Makatibu wa Bunge wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika mwishoni mwa wiki wamekutana Kampala,Uganda kupitia Kanuni za vikao vyao pamoja na Mpango Mkakati wa Kundi lao ambalo ni moja ya vitengo vya Chama cha Wabunge wa Jmuiya ya Madola Kanda ya Afrika. Katika Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Makatibu wa Mabunge ya Ghana, Botswana,Uganda,Nigeria, Kenya,Afrika Kusini na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Sekretarieti ya Chama hicho iliwakilishwa na Nd. Saidi Yakubu (kwanza kushoto waliosimama) na Nd. Demetrius Mgalami (wa tatu kushoto waliokaa) na Nd. Hassan Amour wa Baraza la Wawakilishi (wa tatu kushoto waliosimama). PICHA KWA HISANI YA SEKRETARIETI YA CPA KANDA YA AFRIKA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...