Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. kama miwa inalimwa kilombero na kiwanda cha sukari kiko hapo.

    kama migodi ya dhahabu na almasi iko shinyanga na ni ajira ya washinyanga.

    kama bwawa la kidatu na matambo wa umeme uko kidatu.

    nini kinashindikana kujenga mtambo wa umeme kusini karibu na chanzo cha gesi?

    ReplyDelete
  2. Mh. Zitto umejianika udhaifu wako kama kiongozi! Awali nilijua wewe ni mtu makini sana na mtetezi wa haki za wanyonge lakini kwa kusoma makala zako najifunza kuwa huna uelewa, si msomi mwenye kujua wajibu wake kwa jamii. Unaipotosha jamiii na athari yake unaigawa nchi na wananchi wake! Hoja unazozitoa zinaonyesha ufinyu wa mawazo ulionao na huwezi kumshawishi mtu makini ila asiyejua! Suala la damu tumechangia sote kuilinda nchi yetu! Unatukumbusha sisi wazazi wetu waliopoteza maisha yao japo hawakuwa watu wa Mtwara au Lindi. Lakini waliweka utaifa mbele na kuwa tayari kufa ili tufike hapa tulipo! Matusi ya Dar-Es-salaam nawaachia watu waelewa wazidi kukuona hufai hata huo Uraisi unaouota! Njaa, umaarufu na kiu ya madaraka! Eee Mungu tuepushe na aina hii ya viongozi uchwara

    ReplyDelete
  3. Kutoa uhuru wa kuandika mawazo potofu ya kuua umoja weut pia ni hatari. Mmiliki wa blog hii unapoteza umakini wako! Maslahi ya taifa mara zote yaweke mbele! Mungu ibariki Tanzania kwani uhuru ukizidi alisema Mwalimu hugeuka na kuwa uendawazimu. Huu ndio uendawazimu wa wenye kiu ya madaraka, umaarufu na kuona kuwa ni watetezi wa haki za watu! Kumbe ni wauaji zaidi ya Dikteta Idd Amin. Watatumaliza na taifa litaangamia!! Mungu tuepushie uchochezi na mbinu zao chafu zishindwe. Amina

    ReplyDelete
  4. Mh. Zitto mi ni kati ya vijana ninao kuheshimu sana japo kuwa hatutoki katika chama kimoja. Ila katika hili, sijaona ukitoa mawazo mbadala ya kunufaisha watu wa Mtwara na Lindi. Sana sana umeishia kuiponda taarifa iliyotolewa na serikali. Nadhani ingekuwa vyema ungejibu hoja iliyotolewa na mwandishi mmoja mapema leo. Ili kama kuwashauri ndeugu zetu wa Mtwara na Lindi tufahamu tunawashauri vipi. Maana mpaka sasa wanalalamika gas iwatendee haki, ila mbadala wa kuwaletea hayo maendeleo, moja - hawana mbili - kama wanayo, hayana uzito wa mashiko ukisoma makala ya mwandishi aliyeandika kimombo maoema leo hii. Mbadala wa kuwaletea hayo maendeleo ni upi? Mdau.

    ReplyDelete
  5. Zitto ni sahihi sana, hakuna sababu serikali kukosa kujenga bomba Mtwara.hivo ndio maendeleo hupatikana kwa kusambaza huduma kwa kila mkoa na wilaya sio kila kitu kiwe Dar. kwahili asilaumiwe Zitto kabwe kabisa, japo kuwa Rais Kikwete amejaribu kutowa maelezo ya kina. bado haijawa sababu kukosa kujenga huko.
    Mh zitto atakaye chukia na achukie upo sahihi kabisa, suala la kuligawa taifa, hili huwa ndio kimbilio lao viongozi wa juu ili waonekane kuwa wapo katika nia njema, hebu angalia mfano mdogo tu katika hospital hakuna hata vitanda lakini wao wananunuwa magari makubwa.mimi sioni sababu kwanini serikali isigawane huduma kama hizi ambazo huleta migogoro katika jamii za kiafrica.
    Serikali isipuuze malalamiko ya wananchi wa upande unaolalamika bali itazame hoja na uzito wa suala lilalamikiwalo katika jamii hii.
    Hili sio suala la kufanya wananchi waitwe mahaini,wapo katika kutafuta usawa wa maisha yao na vizazi vitokavo huko.serikali isitumie ubabe wa kuamuwa, busara itumike na mawaziri wasijione wanaitika wito wa bwana japo kuwa uhalali wa hilo litakiwalo halipo katika upande wao.hii ni nchi na nchi inataka viongozi waadilifu na waelevu katika nyanja zote.Taifa libaki kwa wote ili tudumishe amani na tuwe watu wa kuaminiana katika kujenga nchi yt.
    nawasilisha.

