Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto) akisalimiana na Mhe. Armando Emillio Guebuza, Rais wa Msumbiji mara baada ya Rais huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo. Mhe. Guebuza ni miongoni mwa Marais wanaohudhuria Mkutano Maalum wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC-TROIKA) unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 10 Januari, 2013.
Mhe. Guebuza (kushoto) akifuatana na Waziri Membe mara baada ya kuwasili
Mhe. Rais Guebuza wakati alipokuwa akiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili nchini.
Mhe. Rais Guebuza akiangalia ngoma za utamaduni (hazipo pichani) zilizokuwa zikitoa burudani kiwanjani hapo mara baada ya kuwasili.
Moja ya kikundi cha utamaduni kilichokuwa kikitoa burudani kwa Mhe. Rais Guebuza alipowasili nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Michuzi,TROIKA ni nini,naomba wanaofahamu wanieleweshe

    ReplyDelete
  2. TROIKA ni UTATU, katika jumuiya mbalimbali huwa kuna kamati ndogo zinazoundwa na nchi tatu yaani 1.Mwenyekiti wa Kamati wa zamani 2. Mwenyekiti wa Kamati wa sasa 3. Mwenyekiti wa Kamati ajaye. Kwa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC 1. Mwenyekiti wa zamani (Afrika ya Kusini 2.Mwenyekiti wa sas (Tanzania) 3 Mwenyekiti ajaye (Namibia). Kwa hii TROIKA inaundwa na Afrika ya Kusini, Tanzania na Namibia. Msumbiji imehudhuria akiwa ni Mwenyekiti wa SADC.
    johnJohn

    ReplyDelete
  3. troika in 3 kwa kirusi.inaingiana na chochoche kinachoingiliana na 3,mfano kule mido east(middle east)wanatumia troika kumaanisha E.U,U.N,U.S.A

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...