. Kuna siku nilimuuliza rafiki yangu (mhandisi-tanesco)huwa wananchi wanakupokeaje ukijitambulisha kama mhandisi wa umeme na unafanya kazi tanesco? Alinijibu kuwa wananchi wanaelewa kosa si la wafanyakazi, tena eti huwa wanampa moyo na kuwapongeza kwa jitihada zao binafsi za kuhakikisha huo umeme kidogo wanaupata japo kwa mgao. Kweli nimeamini, ni jitihada binafsi.

  ReplyDelete
 2. tanesco watawamaliza kwa kuwauwa hiyo style ni mbovu sana kuna siku kutakuja kutokea milipuko mikubwa na kusababisha hatari kubwa sana serikali wacheni kucheza na raia wema.

  ReplyDelete
 3. Nguzo hizi zipo Mbuji Mpya na sio Tz. kama Michu anavyodai!

  ReplyDelete
 4. Jamani kama hatuwawezeshi kwa kulipia huduma wanazotoa na kubaki kufanya hujuma lukuki ikiwemo wizi wa umeme mnataka wafanye nini? Kwanza wanastahili pongezi kwa kuwa wabunifu kiasi hicho kuliko kuona wananchi wanakosa huduma.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...