Na Abdulaziz Video.
WATU Saba akiwemo askari polisi mmoja wameuawa katika vurugu
zinazoendelea wilayani Masasi mkoani Mtwara, zikiwa zimebeba sura ya
kupinga gesi kwenda Dar es Salaam.
Muuguzi wa zamu hospitali ya wilaya
ya Masasi, Mkomaindo Fatuma Timbu amethibitisha kupokea maiti za watu
saba.
Majeruhi ambao idadi yao haijajulikana wamekimbizwa hospitali ya
misheni ya Ndanda kwa matibabu na hali bado ni tete Vurugu kubwa
zilianza majira ya saa 4 asubuhi leo baada ya polisi waliokuwa wakiendesha
pikipiki kumgonga mtu na kukataa kutoa ushirikiano,Hata hivyo hoja
hiyo ilihamia kwenye gesi na kundi la vijana mara moja walivamia nyumba
ya mbunge wa Masasi, Mariam kasembe na kuiwasha moto, pamoja na magari
mawili.
Aidha vijana hao walivamia nyumba ya Anna Abdallah na
kuiteketeza kwa moto,kabla ya kuivania ofisi ya CCM wilaya na kuichoma
moto pamoja na magari matatu.Hasira za wananchi hao zilifika kituo
kidogo cha polisi kilichopo Mkuti na kukichoma moto, baadae walichoma
moto magari matano ya halmashauri ya wilaya.
Pia walichoma moto ofisi
ya elimu ya halmshauri ya wilaya Masasi vijijini, kabla ya kuichoma
ofisi ya maliasili.
Polisi kutoka maeneo mbalimbali yandani na
nje ya mkoa inadaiwa walitumia risasi za moto na kusababisha vifo vya
watu Sita huku polisi akidaiwa kuuawa kwa kupigwa na wananchi….
serikali iko wapi jamani?jamani nchi zenye vita kubwa nazo zilianza kama sisi tunavyofanya leo.serikali isipokuwa thabiti basi ile sifa ya kisiwa cha amani itakuwa historia.tuache siasa tujenge nchi.unachoma magari ya halmashauri ili iweje?maendeleo hayawezi kuja kwa utaratibu huu.
ReplyDeleteJamani mbona namiss Mchonga kwenye mambo kama haya, yaani kama namsikia "nyinyi vijana, mnaleta mambo gani...." sasa hii gesi ilikuwepo Mtwara tangu dunia iumbwe, hawa wenzetu waliilalia na hawakufanya chochote juu yake, leo mtaalamu kaja kawasaidia kuitoa na kuibadilisha kuwa umeme sasa wanapigana na hatimae kufa bila kuonja baraka Mungu aliyowawekea tangu dunia iumbwe, HEKIMA iko wapi hapa?? Kwani hiyo gesi ikifunguliwa na kuachiwa kwenye hewa ya Mtwara watafaidika nini? Si lazima iende na kubadilishwa iwe umeme? Tulizaneni jamani ili mfaidike na baraka za Mungu... HEKIMA, AMANI na UMOJA ndio ngao yetu waTanzania... Mungu endelea kuibariki Tanzania na watu wake.
ReplyDeleteInasikitisha kuona gari ls kubebea wagonjwa ambulance (picha na2) nalo likichomwa. Sasa hawa jamaa wakiugua au wake zao wakiugua au kuwa wajawazito watabebwa na nani! Tuwe waelewa tuache fikra mbovu za kuunguza magari ya serikali kwani sasa gari jingine halitapatikana na wananchi wataendelea kuteseka hadi hapo fedha zao za kodi zitakapo tosheleza kununua gari jingine la wagonjwa
ReplyDeletePole sana wale walioumia na kupotelewa na ndugu katika hili janga..
ReplyDeleteHapa naelewa Serikali lazima ibebeshwe lawama, I hate to do it ila ndo UKWELI.
Kinachokosa katika mgogoro mzima huu ni COMMUNICATION nzuri. Serikali imeshindwa nini kukaa chini na hawa watu kuwasikiliza??? Maelezo kama "Kahawa zinalimwa Moshi na watanzania wote wamefaidika" HAYATOSHI KABISA
All the stakeholders need to sit down and discuss amicably, hawa wanaofanya hivi wanahitaji assurance watafaidika vipi? they have a point.
Hiyo ni Gesi. Je ikija Petroli? Nigeria itakuwa nafuu.