    ReplyDelete
  6. Mimi bonafsi nathani kuna umuhimu wa wanasiasa vijana kama Zitto kusoma historia za mataifa kama America kujua civil war (1861-1865) kati ya South and North vilitokana na nini haswa? japokuwa historia inasema vilitokana na abolishment of slavery ukweli unabaki kuwa mataifa ya Kusini 13 confederates yenye rasilimali zaidi IKIWEMO Watumwa wakati huo wakihesabika kama asets kujiona hayahitaji wenzao wa Kaskazini na kuamua kukataa wito wa kuondoa utumwa na kujitenga! Hiki ndicho tunachokianzisha hapa kwa siasa zetu uchwara kama za Zitto! Mbona hao Mtwara na Lindi hawakudai vyao kabla ya gesi kugundilika! Ni ukweli usiopingika wana Mtwara wanahitaji wanasiasa kama Zitto kuyapalia makaa yenye majivu moto!

    ReplyDelete
  7. Zitto ufai kuwa kiongongozi wala mbunge nenda kwanza somalia uone yaliyotokea uko na pia Rwanda au Burundi inaonekana wewe na chama chako mnataka kuigawa Tanzania nakuomba Amani Iliyoletwa na Mwalimu Baba wa Taifa sisi wenye uchungu wa nchi yetu atutakubali nchi ingawanyike au iwe na vita,naomba nao wanasiasa wenye akili finyu na wanasiasa ambao hawana Vision hatutaweza kukubali Ndugu zitto nakuomba wacha polojo nenda somalia ujifunze kwanza nenda somalia wewe na mbowe na dk slaa
    asante.
    mukasa

    ReplyDelete
  8. Mbona pamba ililimwa Mwanza na kiwanda cha nguo kikajengwa Dar, Shinyanga Wakachimba Almasi kiwanda cha kuchongea kikajengwa Iringa, Mheshimiwa Sugu akitoa nyimbo soko lake anauzia Dar,Ngano inalimwa arusha Mikate inaliwa dar na mifano mingi, vijiji vya mtwara na lindi sijui vinamatatizo gani, wawekezaji pamoja na serikali zimetumia matrilion ya shilingi kufanikisha suala zima la upatikanaji wa hii gesi,hawajiulizi hela imetoka wapi, na iatarudishwaje, wamesahau kuna mtu binafsi ametoa pesa yake mfukoni, jamaa ana mkataba wa muda fulani, kwahiyo lazima ahakikishe pesa yake inarudi ktk kipindi cha mkataba wake nae apate faida, Waulizeni wa Zanzibar walileta malingo miaka fulani nyuma wakataka wajitenge eti wakitegemea karafuu na kudai wabara tunawazulumu, wako wapi sasa, nani anataka tena karafuu, hiyo gesi ikiisha humu ardhini mtakimbilia wapi, au mtabaki kujivunia daraja. wamasai wamechukua kazi zenu za ulinzi, nani anataka mmakonde tena, nendeni kule, msijali jamani nyie ni watani zangu lazima tutaniane,

    ReplyDelete
  9. unajua since hii sirikali yetu inaakili sana kupita sisi tuliowachagua basi inabidi tusiseme lolote lile na kukubali chochote wanachosema. Kwa sababu mpango wao mkubwa unaokuja wa kuiamishia mbuga ya ngorongoro darisalama ambako kuna watu wengi sana na ni karibu ya vitu vyote. Mfano, foleni ambayo ni kivutio kikubwa cha taifa, miondo mbuni yake ambayo huonyesha uwezo wake wa kutopitisha maji popote pale kwa ubunifu na umahili wake mvua ikinyesha. Na ni karibu zaidi ya kambi nzuri za majeshi ambazo ziko automated kulipua mabomu muda wowote ili kuprotect wananchi amabao wanakaa karibu nazo. na ni sehemu ambayo mvua ikinyesha saaaana unajua how far are you from the rivers, na madaraja ambayo yemejengwa imara na kuto poromoka yote bali nusu na kuzuia nusu ya jiji kwenda sehemu pekee yenye mahitaji yote.... Okay ili kuijenga Tanzania inabidi kuanzia darisalama mpaka hapi darisalama ijae kabisa!!!!!!!!

    Mdau Ohio

    ReplyDelete
  10. Mie siku zote nasemaga Zito hana lolote jamani na UPEO wake ni finyu! Mtu kama huyu nae anataka URAISI si AIBU? hivi nani kamwambia watanzania tunamtaka awe RAISI wetu? kwanza ni aibu hata kumpendekeza na kama CHADEMA wakifanya hivyi nitawaona nao wote ni kama yeye! aombe awe kwanza japo Mkuu wa Wilaya!

