Balozi Tuvako Manongi akifungua semina ya siku mbili kuhusu uzuiaji wa mauaji ya kimbari, akifungua semina hiyo, Balozi amewaeleza washiriki kwamba kila serikali na kila raia anao wajibu wa kugundua na kutoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika kuhusu viashiria au dalili ambazo kama hazitadhibitiwa mapema zinaweza kusambisha mauaji ya kimbari au mauaji ya halaiki katika nchi husika. Pembeni yake ni Bw. Adama Dieng, Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uzuiaji wa maujai ya Kimbari.
sehmu ya washiriki wa semina hiyo kutoka Balozi mbalimbali za Umoja wa Mataifa pamoja na wataalamu kutoka Asasi zisizo za kiraia, semina hiyo ili kuwa ni ya kuwajengea uelewa mpana washiriki kuhusu suala zima la mauaji ya kimbari na ulinzi wa raia. wanasema walifundishwa pamoja na namna ya kubaini viashiria vya machafuko, namna ya kukusanya taarifa, mikataba ya kimataifa kuhusu mauaji ya kimbari, uzuiaji wa mauaji ya kimbari na adhari na matukio yao kiuchumi, kijamii na kimaendeleo kwa na wananchi wa nchi husika.
Vitu kama vuguvugu za Harakati za Gesi za Mtwara zinaweza kuwa chachu kwa baadhi ya wengine kutumia nafasi hiyo kufikia malengo.
ReplyDeleteVITU VYA MSINGI VYA KUFANYWA ILI KUEPUKA KUPELEKEA HAYO MADHARA KUTOKEA NI:
1.Kushirikisha watu wa kawaida katika mambo yanayohusu wengi, na sio mambo ya watu yaamuliwe na wachache.
2.Kutoa fursa ya majadiliano na maridhiano panapotokea watu kuwa na tofauti katika jamii.
3.Kutekeleza ajenda zilizofikiwa baada ya vikao vya maridhiano pia kuwa na ufuatiliaji wa mara kwa mara kuhakikisha yanatekelezwa.