ReplyDeleteShida ninayoion hapa siyo hii mali Ghafi. Watu hasa vijana wamechoshwa na huu umaskini uliyo kidhiri na Ufisadi wa wenye nacho. Ndiyo maana Mzee wetu, Babu yetu, Baba Yetu Mwl. Nyerere alisema wacha ikae chini hadi watu wangu wapate akili ya kuililiki.
sasa tunavuna na bado tutavuna!
mimi nakumbuka rafiki yangu kutoka AUSTRALIA miaka mitano iliyopita aliniambia kwa kifupi kwamba hakuna nchi ya amani afrika ,ni kwamba penye amani sasa kesho mapanga nakadhalika. Je TANZANIA amani maana yake nini?amani si lazima kupigana vita bali wananchi kufa ovyo hapo hakuna amani.
ReplyDeleteStupidity Idiot you name it huwezi kuniambia unachoma gari la wagonjwa kwa kudai gesi Stupid
ReplyDeleteKIKWETE USISAHAU KAMA WEWE NI MWANAJESHI WATU WAKO UMETAWALA KIRAIA WANA KOSA NIDHAMU SASA RAFIKI YANGU USHAURI MMOJA NAKUPA TOA MASUTI YAKO VAA MAGWANDA PINDUA SERIKALI YAKO MWENYEWE IWE YA KIJESHI HALAFU HAO WENYE NDOTO ZA 2015 URAISI JASHO LIWATOKE UWEKE MIKAKATI KUWARUDISHIA NCHI RAIA 2020 BASI BILA HIVYO FYOKO FYOKO ITAKUA KILA SIKU MICHUZI USIBANIE KIPANDE HIKI WACHA WATU WASOME NA HUYO RAISI AISOME HII
ReplyDeleteNidham imeshuka sana kwa wananchi towards vyombo vya ulinzi, hii inatokana na upole wa mh mkuu wa nchi, huruma yake na upendo kwa raia wake unamcost, naamini wapo wachochezi wa haya yote na hasa wanaotaka urais 2015 kwa nguvu zote. Waliwahi kusema nchi hii haitatawalika, sasa naona wanaendelea kutekeleza azma zao. Tuwe macho
Deletesiasa za vyama vingi ndizo zinazopandikiza chuki miongoni mwa wananchi na hatimae vurugu tu maendeleo hatufanyi...huwezi kusema serikali kila wakati ikae na wananchi waelewane hakuna kitu kama hicho kuna wakati maamuzi lazima yafanywe na kutekelezwa kama ni kwa manufaa ya wananchi wote.
ReplyDeleteJK kweli alichosema mdau ni kweli kabisa piga GWANDA.
ReplyDeleteHAPO CHADEMA MMEFURAHII!!!! MWOGOPENI MUNGU NINI!!! MMKEKUWA MKISEMA NCHI AITA TAWALIKA NA DAMU LAZIMA IMWAGIKE, MMEKUWA MARA KWA MARA MKIUBIRI HIVYO, MIMI NACHUKIA SANA, NINYI NI BOMU KUBWA ILA WANANCHI HAWAJAWAELEWA VIZURI, NI VIBARAKA WA WAKOLONI ENDELENI KUCHOCHEA MAASI , MUNGU ATA WALIPA HAPA HAPA. SIASA ZA KINAFKI ZISIZO JALI UHAI WA WATU.
ReplyDeleteMzigo wa mwenzio ni kanda la sufi waswahili walisema! leo nimeamini maana kuna mchangiaji hapo anasema 'the most idiotic people in this world, its is a shame'
ReplyDeleteSince you do not know what really is their problem then you are free to assume whatever you want to assume.
Umemuhoji yoyote hapo akakwambia wanafanya wanayofanya kwa ajili ya gesi???
Huyu aliyeshauri mapinduzi ya kijeshi, mawazo yake ni bora hata ya wale watu wa Masasi, maana hayana mantiki kabisa. Tuwe tunatoa ushauri wa maana hata kama tuna jaziba busara ni muhimu kutumika.
ReplyDeleteBusara za MH. MIZENGO PINDA zingekuwa zinaheshimiwa na kufuatwa Tanzania ingeendelea kuwa kisiwa cha amani. Kumbukeni alivyoshughulikia suala la albino! Nakutakia kila la Heri katika juhudi zako ulizozianza kushughulikia mzozo huu wa gesi. Ushauri- “usiwe unachelewa hadi maafa yatokee ndipo unajitokeza” ‘be proactive’
ReplyDeleteYou may assume, they are stupid and idiots only to find you are the most of both.