    ReplyDelete
  11. Mheshimiwa Zitto wacha siasa za majitaka. Huko ni kujitafutia unaarufu usio na mashiko.
    Kama kweli una hakika asilimia 90 ya ufisadi ipo Dar basi simama kifua mbele toa orodha na uthibitisho kwa vyombo husika ili mafisadi washughulikiwe.
    Nakumbuka uliibua suala la fedha zinazowekwa nje ya nchi, ukaenda mbali zaidi kudai ati unayo majina, lakini ulipoombwa utoe majina hayo.....kila mtu anajua ulichojibu...Sasa usiwe mkosa uelewa japo kidogo. Fahamu kwamba viwanda vingi vinavyohitaji gesi asilia vilijengwa Dar es salaam miaka mingi iliyopita, fahamu pia kwamba mitambo mikubwa ya kupokelea umeme ipo Dar, sasa leo unapokurupuka na kudai ati gesi isletwe Dar, je tukiwaachia wao wa Mtwara wewe kwako kigoma utapata umeme wa bei nafuu? Halafu zingatia ukweli kuwa ni asilimia 14 tu ya gesi ndiyo iko Mtwara na iliyobaki ipo nje ya mikoa unayoitetea. Hapa inaonyesha wazi kuwa ukipewa nchi utaacha uchumi uanguke kwa kutaka kuwafurahisha watu kuwa wabaki na rasilmali zao. Nilitarajia ungewashauri waandae mpangomkakati utakaowawezesha wao kunufaika na mrahaba wa gesi kwa maendeleo ya mikoa yao.

    ReplyDelete
  12. We Zito chizi nini au mzito kichwani, juzi umetoa hotuba bungeni ukasema mauzo ya mazao mbalimbali kama Pamba, Katani, Korosho, Chai, Kahawa na mengineyo yalikuwa na thamani ya dola 761.1 milioni, leo unakuja tena na takwimu unasema korosho peke yake ilikua 151 milioni dola, ina maana mazao yote watanzania tunayolima na kuuza nje ya nchi korosho ndo inauzwa sana, kwa ratio ipi unayosema wewe kichwa maji, yaani mazao yoote hapa tanzania, kahawa,pamba, katani, asali, mahindi, dengu, mchele, chai,alizeti,na mengine yote yalichangia milion 610 tuu, ikiwa na maana korosho pekee ni asilimia tisini, we bwege kweli wewe. rudi chekechea, hujui takwimu za uuzaji nchini, unazitoa mitaani, kama korosho 151, unasema pamba 53, ina mana kahawa lazima 260, chai lazima 230, hapo tayari hapo jumla tayari dola 690 , ngano je, katani, ndizi, ushaniboa bwana, we chizi tu

    ReplyDelete
  13. Jamani wananchi wamechoka msiwaone wamedata wanajua mnachokifanya rudisheni pesa kwanza nje,ndo muongee,mnalinganisha enzi za mwalimu na sasa watu walikuwa wazalendo hawachakachui kama sasa.

    ReplyDelete
  14. Mh , naona, unataka kugawa taifa hili, inawezekana wakawa watu wa mtwara walikuwa na nia nzuri , ila ile walioinesha kwenye mabango ni ya kupigwa vita na ni ya kibaguzi. wangehoji mikataba na jinsi gani mapato yataingia (mgawanyo wa mpato). ningeliwasupport moja kwa moja, bt ww mheshimiwa unawatia maneno mdomoni, mabango yao hayakuonesha hivyo zaidi ya ubaguzi. Mh tunaomba kuwela utaifa mbele, umoja na mshikamano katika kuleta maendeleo, lakin siasi za kutagawa HATUZITAKI. Lete hoja ya kulisukuma taifa mbele kwa ujumla wake.

