Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kushoto mwenye kaunda suti), akimkabidhi baadhi ya misaada ya vyakula mke wa mzee Lenati Semgweno ( hayupo pichani) , Maria Lucas ( kulia) baada ya Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo alipoitembelea familia hiyo kuijulia hali Januari 10, mwaka huu , Kijijini Makuyu, Kata ya Mvomero , Wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( wenye kauda suti) ,akiwa amekumbatia Joseph Herman miongoni mwa watoto watano wenye ulemavu wa viungo na mtindio wa ubongo wa familia ya Lenati Semgweno ( hayupo pichani) pamoja na baadhi ya ndugu na jamaa wakiwemo na watendaji wa Serikali ya Wilaya ya Mvomero, wakati Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo alipoitembelea familia hiyo kuijulia hali Januari 10, mwaka huu Kijijini Makuyu, Kata ya Mvomero , Wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( mwenye kaunda suti), akimkabidhi mkate , mtoto wa kwanza wa mzee Lenati Semgweno , Charles Lenati ,mlemavu wa viungo na mtindio wa ubongo , wakati Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo alipoitembelea familia hiyo kuijulia hali Januari 10, mwaka huu Kijijini Makuyu, Kata ya Mvomero , Wilayani humo.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.
Hongera saa ndugu. Toa sana kwa hawa ndugu.
ReplyDeleteWananchi wako wenye nguvu wape akili ya kutafuta wao wenyewe.
Hacheni kumkufuru Mungu kwa kufanya siasa kwenye shida na umasikini wa binadamu. Kumbukeni kwa Mungu hamtaweza kuleta siasa zenu.
ReplyDeleteUsitoe kwa ajili ya siasa. Unafanya hivyo kwa kuwa unapiga picha za hao walemavu ili upate umaarufu wa kisiasa! Hilo si sahihi hata kidogo, wewe kama mbunge ni wajibu wako kuwaangalia na kuwatetea hao sio ofa kama unavyofanya na kuppiga picha nao.
ReplyDeleteNdio maana siwezi kuwa mwanasiasa,najua hao ndugu zetu wanashida za kweli haswa ambazo zinahitaji kupewa ufumbuzi na si kuwafanyia watu maigizo wakati unajua unatoa kwa malengo mengine kabisaa. Mungu tusaidie tuweze fahamu mbivu na mbichi.
ReplyDelete