ReplyDeletepoleni Mtwara.Elimu Kwanza
ReplyDeletewewe ukiwaita wao wahaini,wao watakuita wewe mkoloni!jamani busara zimekwenda wapi?kusini walivumilia kwa muda mrefu sana "economic stagnation" ili kutoa nafasi kwa Ukombozi wa Msumbiji na Afrika ya Kusini!Viwanda vyote vya Korosho "kwishnei!",bandari za Lindi na Mtwara "mufilisi!",mazao wanakopwa!jamani,hebu tuwe wasikivu kidogo na tujiulize,of all the places in Tanzania,kuna watu wakarimu na wapole kama watu wa Mtwara na Lindi? no,no, tumekosea mahali...hebu tukubali makosa,na tujirekebishe!ubabe utalipwa kwa ubabe!upole utalipwa kwa upole!as simple as that!Punda naye akishachoka mizigo hugoma kutembea,hujalijua hilo?
ReplyDeletemungu saidia jamaa hii ya kitanzania, kwani wanacheza na moto
ReplyDeleteJAMANI WATANZANIA,TUSIKILIZANE KWANZA ,SERIKALI ITAMBUE KUWA MOJA NDANI YA RASILIMALI ZOZOTE ZILIZOPO MTWARA RASILIMALI YA GESI NDIO INGEWEZA KUWANUFAISHA WANAMTWARA MARA MOJA,KIUCHUMI,KIJAMII,KISIASA NA KIMAZINGIRA,ZAIDI NISEME SERIKALI HAIKUWA NA HAJA YA KUISAFIRISHA ILE GAS TO DSM BADALA YAKE MAKAMPUNI WAWEKEZAJI ZIWEKEZE NDANI YA MKOA ILE ILI NA YENYEWE IPIGE HATUA MBELE KAMA DSM,ARUSHA,MWANZA etc.na wanamtwara wananufaike nayo...la sivyo madhara yatazidi kuwa makubwa mno.
ReplyDeleteHIZI VURUGU KUNA MKONO WA CHADEMA HAPA, TUWE WAZI WALA TUSIZUNGUKE MBUYU.
ReplyDeleteNDUGU 'WATANZANIA' MIMI NAONA KUWA MUAMKO WA WATU WA MTWARA NA WALE WENGI WANAOONA KUWA WANANYIMWA HAKI NI MATOKEO YA ELIMU NA KUPUNGUA KWA VIONGOZI WANAOKUBALI MAMBO BILA KUULIZA MASWALI. MASWALI KAMA KWANINI ARUSHA, IRINGA, MBEYA, SONGEA, MWANZA, BUKOBA, TUNDUMA, KYELA DAR ES SALAAM KUNA MAENDELEO MAKUBWA WAKATI KIGOMA, MTWARA NA LINDI HAKUNA????WAUZA BIASHARA ZA MKONONI HAPA DAR NI MACHINGA..KWANINI SIO WAHAYA??? HAYA SIO MASWALI YALILOVUMBULIWA NA CHADEMA. UKWELI NI KUWA AU KWA AAJILI YA MAZAO, BARABARA NA VIWANDA NDIO KULICHOCHEA MAENDELEO YA MAENEO HAYO. WAUZA BIASHARA ZA MKONONI HAPA DAR NI MACHINGA..KWANINI SIO WAHAYA??? MTWARA WANAHAKI YA KUDAI MANUFAA YA GESI YAWAFAIDISHE WAO KWANZA KWANI MAHOTELI YA UTALII YALIOKO ARUSHA NA DAR HAYAKUJENGWA MTWARA ILI YANUFAISHE WATU WOTE! HUO NDIO UKWELI. NAUNGA MKONO KUWA WATANZANIA WENZANGU WA MTWARA WAFAIDIKE KATIKA SWALA HILI ZAIDI YA MTU MWINGINE HASA KATIKA KUWEKA MAZINGIRA YA KUCHOCHEA MAENDELEO YAO. KUDAI HAKI HAKUNA MIPAKA...SERIKALI IKISUBIRI MPKA WANANCHI WADAI HAKI KWA NGUVU MATOKEO YAKE NDIO HAYO... ANAKUFA MTU ITAKUWA KUCHOMA GARI LA WAGONJWA??
ReplyDelete