    ReplyDelete
  15. Hivi kuna tatizo gani kwa serikali kuwaeleza watanzania waziwazi,"gesiasilia na matumizi yake mbalimbali?".Watu wanachanganya mambo makuu mawili hapa.Kwanza,suala la kufua umeme utakaotakana na gesiasilia.Watanzania wa Mtwara wanahoji,na kwa hili hata mimi nitawaunga mkono,wanahoji,kwanini,"Mtambo au Kiwanda cha Kufua Umeme wa Gesi kisijengwe Mtwara au Lindi inakotoka gesi yenyewe,na kisha,umeme huo ukasambazwa nchi nzima kupitia mtandao wa gridi ya Taifa?badala ya kusafirisha gesighafi hadi DSM kupitia hilo bomba la gesi,ndipo umeme huo ufuliwe huko Dsm?"Kuna tatizo gani kuhusu hilo?Au kuna Usaliti gani katika kuhoji hilo?La,pili,kuna suala la matumizi ya gesi kwa ajili mahitaji ya majumbani(domestic consumption).Katika hili,iwapo ni nafuu zaidi kigharama(more viable costwise)kujenga bomba la gesi toka Mtwara hadi Dsm ili lisafirishe gesiasilia kwa madhumuni hayo,hakuna anayepinga.Lakini,ningekuwa mimi ndiye mwenye kauli ya mwisho,ningependekeza,Makampuni ya kujaza gesi katika mitungi,yafungue Viwanda au Ofisi zake huko Mtwara au Lindi kwa madhumuni hayo.Na kisha gesi hiyo isafirishwe hadi DSM na kwingineko itakako hitajika.Lakini,kama ni vyema zaidi kutokana na gharama kubwa za uzalishaji,kazi ya kujaza gesi katika mitungi ifanyikie Dsm,hakuna tatizo wala mjadala!Tatu,la muhimu zaidi ni kuangalia vipi gesi hiyo itaweza kutumika katika uzalishaji wa bidhaa zingine zaidi nje ya "hayo mahitaji muhimu mawili,umeme na kupikia".Tayari,serikali imetamka kwamba,kuna viwanda mbalimbali vitakavyo jengwa huko Mtwara na Lindi,kama kiwanda cha mbolea,na kile cha saruji.Na vingine vingi vitafuatia.Kwanini,serikali isitumie fursa hii,kuweka bayana "Mpango Mzima wa Utekelezaji wa Viwanda Mbalimbali"uliokusudiwa kutekelezwa katika mikoa hiyo,kwa kutaja Tarehe zake za Utekelezaji na Kukamilika kwake,ili roho za watu zitulie!Kuna ubaya gani katika hilo?Vipi watu wa Mtwara waitwe wasaliti kwa kudai "Ufafanuzi kutoka serikalini kuhusu masuala hayo yanayo gusa mustakabali wa maisha yao?".Gesiasilia isipo wakomboa wenzetu hawa waliosahaulika miaka nenda rudi toka tupate uhuru(this is a naked absolute truth),hebu niambie,"kitu gani tena kitakacho kuja kuwakomboa kiuchumi".Katika kulisema hilo,watu wasidhani kwamba,tuna nia ya kuigawa nchi,"not all"!.Tuache hizi siasa za kuganga njaa.Au kugeuzwa makuwadi wa World Bank & IMF!(you know damn well,what Um talking about!).Watanzania wote tuko pamoja katika hili,wala msidanganyike,kwamba,kuna baadhi yetu wanataka kuleta machafuko(?)au kuigawa nchi vipande vipande!this is ridiculous!nilimsikiliza Waziri mmoja,mishipa ya shingo imemvimba,akitamka bila haya,"hatutakubali(nani ?)nchi yetu imegwe vipande vipande?nani aliyemwambia tanzania hii ya leo,yupo atakayekubali kuiona nchi hii ikimeguka vipandevipande kama yeye anavyodai?acheni kupotosha madai au ajenda ya wakazi watanzania wa mtwara!get down to the real basics of the issues!Lini Mwalimu Nyerere utarudi tena?

    ReplyDelete
  16. Kama kuna jambo juu ya Mh Zitto lisemwe na siyo kumuandama na kumshambulia binafsi badala ya kuchangia hoja iliyo mbele..
    kwani kuna tatizo gani gesi hii kusafishwa mtwara!?? hebu tazameni hili Gesi isafirishwe kwa bomba kutoka Mtwara hadi Dar halafu umeme ukisha patikana usafirishwe tena Mpaka mtwara!! gharama za ujenzi wa bomba lile zinatosha kutumika kutundika nyaya za umeme pamoja na nguzo zake toka mtwara hadi dar(gharama za ujenzi wa bomba la gesi ni kubwa kutokana na uhatari wa gesi msingi wa bomba huchimbwa chini sana,kuondosha miti,kukata barabara ikibidi kuondosha majengo zote hizi ni gharama ambazo zinaweza kuepukika) sasa kwa nini kiwanda kisijengwe Mtwara halafu umeme ukasafirishwa kwa nguzo tu ambazo gharama yake ni nafuu sana ukilinganisha na bomba na tukaepuka gharama za ujenzi wa bomba hilo!!?? isitoshe watu wa huko watapata ajira na hii itaharakisha maendeleo kwani nishati mama ya uwepo wa viwanda itapatikana kwa urahisi na kupunguza uhamiaji wa ndani wa watu kuja mjini(dar)!
    Katika historia angalieni Niger Delta huko Nigeria mafuta yanachimbwa mjini kwao lakini ndio masikini wa kutupwa na matokeo yake mnayasoma kila kukicha magazetini!!sasa badala ya kumsakama Mh Zitto tazameni na uhalisia wa jambo ulivyo!!

    ReplyDelete
  17. sioni tatizo la watu wa mtwara,wako sahihi kabisa.kosa ni la serikali kabla ya kutekeleza mradi wowote lazima wadau wote wahusishwe.hawa wananchi walishirikishwa?hapa ndo umuhimu wa integrated resource management unapohitajika.michuzi usibane

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...